Kama ni hivyo kwa nini wanaharakati wanalia mitandaoni kuwa Mbowe aachie kwa busara na si kwa box la kura?
TAL aachane na wanaharakati bali awashawishi wajumbe wampigie kura.
Shida ya chama chao kila mmoja mjuaji na kujifanya kuwa yeye ndio chama. Hii ya kujifanya kuwa mtu ndio chama imeshapitwa na wakati, na kama chama chao kitakuwa kimejijenga kwa sababu ya mtu basi CCM itatawala hadi mwisho wa dunia.
Taasisi inatakiwa kuwa na nguvu kuliko mtu. Watu wanakuja na kuondoka ila taasisi itabakia milele.
Kama chadema inasimama kwa sababu ya TAL basi kuna tatizo. Au unafikiri CCM/Serikali inaogopa maneno ya mtu? Ili taasisi isimame lazime ijijengee ideology ambayo ndio itakuwa inaendesha taasisi na sio mtu. We need strong institution and not a strong person.
Ndio maana Malema wa Afrika Kusini amebakia kupiga domo tu wakati wenzie wanachukua majimbo na kujenga taasisi zao. Zuma kasajili chama kipya na kilipata uwakilishi mkubwa kuliko Malema wa siku nyingi na chama chao.
Achana na wanaharakati mkuu, Tundu Lissu ni mwanachama wa CHADEMA, Odero ni mwanachama wa CHADEMA, Mapunda ni mwanachama wa CHADEMA.
Wote hao ni wanachama na hawajasema Mbowe aachie uenyekiti kwa busara.
Sasa wewe inakuwaje unaacha kusikiliza maneno ya wanachama wanaoenda kugombea uenyekiti, unasikiliza maneno ya wanaharakati wa mitandaoni ambao hata kura hawapigi?
Unasemaje shida ya chama chao kila mtu mjuaji kwa kusikiliza maneno ya wanaharakati wasio wanachama? Wanaharakati usiwahesabu kama CHADEMA. Hawana hata kadi ya uanachama.
Kuhusu tatizo la kuangalia sana mtu, Tundu Lissu mwenyewe kashasema moja ya ajenda zake ni kufanya chama kiende kimfumo zaidi, kisimtegemee mwenyekiti sana, kifanye mabadililo ya katiba, kifanye ugatuzi wa madaraka yaende chini zaidi, kufanya uongozi wa kushirikiana zaidi. Kwa hiyo hayo yote Tundu Lissu kashayasema.
Nenda Clubhouse kasikilize Tundu Lissu akiwaonya sio tu CHADEMA, bali Watanzania wote, kuw anchi inaongozwa kwa sheria, kanuni, katiba, si kwa matakwa ya mtu.
Kasikilize chawa mmoja wa Lissu anaitwa Baba Mary alivyokuwa anampamba Lissu kwa kusema "Lissu ni mwenyekiti mtarajiwa, Lissu kashapita" halafu Lissu alivyomjibu kuwa mto huo hatujauvuka bado, tufanye kazi inayotakiw akufanywa kuuvuka, Lissu alimrudisha chawa kwenye mstari kwa kuchambua mambo kwa ukweli na uwazi bila kupenda kusifiwa na chawa.
Sasa kama Lissu mwenyewe anakataa uchawa, kwa nini unamsikiliza chawa badala ya kumsikiliza Lissu?