Kama kuna wanachama wa CHADEMA wanataka kuchallenge uongozi wa Mbowe, kihalali, kwenye uchaguzi wa ndani, kwa nini unawalazimisha waende ACT?
Nilikuwa nawasema vibaya sana wanaharakati wa mitandaoni ambao si wanachama wa CHADEMA waliokuwa wanamkataa Mbowe kwa kusema "Mbowe Must Go". Hoja yangu kubwa ilikuwa kwamba wanaharakati hao hawana uhalali wa kutaka kumuondoa Mbowe kwenye uenyekiti, kwa sababu hawana hata uanachama (majority). Hatujui kama wao ni washabiki wa CHADEMA kweli au ni mapandikizi ya CCM yanayotaka kuivuruga CHADEMA. Mambo ya CHADEMA, waachiwe wanachama halali wa CHADEMA kuamua.
Kauli yangu hii haikuwa endorsement kwa Mbowe. Ilikuwa kanuni ya kwamba watu wasio wanachama hawana kauli kwenye mambo ya chama.
Baada ya Tundu Lissu kuchukua fomu kugombea uenyekiti wa CHADEMA, criticism hii haipo tena. Kwa sababu sasa wanaotaka kumuondoa Mbowe si wanaharakati tu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA naye anataka kumuondoa Mbowe kwenye uenyekiti.
Sasa wewe ni nani umwambie Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu, anayetumia haki yake ya kikatiba ndani ya CHADEMA kugombea uongozi, hana haki ya kuwania uenyekiti?
Unatumia kanuni gani kumkataza Lissu kuwania uenyekiti wa CHADEMA?