Mbunge Mstaafu na Mtu Maarufu anahitaji Mchango wa matibabu, wewe unadhani uta survive vipi?

Duh!!, Umasikini kitu Kibaya Sana.Wengi wanakufa kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.
Naonaga pale Mloganzila mgonjwa anaporuhusiwa ndugu wanavyofanya vikao pale chini vya michango ya kulipa bili ndio mgonjwa atoke.
Hao ndugu wenyewe ukiwaangalia wengi hata nauli ya mwendo Kasi ya kimara ni shida, wamekauka midomoo.. Sasa Kuna huyo mkuu wa msafara yeye anapiga simu kwa ndugu wa mbali na kile kitecno triple line.
Kuna binti mmoja aliambiwa akalipie elfu kumi na sita ili apigwe x Ray.
Aliruka hatua kumi na sita huku akilalamika ashamchungulia daktari kwa elfu ishirini bado alipie x-ray ndio alipie dawa? Kwani waganga wa jadi wameisha?
 
kamanda una uhuru wa maoni ila figo ni habari nyingine mungu atupe huruma yake naogopa sana sana. Huku africa hatuwezi hakika Mungu atusimamie, Professor Jay Mungu akuponye uwe mfano wa shuhuda ya mfano. Zaburi 86 ikawa neno la uzima.
 
Acha uongo wewe.. muhimbili mgonjwa awezi lazwa chini..Moi tupo mara nyingi tu
 
Dah!!!, Inasikitisha sana.
 
Dawa zinaua sana figo, sasa na magonjwa yanavyotuandama kuziepuka ni mtihani.

Use Antibiotic when necessary and let it be the last options bro…

Pia unaweza kuwa na good lifestyle ila unakuta vyakula tunavyokula hasa hawa broilers, mayai, maziwa unakuta yana antibiotic residues kama zote…

Sidhani kuna mfugaji ambaye yuko tayari ku discard maziwa, mayai kisa ametoka kutibu mifugo yake..

Public health is still a big proble kwetu waafrika kwa ufupi tumejawa na ubinafsi sana kutokujali afya za walaji.
 
Ngoja siku figo ifeli ndy akili ikukae sawa

Unamkumbuka Ruge mtahaba? Bakuli zilivyo pitishwa?
 
Ngoja siku figo ifeli ndy akili ikukae sawa

Unamkumbuka Ruge mtahaba? Bakuli zilivyo pitishwa?
Nakumbuka kulikuwa na ofc nafanya Kaz moja Kati ya maboss wa hyo kampuni aliuguwa figo michango ikachagwa na jama Ni doni tu nae siku moja nikasikia majungu kutoka kwa kijna wa boss akisema tunamchangia mtu ambae anajenga nyumba dsm tegeta .. kweli watu wanachangishana
 
Ole wetu watu wa chini tunaobeba mzigo wa umeme na tozo kibao.

Hii inaonesha utofauti uliopo,

Je huko muhimbili hawapo wagonjwa wenye shida na wanaugua kuliko huyu.
 
Watu wanafanya masikhara sana na maradhi
 
Umenifikirisha sana...
 
Hiki ni kiwanda cha uongo. Prof hahitaji michango bali michango ndo inakuhitaji Prof. Sio wakati wote tunamchangia mtu kwa sababu hana uwezo bali ni kuonyesha mshikamano wakati wa shida
Kwanza alivunjiwa nyumba,, ikabidi ajenge ingine
Pili hela ikatumika kwenye kampeni na ubunge hakupata,
Tatu ameugua kila wiki cost milioni 4,,
Lazima atepete tu
 
Ushawahi jiuliza Jasiri muongoza njia ambaye alisifika kwa kupiga dili zote zamoto za 600M mpaka 1B ilikuwaje ikafikia akaanza kuombewa michango ijapokuwa alikuwa mkurugenzi wa Clouds na anashea zake pamoja na mtonyo wake?

Hebu acha kiburi cha uzima ndugu yangu, hakuna utajiri unaozidi afya hebu rudia kusoma nachosema.

Unaweza ukapata ugonjwa unaokutaka ubadilishiwe damu kila baada ya week which costs millions. Ruge alipigwa 6M kila siku akiwa kwenye matibabu watu walijivunga kimya ila ilienda ikafikia wakati sasa wakaona hela inakaribia kukata wakanyoosha mikono juu watu wachangie.

Hakuna ambaye alitegemea mtu kama Ruge jinsi ana uwezo wa kutengeneza pesa ingefikia wakati angetembeza bakuli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…