Mbunge Luhaga Mpina amuunga mkono Rais Samia kuwabana Mawaziri

SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2013
Posts
390
Reaction score
385
TAARIFA YA MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB), MBUNGE WA JIMBO LA KISESA (CCM) KWA UMMA, LEO TAREHE 6 APRILI, 2022 KUUNGA MKONO KAULI YA MH. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ALIYOITOA MACHI 30, 2022 KUHUSU BAADHI YA MAWAZIRI KUSHINDWA KUTOA MAJAWABU NA UFAFANUZI WA KINA JUU YA MALALAMIKO YANAYOTOLEWA NA WANANCHI YANAYOHUSU UTENDAJI KAZI WA SEKTA WANAZO ZIONGOZA.

1: Utangulizi:

Ndugu wananchi, Mtakumbuka kuwa Mnamo Machi 30, 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake wakati akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa mwaka 2020/2021, Mhe. Rais alikemea vikali tabia ya baadhi ya mawaziri kushindwa kutoa majawabu na ufafanuzi wa kina wa hoja na malalamiko ya wananchi yanayoelekezwa kwenye sekta wanazo zisimamia huku akiahidi kuchukua hatua kali kwa mawaziri wa aina hiyo.

Nanukuu“…..Kila kitu Rais aseme, kila kitu Rais, Kwa hiyo mitandaoni huko Rais hajasema, Rais hajasema, Who is Rais, Rais ni Taasisi ninyi ni wasaidizi wangu nisaidieni kusema huko, kwa hiyo kila mtu kwenye sekta yake linapotokea awe mwepesi wa kusema tutaangaliana kwenye hilo” amesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, (Machi 30,2022)

Nichukue nafasi hii kwa dhati ya moyo wangu, kumshukuru na kumpongeza sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa 2 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maono na upeo wake mkubwa katika kuisimamia Serikali.

Ni ukweli usiofichika wako baadhi ya Mawaziri ambao sekta zao zinalalamikiwa kila uchao lakini wanashindwa kutoa majawabu na ufafanuzi na badala yake yanatolewa majibu mepesi mepesi kwa maswali magumu juu ya matatizo makubwa ya wananchi na viongozi wakiwemo waheshimiwa wabunge wa Bunge letu tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa pale wanapohoji bungeni na kwenye Kamati za Bunge masuala mbalimbali yanayo lalamikiwa na wananchi.

Nitolee mfano wa hivi karibuni ambapo mtakumbuka Waziri wa Nishati alipokuwa akijibu hoja za wabunge katika kikao cha Bunge kilichopita cha Mwezi Februari 2022, kuhusu kuchelewa kwa Mradi wa Bwawa la kufua Umeme la Julius Nyerere na katikakatika ya umeme inayoendelea maeneo mbalimbali nchini.

Waziri wa Nishati badala ya kueleza kwa kina nini hasa kilichosababisha alianza kuwasakama wabunge wanaohoji matatizo hayo na kusema kuwa hawakutaka yeye awe Waziri na kwamba waanzishe mapambano binafsi na yeye na siyo mambo yanayohusu nchi.

Nanukuu “…...Maneno ya kushambuliana binafsi yanasikitisha kwamba Waziri kapanda helikopta kaweka hivi na nini, hii sio sifa ya Mbunge eeh… hatuko hapa kutupiana mawe hili ni meli yetu wote, aahiya, nikifeli mimi imefeli nchi, akifeli Rais imefeli nchi kama una matatizo ya Mhe. Samia Rais, Samia Suluhu kuwa Rais au 3 mimi kuwa Waziri tutafute jambo jingine sio mambo ya nchi” Waziri wa Nishati (15 Februari 2022).

Ndugu wananchi, kitendo cha Waziri wa Nishati kushindwa kusikiliza kwa makini hoja za wananchi na wawakilishi wa wananchi bungeni na kuwageuza wanaohoji kuwa ni maadui wa Serikali kumepelekea madhara na hasara kubwa kwa taifa letu katika baadhi ya maeneo, ikiwemo uamuzi wa kufuta kiholela tozo ya Tsh 100 kwa kila lita ya mafuta ya Dizeli, Petroli na Mafuta yaTaa ambazo ni Fedha za Mfuko wa Umeme Vijijini, kukatikakatika kwa umeme, mfumko mkubwa wa bei na ucheleweshaji wa Mradi wa Bwawa la kufua Umeme la Julius Nyerere nk.

2: Kufutwa kiholela tozo ya Tsh 100 kwa lita kwenye Mafuta Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 28 Februari, 2022 Waziri wa Nishati alitangaza kufuta tozo ya Tsh. 100 kwa kila lita ya mafuta ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa ambazo ni fedha za Mfuko wa Umeme Vijijini kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Machi hadi Mei 2022, maamuzi ambayo yataikosesha Serikali mapato ya kiasi cha Tsh. Bilioni 30 kwa mwezi na kwa kipindi cha miezi mitatu Serikali itapoteza mapato ya Tsh. Bilioni 90.

Baada ya tangazo hilo kutolewa wengi tulishikwa na butwaa nikiwemo mimi inakuwaje maamuzi hayo yafanyike bila Bunge? ilipofika Machi 6, 2022, Kamati iliwaita Wizara ya Nishati kuhoji kwanini maamuzi hayo yamefikiwa bila kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu?

Na mimi Luhaga Joelson Mpina, Mbunge wa Kisesa nilikuwa miongoni mwa wabunge waliohoji suala hili lakini 4 Wizara ya Nishati ilisimamia msimamo wake kuwa wamefanya maamuzi hayo kwa mujibu wa sheria na kwamba fedha hizo hazimo katika bajeti ya Serikali.

Nitumie nafasi hii kufanya uchambuzi mdogo kuhusu Sakata la kufutwa kiholela kwa tozo yaTsh. 100 kwa lita ya mafuta ya Dizeli, Petroli na Mafuta yaTaa kama ifuatavyo:-

1. Chimbuko la kuanzishwa kwa tozo ya sh 100 kwa kila lita ya mafuta ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa kwa ajili ya Mfuko wa Umeme Vijijini ilianza mwaka 2005, ilipopitishwa Sheria ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005 (Rural Energy Act 2005), ambapo kupitia Sheria hiyo, Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na Mfuko wa Umeme Vijijini (Rural Energy Fund) vilianzishwa. Hali ambayo ilipelekea kuongezeka kwa kasi ya usambazaji wa umeme vijijini kutoka vijiji 2,018 mwaka 2015 hadi kufikia vijiji 10,312 mwaka 2020.

2. Kuanzishwa kwaTozo, Mwaka wa Fedha 2013/2014, Waziri wa Fedha na Mipango, Hayati Dk. William Augustao Mgimwa (Mb) akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Serikali Bungeni alisema Nanukuu“…. Sheria ya Petroli (Petrolium Act), Sura 392, ili kutekeleza dhamira ya Serikali ya kusambaza umeme vijijini, napendekeza kuanzisha tozo ya mafuta ya Petroli (Petroleum levy) ya Shilingi 50 kwa kila lita ambayo itakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mapato yatakayo kusanywa kutoka kwenye tozo hiyo yatatumika kugharamia mahitaji ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Katika kusambaza umeme vijijini hatua hii itatekelezwa kupitia Tangazo litakalochapishwa katika Gazeti la Serikali, Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato 5 ya Serikali kwa kiasi cha Tsh. Bilioni 123.725” alisema Dk. William Augustao Mgimwa, Waziri wa Fedha na Uchumi wa kipindi hicho na Bunge liliridhia mapendekezo hayo.

3. Ilipofika Mwaka wa Fedha 2015/2016, Waziri wa Fedha na Uchumi wa kipindi hicho, Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb), aliwasilisha bungeni pendekezo la kuongeza tozo.

Nanukuu“Mhe. Spika, napendekeza kuongeza tozo ya mafuta ya Petroli kwa viwango vifuatavyo, mafuta ya Dizeli kutoka Tsh. 50 kwa lita hadi Tsh 100 kwa lita ikiwa ni ongezeko la Tsh 50 kwa lita, Mafuta ya Petroli kutoka Tsh 50 hadi Tsh 100 kwa lita ikiwa ni ongezeko la Tsh 50 kwa lita, Mafuta ya Taa kutoka Tsh 50 kwa lita hadi Tsh 150 kwa lita ili kuondoa uwezekano wa kuchakachua; hatua ya kuongeza tozo ya mafuta ya petrol inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Tsh Bilioni 136.786 fedha hizi zote zitaelekezwa katika Mfuko wa REA” alisema Mhe. Saada Mkuya Salum, Waziri wa Fedha na Uchumi wa kipindi hicho. Bunge liliridhia pendekezo hilo kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za usambazaji wa umeme vijijini.

4. Tozo ya Tsh 100 kwa kila lita ya mafuta ya Dizeli na Petroli na Tsh 150 kwa kila lita ya Mafuta ya Taa kwa ajili ya Mfuko wa Umeme Vijijini ilianzishwa na Bunge kupitia hotuba za Bajeti za miaka ya 2013/2014 na Mwaka 2015/2016 na tangu kipindi hicho fedha zimekuwa zikikusanywa nakupelekwa katika Mfuko wa Umeme Vijijini kwa ajili ya kutekeleza miradi ya usambazaji wa umeme vijijini kila mwaka wa fedha.

Hivyo tozo ya Tsh 100 ya kila lita ya mafuta ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa iliyofutwa na Waziri wa Nishati ilianzishwa na Bunge na ipo kwenye bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2021/2022.

5. Mapato yaliyofutwa na Waziri wa Nishati ya kiasi cha Tsh. Bilioni 90 yamo katika Makadirio ya Mapato ya Tsh Trilioni 37.68 yaliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mwaka wa Fedha 2021/2022 na kutungiwa Sheria Appropriation Act 2021.

6. Mapato yaliyofutwa hayakuwekewa chanzo mbadala cha kufidia mapato hayo na kwa kuwa ni kuanzia Machi hadi Mei utakuwa umebaki mwezi mmoja tu mwaka wa fedha wa 2021/2022 kumalizika na hivyo hakutakuwa na nafasi nyingine ya kufidia mapato hayo.

7. Mapato ya Mfuko wa Umeme Vijijini ni mapato lindwa (Refenced Funds) na hairuhusiwi kubadilishiwa matumizi au kufutwa bila utaratibu, REA inawakandarasi iliyosaini nao mikataba na wanaendelea na ujenzi maeneo mbalimbali nchini. Kitendo cha kuyaondoa mapato haya ni kuhujumu miradi ya umeme inayoendelea vijijini.

8. Naomba ieleweke kuwa, ninachokilalamikia hapa sio kufutwa kwa tozo ya Tsh 100 kwa lita ya mafuta ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa, isipokuwa ninachokilalamikia mimi ni utaratibu uliotumika kufuta tozo hiyo, Waziri wa Nishati kama aliona kuna uhitaji wa kufuta tozo hiyo kwa lengo la kuwapunguzia maumivu wananchi kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta duniani alipaswa kufanya tathmini ya kina na kushirikisha Taasisi nyingine 7 za Serikali na kupata kibali cha Bunge kama Sheria, Kanuni na Taratibu zinavyosema.

9. Waziri wa Nishati alilikwepa Bunge kwa makusudi na hapakuwa na dharura yoyote kwa maamuzi aliyochukua, Bunge liliahirishwa tarehe 18 Februari 2022 na tangazo la Waziri kufuta tozo lilitolewa tarehe 28 Februari 2022 ikiwa ni siku 10 tu baada ya Bunge kuahirishwa.

Hii inamaanisha kuwa mchakato wa kufuta tozo ulianza na kukamilika ikiwa Kamati na Bunge likiendelea na vikao vyake Dodoma ambapo Waziri angeweza kutumia fursa hiyo kuwasilisha bungeni mapendekezo yake.

10. Maamuzi ya Bunge katika kupitisha Bajeti ya Serikali hufanywa kwa kupiga kura na baadae kufuatiwa na kutungwa kwa Sheria na Kanuni kusimamia utekelezaji wa bajeti hiyo ambapo ni The Appropriation Act, Finance Act, Government Notice (GN). Lakini jambo la kusikitisha maamuzi ya Waziri wa Nishati haya kuzingatia uwepo wa Sheria na Kanuni hizo.

11. The Mid-year Budget Review hufanyika kila ifikapo Disemba, Serikali iliwasilisha katika Kikao cha Bunge cha Februari 2022 ambapo mambo yanayohitajika kufanyiwa mapitio ikiwemo ongezeko la mapato la Tsh Trilioni 1.3 ya Mkopo IMF-Uviko 19 katika Bajeti ya Serikali, hata hivyo suala la kufuta tozo ya Tsh 100 kwa lita katika mafuta na kupunguza mapato kwa kiasi cha Tsh Bilioni 90 halikuwasilishwa na Serikali.

12. Madai ya Waziri wa Nishati kuwa maamuzi ya kufuta tozo ya Tsh 100 kwa lita ni mwendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa mwezi Oktoba 2021. Maagizo ya Mhe. 8 Rais hayamuondolei wala hayampi kinga Waziri wa Nishati kutokufuata sheria na taratibu zilizopo na ninamshukuru sana Mhe. Rais katika hotuba yake amejitoa na kuwa hahusiki katika suala hilo na alisingiziwa.

13. Waziri wa Nishati hana mamlaka kisheria ya kuondoa tozo yoyote iliyopitishwa na Bunge au kupunguza mapato yaliyoidhinishwa na Bunge. Maamuzi ya Waziri wa Nishati kufuta tozo hii bila kupata ridhaa ya Bunge amevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amevunja Sheria za nchi alizoapa kuzilinda, kuzitetea na kuzisimamia na pia ameingia kwenye makosa ya uhujumu uchumi.

14. Hapa kuna maswali mengi ya kujiuliza, kama maamuzi haya yalikuwa na nia njema ya kuwapunguzia ukali wa maisha watanzania kutokana na athari za kupanda kwa bei za mafuta duniani, Kwa nini Waziri wa Nishati hakufanya tathmini ya kina na kwanini suala hili aliamue peke yake? Je inawezekanaje Waziri mmoja kufuta mapato ya Serikali kiasi cha Tsh Bilioni 90 peke yake.

15. Najiuliza kama sheria, kanuni na taratibu zinamuelekeza Waziri wa Nishati kushirikisha Taasisi nyingine za Serikali na baadaye Bunge kuidhinisha, Kwanini Waziri alilikwepa Bunge? Na kwa nini Waziri hakuzingatia Sheria katika maamuzi yake? Na Je iliwezekana vipi haya yote kufanyika wakati kuna Mwanasheria Mkuu wa Serikali?.

16. Naomba kurejea tena hotuba ya Mhe. Rais ya tarehe 30 Machi, 2022 wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo Mhe. Rais alitengua 9 maamuzi ya Waziri wa Nishati ya kufuta tozo ya Tsh 100 kwa lita ya mafuta ili kulinda mapato ya Serikali na kwamba iliamuliwa kinyume cha Sheria na bila tathmini ya kina, alisema Nanukuu “….Waziri akaona nikitoa shilingi 100 ya pande kwa kwa shilingi 56 nitaleta unafuu ndani ya nchi, lakini kwa bahati mbaya hakuangalia kwa upana zaidi kwamba ile ilikuwa tayari iko kwenye bajeti iliyopitishwa na Bunge.

Kwa hiyo kulikuwa kuna utata kidogo tumekaa kama Serikali tumerekebisha, ile shilingi iliyotoka nimeagiza irudishwe na kwamba tathmini tuliyofanya hata kama ile shilingi tungeitoa kwa mwenendo wa upandaji wa bei ya mafuta duniani bado isingekuwa na impact, ila tungejikosesha kile ambacho tunakusanya kwa hiyo tumeamua shilingi irudishwe” Amesema Mhe. Samia Suluhu Hassan (Machi 30,2022).

17. Kwanza nimpongeze tena Mhe. Rais, Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi yake ya kulinda Sheria za nchi na kuokoa mapato ya Serikali kiasi cha Tsh. Bilioni 60 ambayo yalikuwa yanapotea kutokana na maamuzi hayo batili yaliyofanywa na Waziri wa Nishati, ingawa pamoja na maamuzi hayo mazuri yaliyofanywa na Mhe. Rais kwa bahati mbaya sana tayari Serikali imepoteza mapato ya Tsh Bilioni 30 katika kipindi cha Mwezi Machi 2022 ambapo hatukukusanya mapato hayo na kupelekea kuzorotesha kasi ya usambazaji umeme vijijini na kuongeza madeni ya wakandarasi yasiyo na sababu, Hapa tujiulize ni vijiji vingapi leo hii nchini vimekosa umeme kwa maamuzi haya?.

18. Maamuzi ya Waziri wa Nishati kufuta tozo ya Tsh 100 kwa kila lita ya mafuta bila kufanya tathmini ya kina na bila kuzingatia sheria za nchi, yanaacha maswali mengi bila majibu kuwa alikuwa anasukumwa na jambo gani? Na kwa kufanya hivyo amevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 62 (3) na Ibara ya 63 (2) na (3), amevunja Sheria za Appropriation Act 2021, The Finance Act, The Budget Act 2015), Rural Energy Act 2005 na Sheria ya Uhujumu Uchumi (The Economic and organized Control Act 1984).

19. Kwa maoni yangu, Waziri wa Nishati hakuwa na nia njema katika suala hili na ninaamini suala la kuchukuliwa hatua za kisheria sio la hiari, wako watanzania wengi wako mikononi mwa vyombo vya dola kwakushukiwa tu, lakini Waziri huyu makosa yake yana ushahidi wa wazi usiotiliwa mashaka yoyote, kwa mujibu wa sheria zetu Makosa ya Uhujumu Uchumi yanaanzia na kiasi cha Tsh Bilioni 1, Waziri wa Nishati ameliingizia taifa hasara ya Tsh Bilioni 30.

Najiuliza vyombo vya Dola ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) viko wapi kutekeleza jukumu lake la kisheria, Waziri huyu amekwamisha utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka 5 hili sio jambo dogo na najiuliza Waziri wa Nishati amejitathmini vipi kuhusiana na kashfa hii nzito inayomkabili.

20. Namalizia kwa kumpongeza sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuzilinda na kuzitetea Sheria za nchi lakini pia kwa kukataa rasilimali za umma zisifujwe na watu wachache, naahidi kwamba nitaendelea kuishauri kikamilifu Serikali yangu ndani na nje ya Bunge.

Na kwa kuwa Bunge la Bajeti limeanza nimejiandaa vizuri sana kuwasilisha hoja mbalimbali bungeni na nitaweka wazi mambo yote yaliyojificha yanayosababisha

Kuchelewa kwa Mradi wa ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere

(ii) Kukatikatika na migao ya umeme inayoendelea maeneo mbalimbali nchini.

(iii) Tatizo la kupanda kwa bei za bidhaa (mfumko wa bei)

(iv) Kuchafuka kwa Mto Mara.

(v) Ucheleweshaji wa hukumu za mapingamizi ya kodi yenye jumla ya ya kiasi cha Tsh. Trilioni 360. Deni la Taifa.

Mungu Libariki Jimbo la Kisesa,

Mungu Ibariki Tanzania,

Mungu Ibariki Afrika.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.
 
Wakina Mh Mpina wanatakiwa wawe wengi ili Taifa hili lisipoteze muelekeo. Mh Mpina kasahau suala la Tanesco lilivyotangazwa tena bila ya kuchukua tahadhari zozote za consiquences za kuhujumu juhudi za Mh Rais SSH kualika wawekezaji katika sera yake ya' tuna fungua nchi.' That was a systematic sarbotage kwa Rais.

Anyway umeme huku kwetu leo kutwa mzima haujakatika. Pongezi kwa wadau wote wa kutuletea Umeme wa uhakika.
 
Tivu ake atuliza
Alishinda?
Wakina Mh Mpina wanatakiwa wawe wengi ili Taifa hili lisipoteze muelekeo. Mh Mpina kasahau suala la Tanesco lilivyotangazwa tena bila ya kuchukua tahadhari zozote za consiquences za kuhujumu juhudi za Mh Rais SSH kualika wakezaji katika sera yake ya' tuna fungua nchi.' That was a systematic sarbotage kwa Rais.

Asije akanyamazishwa na chama chake.Makamba hatoshi kwenye hiyo wizara.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo mpina shida yake ni kuondoa hiyo tozo tu?
Jamaa yake mambo mangapi alikuwa anayafanya kinyume na sheria hakuwahi kupinga? Tena hili la yozo lilikuwa linawapa nafuu wananchi wakati huu ambapo bei ya mafuta inapsnda mno kiasi cha kuumiza wananchi, ila jamaa yake alikuwa anafanya maamuzi mabovu yasiyo na tija kama la kutoongea lolote kwenye 1.5 T usiyo na maekezo katika matumizi ya serikaki , ila hakuwahi kufunua domo lake.
Sio bure ana lake!
 
Kuondolewa kwa tozo ya mafuata ya 100/- na kurudishwa kwake kumemchonganisha Rais na wananchi anao waongoza. Nani alikuwa nyuma ya huu ushauri ni siri hatuwezi kujua. Mh Mpina anajituma ama anatumwa nayo ni siri. Hapa jF kumepatikana hoja ya kujadili.
 
Mpina jitayarishe 2025 uende ukalime hukumbuki ulivyobebwa kwenye uchaguzi mkuu 2020
Sisi wavuvi hatutakusahau kwa ukatili wako
 
Hii ni takataka, Chama kina forum za kuongelea mambo yake, na yeye ana forum, lazima ajutie kuandika takataka hizi
 
Mpina sasa akae kimya. Kipindichake kulikuwa na uozo mwingi na hakuwai kuongea chochote
 
kwa bahati mbaya sana tayari Serikali imepoteza mapato ya Tsh Bilioni 30 katika kipindi cha Mwezi Machi 2022 ambapo hatukukusanya mapato hayo na kupelekea kuzorotesha kasi ya usambazaji umeme vijijini na kuongeza madeni ya wakandarasi yasiyo na sababu, Hapa tujiulize ni vijiji vingapi leo hii nchini vimekosa umeme kwa maamuzi haya?.​
Duh...!.
P
 
Wakina Mh Mpina wanatakiwa wawe wengi ili Taifa hili lisipoteze muelekeo. Mh Mpina kasahau suala la Tanesco lilivyotangazwa tena bila ya kuchukua tahadhari zozote za consiquences za kuhujumu juhudi za Mh Rais SSH kualika wawekezaji katika sera yake ya' tuna fungua nchi.' That was a systematic sarbotage kwa Rais.

Anyway umeme huku kwetu leo kutwa mzima haujakatika. Pongezi kwa wadau wote wa kutuletea Umeme wa uhakika.

Anayehujumia ndo kamwekea pale kwani yeye hana akilli timamu kujua anahujumiwa . Anachofanya makamba kina baraka za SSH kww asilima 200
 
Kwa hiyo mpina shida yake ni kuondoa hiyo tozo tu?
Jamaa yake mambo mangapi alikuwa anayafanya kinyume na sheria hakuwahi kupinga? Tena hili la yozo lilikuwa linawapa nafuu wananchi wakati huu ambapo bei ya mafuta inapsnda mno kiasi cha kuumiza wananchi, ila jamaa yake alikuwa anafanya maamuzi mabovu yasiyo na tija kama la kutoongea lolote kwenye 1.5 T usiyo na maekezo katika matumizi ya serikaki , ila hakuwahi kufunua domo lake.
Sio bure ana lake!
Kuiondoa Tozo hiyo ndio kumepelekea kuongezeka kwa bei ya kufungiwa umeme wa REA 27,000/=.
Huko vijijini.

Watu wanaongelea vitu hai na wewe cheti hewa unaongelea mizimu iliyokwisha kufa?
 
K
Mpina jitayarishe 2025 uende ukalime hukumbuki ulivyobebwa kwenye uchaguzi mkuu 2020
Sisi wavuvi hatutakusahau kwa ukatili wako
Kwa hiyo unamshauri anyamaze? Nani CCM ambaye hakubebwa? Hata huyo waziri anayemsema nani asiyejua anabebwa!!
 
Bunge la Bajeti limeanza, nimejiandaa vizuri nitaweka wazi baadhi ya hoja ngumu ikiwemo kuchelewa bwawa la umeme, kukatikakatika kwa umeme, kupanda bei za bidhaa, kuchafuka kwa Mto mara. Tutayasema yote bila kumuogopa mtu, vitisho kutoka kokote- Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa.
 
Bunge la Bajeti limeanza, nimejiandaa vizuri nitaweka wazi baadhi ya hoja ngumu ikiwemo kuchelewa bwawa la umeme, kukatikakatika kwa umeme, kupanda bei za bidhaa, kuchafuka kwa Mto mara. Tutayasema yote bila kumwogopa mtu, vitisho kutoka kokote- Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa.
Mwendazake timu tulieni Zama zimebadilika ......
 
Back
Top Bottom