Mbunge wa Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria

Mbunge wa Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria

Miezi michache imebakia kuvunjwa bunge, nionavyo kusingekuwa na haja ya kumchagua.
 
Mila zetu za kiafrika zinakataa kutenda hivyo! Maiti akishazikwa, unapitisha hata siku mbili au tatu, mila inakuruhusu kuifanya yaliyo ya muhimu sana kwa vile inakuwa bado ni msiba mbichi sana
 
Bandika bandua...

Hii ndio faida ya kujipendekeza na kuitetea serikali hata kwenye mambo ya ajabu. Kwenye awamu hii Wanaosaka teuzi fuateni nyayo za Mwigulu.
Mkuu wetu anapenda watu wanafiki na wanaojua kujipendekeza.

Hii haraka ni kama mtu aliyekuwa anasubiria. Hataki kabisa kuomboleza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Mwigulu Nchemba kule twitani amewahi hata kutoa neno la pole kwa familia ya marehemu balozi mahiga kweli, mi sijaona kabisa?
Au tusubiri huenda atatoa baada ya uteuzi huu.
 
Kama ambavyo uwaziri wake haunisaidii mimi , kama wewe sio mkewe au mumewe basi Huli mshahara wake ....so tujadili kwa picha pana ,hakuna mtu mwenye haki ya kupata stress na kazi yake zaidi ya familia yake ....au pengine mchepuko wake
Na mimi naongezea, ENDELEA NA STRESS ZAKO MA CHUKI ZAKO ILA JAMAA NDIO ANAENDA KUWA WAZIRI WA KATIBA MA SHERIA, na huna la kufanya!
 
Watajuana wenyewe na teuzi zao. Ila jamaa nae kiungwana angesubiri kidogo siku mbili tatu. Yaani marehemu hata 'haja-settle' vizuri kwenye nyumba yake ya milele!
 
Hakuna wachezaji wa akiba hivyo majeruhi inabidi warudi uwanjani.
 
Wapinzani wa Mwigulu ni wanafiki sana. Juzi walitoka kusema sio chagua la Rais na kudai hata jina lake Rais hataweza kulirudisha.

Sasa hivi wamebadilisha stori.

Hongera zako Dr.Nchema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha wivu wewe mtoto wa kike,so nyie ndio mliokuwa mnasema hata ajipendekeze vipi harambi uwaziri tena
Bandika bandua...

Hii ndio faida ya kujipendekeza na kuitetea serikali hata kwenye mambo ya ajabu. Kwenye awamu hii Wanaosaka teuzi fuateni nyayo za Mwigulu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha ha, yaani nimezima data masaa mawili tu, nakuta habari mpya.
 
Back
Top Bottom