Mbunge Mohammed Issa aliyesema yeye si Mtanzania, kwanini bado yupo Bungeni?

Hayo ni maajabu ya Musa na Speaker/kaimu speaker akakaa kimya tu.
 
Anajua anachofanya Bosi angekuwa Magu angthubutu?!
 
Hii mbegu wamaepianda Wazanzibar kwasababu ile ile aliyosema Nyerere '' Sisi ni Wazanzibar wao ni Watanganyika''
Ukishajitambulisha kwa Uzanzibar huwezi kukwepa Utanganyika. Ukishaondoa Zanzibar huwezi kuwa na Tanzania

Ni Wazanzibar hawa akina Jussa, Othman, Duni wanataja 'Tanganyika'' wanaosema Watanganyika ni Wapumbavu wamelala kama huyu Mbunge wa watu 3,338 wa ACT Wazalendo anayesema tutumie passport.

Ukisoma mandhari ndani ya Taasisi za nchi hata hapo Bungeni Watanganyika wakiwemo wa CCM wamechoka.
Tunahitaji Tanganyika tu kama watahitaji Muungano wataomba wao, Watanganyika hawana cha kupoteza!

JokaKuu Pascal Mayalla @
 
Naanza kuwa tofauti na wewe kidogo.
Hatuwezi kuvunja muungano kwa sababu ya kikundi hiki kidogo ambacho tunajua historia yake toka muungano uwepo. Huu utakuwa ni ujinga wa hali ya juu sana.

Muungano utaendelea. Serikali itabaki kuwa moja tu. Acha hiki kikundi kiendelee kupiga kelele huko huko kwenye serikali moja.

Hiki kikundi kimepewa fursa, kilipoanza kupenyeza mambo yake ya "KERO" zisizokuwa na mwisho; na kwa ujinga wa CCM wakadhani kitaishia hapo. Sasa wamejitokeza mbele kabisa kwa ujasiri wote, kudai wao ni Wazanzibari, na siyo waTanzania!
 
Yeye ni Mzanzibari kwanza utanzania ni subset.
Kama umesoma hesabu za set utamuelewa.
Ndio maana tunasema huu Muungano una utata sana
Tukienda kwenye hesabu, mimi nitakupeleka kwenye AI (Artificial Intelligence), sasa sijui kama hapo tutaelewana.
Hili ni jambo jepesi tu, achana na 'subsets' hizo ambazo hazimo katika uraia wa nchi yoyote. Just be straight, on point.
 
Serikali moja ipi hiyo ambayo itabaki kati ya hizi za sasa mbili? Na lini hiyo serikali moja itauliwa na kubaki na hiyo moja?
Unless otherwise umekoment upupu na ujinga ambao huuelewu
 
Kwamba yeye siyo 'MTanzania'?

Wewe unadhani yupo sahihi?
Unaweza kuwa Mtanzania lakini usiwe Mzanzibar

Ndio sababu yeye anajivunia Uzanzibar wake

Yupo sahihi kwa sababu hajawahi Kuomba uraia wa Tanzania amekutana nao kwa mujibu wa katiba πŸ˜€
 
Unaweza kuwa Mtanzania lakini usiwe Mzanzibar

Ndio sababu yeye anajivunia Uzanzibar wake

Yupo sahihi kwa sababu hajawahi Kuomba uraia wa Tanzania amekutana nao kwa mujibu wa katiba πŸ˜€
Mbona unajichanganya mwenyewe?
Analo gamba (Pasipoti) aliyoomba yeye mwenyewe. Ni lini kila raia huomba uraia wa nchi aliyozaliwa, aliyokuta wazazi wake ni raia wa nchi hiyo?
 
Tukienda kwenye hesabu, mimi nitakupeleka kwenye AI (Artificial Intelligence), sasa sijui kama hapo tutaelewana.
Hili ni jambo jepesi tu, achana na 'subsets' hizo ambazo hazimo katika uraia wa nchi yoyote. Just be straight, on point.
Mbona ni suala ambalo lipo wazi.
Mzanzibar ni mzanzibari kwanza na mtanzania kama chaguo la pili.
Kule Zanzibar kuna kazi zinatangazwa ukiomba hizi kazi unatakiwa uambatishe kitambulisho cha ukaazi wa zanzibar hawahitaji cheti cha nida unafikiria ni kwa nini.
Ili kuwa Rais wa Zanzibar unatakiwa uwe mzanzibari ukiwa Mtanzania tu huna sifa za kugombea uraisi wa Zanzibar
 
Serikali moja ipi hiyo ambayo itabaki kati ya hizi za sasa mbili? Na lini hiyo serikali moja itauliwa na kubaki na hiyo moja?
Unless otherwise umekoment upupu na ujinga ambao huuelewu
Ukitaka 'upupu na ujinga' kama unavyo sema utaupata sana hapa, kwani umejaa tele ukitaka hivyo.
Hujui kuundwa kwa serikali moja kunafanyikaje?
 
Huo ni upumbavu uliovumiliwa miaka mingi. Haina maana hauwezi kukomeshwa.
 
Kwamba yeye siyo 'MTanzania'?

Wewe unadhani yupo sahihi?
Yupo sahihi yeye ni Mzanzibari ndio maana anaweza kumiliki ardhi zanzibar bila masharti yeyote kama ambayo anapewa Mtanzania asiyekuwa Mzanzibari.
Labda mtakuwa mmeelewa nyie vichwa ngumu
 
Mbona unajichanganya mwenyewe?
Analo gamba (Pasipoti) aliyoomba yeye mwenyewe. Ni lini kila raia huomba uraia wa nchi aliyozaliwa, aliyokuta wazazi wake ni raia wa nchi hiyo?
Yeye kazaliwa nchi ya Zanzibar

Usichoelewa ni kwamba Tumeungana kwenye baadhi ya mambo tu Ndio sababu kuna Mufti kwenye kila nchi πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Naanza kuwa tofauti na wewe kidogo.
Ni jambo jema tunapata mitazamo tofauti. Na wala usihofu mkuu, kuwa critical na simamia hoja unayoiamini.
Hatuwezi kuvunja muungano kwa sababu ya kikundi hiki kidogo ambacho tunajua historia yake toka muungano uwepo. Huu utakuwa ni ujinga wa hali ya juu sana.
Tatizo kikundi hicho kimepewa 'umuhimu sana' kama kwamba Wazanzibar ni Raia wa daraja la I.
Kila siku kuna kero za Wazanzibar, zile za Watanganyika zinashughulikiwa na nani?

Tunatumia pesa nyingi kuwa 'please' mchango wao kwa maendeleo yetu ni matusi passport..
Yupo Dodoma analipwa mshahara na marupu rupu kukaa kulala na kusikiliza mambo yasiyomhusu.
Anavimbiwa na kutoa matusi Tanganyika.

Hapana! Hebu tushawishi Mtanganyika kwanini Mtanganyika anahitaji muungano wa aina hii
Muungano utaendelea. Serikali itabaki kuwa moja tu. Acha hiki kikundi kiendelee kupiga kelele huko huko kwenye serikali moja.
Wazanzibar hawataki na huyo anayeongea au wanaoongea wana 'Baraka'.

Hivi tangu Wazanzibar waanze kuporomosha mitusi mwaka huu umemsikia nani wa CCM Zanzibar, CCM Taifa, ACT Zanzibar akikemea. Hii maana yake wote wanakubali hoja kama za passport na upuuzi mwingine

Tunaweza kutumia passport kwenda Zanzibar, hakuna shida.
Naomba ushawishi watu kwanini Mtanganyika wa Rorya, Isevya, Kantalamba, Kadewele, Naliendele , Mafia , Amani wanahitaji Muungano!
Hiki kikundi kimepewa fursa, kilipoanza kupenyeza mambo yake ya "KERO" zisizokuwa na mwisho; na kwa ujinga wa CCM wakadhani kitaishia hapo. Sasa wamejitokeza mbele kabisa kwa ujasiri wote, kudai wao ni Wazanzibari, na siyo waTanzania!
Anayetoa fursa hiyo ndiye anayefumbia macho ! Unachoita kikundi kilimshawishi alete KERO ya bili ya umeme ya Bilioni 60 kwa Watanganyika. Yaani imefika mahali hata bili za umeme tunalipa!! ni kwa 'return gani' huo ni muungano gani. Tunaungana kwa 'give and take'' . Tushawishi kwa sasa tunapata nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…