Kusema hoja ya kumuondoa Mkiti Imekuwa hoja baada ya Lissu kugombea haina mashiko, kwa hiyo Lissu asingegombea isingekuwa hoja.
Katiba ya Chadema iko wazi hakuna mtu anayekatazwa kugombea uenyekiti hata 2019 kuna wanachama waligombea na Lissu alikuwepo, mbona hatukuwaona wanaharakati wakihangaika kama safari hii.
Hujaelewa.
Hakuna popote niliposema hoja ya kumuondoa Mbowe imekuwa hoja baada ya Lissu kugombea.
Hii siku zote ilikuwa hoja.
Ila, ilikuwa hoja ambayo ilikuwa haijapata endorsement ya mwanachama wa CHADEMA kugombea Uenyekiti, not necessarily Lissu, mwanachama yeyote wa CHADEMA hakuwa amegombea uenyekiti, hoja ilionekana kwa kiasi kikubwa ni ya wanaharakati tu waliokuwa wanataka kuipangia CHADEMA cha kufanya bila hata ya kuwa wanachama.
Lakini sasa hivi kuna Tundu Lissu kai endorse, si yeye tu, kuna Odero Charles Odero anagombea uenyekiti, kuna mtu anaitwa Mapunda anagombea uenyekiti.
Kuna watu watatu zaidi ya Mbowe wanagombea uenyekiti.
Hawa si wanaharakati tu. Hawa ni wanachama wa CHADEMA.
Tundu Lissu ni Makamu Mwenyekiti.
Hoja imekubaliwa mpaka na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.
Kwa nini unaidogosha kwa kusema ni hoja ya wanaharakati tu wakati mpaka Makamu Mwenyekiti wa chama kaikubali hoja?