Toka maktaba uchaguzi wa ndani CCM 2015 :
Mabomu,risasi za moto zatumika ofisi za CCM Kiteto
Gari la Ole Sendeka lavunjwa vioo,Ole Nangoro anusurika kichapo
· Nyumba yake yavamiwa na wanachama, wavunja taa na kumpiga mlinzi
Habari kwa kina :
Agosti 11, 2015
Mabomu,risasi za moto zatumika ofisi za CCM Kiteto
·
Mabomu,risasi za moto zatumika ofisi za CCM Kiteto
Agosti 11, 2015
Mabomu,risasi za moto zatumika ofisi za CCM Kiteto
·
Ripoti:
Na. Mohamed Hamad, Manyara
JESHI la polisi wilayani Kiteto mkoani Manyara limetumia mabomu ya machozi na silaha za moto kuokoa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict Ole Nangoro na Christopher Ole Sendeka pamoja na kamati ya siasa ya Mkoa wa Manyara waliofika kuhakiki matokeo ya Ubunge
Awali wajumbe hao walizuiwa kwa mawe na magogo barabarani kata ya Engusero wasifike makao makuu ya wilaya ya Kiteto wakitokea Dodoma, hali iliyolazimu Jeshi la Polisi kuwaokoa kwa kuwapa ulinzi kwa kuwafikisha Kibaya kwaajili ya kuhakiki matokeo hayo
Baada ya kamati ya siasa ya mkoa kufika katika ofisi za CCM Wilaya ya Kiteto majira ya mchana walianza kuhakiki matokeo ya Ubunge ambayo yalidaiwa kulalamikiwa na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict Ole Nangoro aliyeambatana na wajumbe hao kutaka yahakikiwe
“Baada ya kusikia kuna kamati ya siasa mkoa wa Manyara imefika wanachama tulilazimika kufika ofisi za CCM kutaka kujua hatma ya ujio wao, kwani tumeshuhudia maeneo mengi matokeo ya uchaguzi yanabadilishwa baada ya kutangazwa washindi”alisema mwananchi Rajabu Jagon
Alisema wajumbe hao waliingia ofisini ya CCM kwa zaidi ya masa 6 huku wanachama wakisubirinje hali iliyohofiwa kuwa huenda walilenga kubadilisha matokeo hayo na ndipo kauli za kejeli vitisho zikaanza kutolewa na baadhi ya wajumbe hao na kuwafanya wanachama wapandwe na jazba
Christopher Ole Sendeka mjumbe wa kamati ya Siasa mkoa wa Manyara baada ya kutoka nje alionekana kuibua malumbano na wanachama hao wakidai aliwakashifu hali iliyowapandisha jazba vijana hao na kuanza kurusha mawe kutaka kumpiga.Hali iliyowafanya polisi kuingilia kati kunusuru
Muda mfupi Christopher Ngubiagoi mjumbe wa Halamshauri kuu ya CCM Taifa aliyefuatana na kamati hiyo alitoka nje kutuliza mzuka wa wanachama hao bila mafanikio na ndipo mawe yalipoanza kurushwa na kuvunjwa kioo cha nyuma cha gari la Ole Sendeka na ndipo Polisi wakaanza kurusha mabomu na silaha za moto juu
Tukio hilo lilichukua takriban dakika arobaini na tano baada ya wanachama hao kupambana ana kwa ana na polisi ofisini hapo huku wakijaribu kuwaokoa wajumbe kwa kuwalazimisha watoke kwenye ofisi hizo kwa kurusha mabomu na kutumia silaha za moto
Hii ni mara ya pili kwa mbunge anayemaliza muda wake Ole Sendeka kupata wakati mgumu baada ya dereba wake kumwondosha katika ofisi hizo mithili ya kukwepa majambazi huku akiendelea kushambuliwa kwa mawe hadi alipotoweka katika viwanja hivyo
Katika sakata hilo Jambo leo limeshuhudia uharibifu uliofanywa na wanachama hao kwenye nyumba ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Ole Nangoro ikiwa imevunjwa taa za nje kwa kama ishara ya kutomkubali katika utawala wake
Kwa mujibu wa Christopher Ngubiagaji mjumbe wa Halamshauri kuu ya CCM Taifa aliwaambia wanachama hao kuwa hawakuja kubatulisha matokeo, alitumwa na Katibu wa CCM Taifa Abdurahmani Kinana kuhakiki matokeo hayo yaliyolalamikia na mmoja wa wagombea
Pia alisemba mbali na hilo alikuja kuona hali ya kisiasa kwa mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM kama anaweza kupambana na mgombea kupitia umoja wa vyama UKAWA ili kuwezesha CCM kuendelea kutawala
Kufuatia kauli hiyo mjumbe huyo alisema “mwenye macho haambiwi tazama,hana shaka na kilichoamuliwa na wana-CCM Kiteto na kwamba ataenda kumwambia Kinana kuwa maamuzi wa wanakiteto yanaeleweka ili naye aweze kufanya maamuzi yake
Kauli hiyo iliungwa mkono na katibu wa CCM Wilaya Abeid Maila aliyesema kilichotokea Kiteto hakihusishwi na kiongozi yoyote, bali wananchi waliamua kutaka kujua hatma yao kuwa walichokifanya ni sahihi na wala hawataki kibadiliswe
Mwisho