Mbunge Joseph Kasheku Msukuma ataka Magufuli apewe Mihula minne ya Miaka 20 ili kukamilisha miradi

Baaaaaaaaaaaaaaaaaaassss.
Imeisha iyo tukutane 2030 kupata Rais mpya Inshallah.
 
Tukathubutu kuruhusi hili ipo siku ataingia rais agome kutoka kabisaa kama museveni tukanyage mengine lakini hili hapana
 
Kipimo kipya cha corona kimfikie popote alipo,maneena zake msengerema huyo
 
Huyo ni muimba mapambio tu na kumtukuza mkuu wake.
Miaka 10 ikiisha apishe kwenye kiti cha urais.
 
Magufuli ni raisi tunayemuhitaji kwa kipindi kirefu, idgaf about democracy, wewe umemtaja Nyerere mbona hao wengine hujawataja michango yao?for me baada ya Nyerere ni Magufuli, hatuwezi kuwa na democracy inayotuletea viongozi wa ovyo ovyo, mfano Tundu lisu angeshinda 2020, ingekuwa ni miaka mi 5 mipya ya upuuzi, cha msingi Magufuli ana weakness zake, kelele ipigwe ajirekebishe yeye siyo Mungu kuwa hakosei, ndio maana huwa anarudi nyuma na kusahihisha (kusamehe)

Hawa politician wengi wanawaza matumbo yao, madaraka, wanadhani wakishafika level flani basi cha mwisho ni kuwa raisi, uzalendo hamna. As long as haki za binadamu zinazingatiwa, Magufuli is my president, ila naye ajirekebishe, mkali sana mpaka wasaidizi wake wanaogopa kumshauri
 
Magufuli
Magufuli hapana ndio maana watanzania wengi walimkataa kwenye box la kura sauti ya wengi ni sauti ya Mungu .
 
Magufuli

Magufuli hapana ndio maana watanzania wengi walimkataa kwenye box la kura sauti ya wengi ni sauti ya Mungu .
Kwahiyo kwa akili yako kubwa lissu alikuwa anafaa?ama hashim rungwe?
 
Naona moshi moshi... Nikigeuka huku moshi unafuka..

Amini mda sio mrefu moto utawaka
 
Ha ha ningetaka ningepewa, unadhani kuna ugumu?
 
Kila kiongozi hili jambo ni kawaida. Ni busara zake kuwakatalia. Unakumbuka alikweleza nini Mzee Mwinyi? Kwanini wewe hukubaki madarakani enzi zako
 

Falafel hilo tu
 
Hivi msukuma anajua lugha ya kichina? Kwa hiyo anataka kukopi china na kupesti Tanzania. Bunge la ndugai tutaona na kusikia mengi.

Ikumbukwe wenzetu imani ile wanamwangalia. Yakiamka watu wakwanza waanze na Hawa.
 
Tayari

Sasa Nape alikuwa anaongea nini?

Rais akiwakumbuka wafanyakazi tu ataungwa mkono wa ajabu Amalizie miradi
Mkuu hivi sisi ambao tunapinga rais kuongezewa muda tunapeleka wapi malalamiko yetu ?.

Maana hata hao wabunge hawawezi kutuwakilisha maana hatukuwachagua sisi..

Au tuwakilishe maombi yetu mbele ya lucifa.
 
Nchi nzima imejidharau maana yake,kwamba mwenye akili ni mmoja tu wengine wote Mazuzu?ubinafsi ndio chanzo cha hayo yote wengi wanajua akiondoka nao ndio mwisho wao,hivyo wanajitahidi kupambana ili nao wasiondoke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…