Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(CHADEMA) ajiuzulu na kuhamia CCM

Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(CHADEMA) ajiuzulu na kuhamia CCM

MWITARA: Tuna tatizo kubwa sana hapa kwetu! Huko alikokwenda ndiko atahoji Ruzuku, ndiko ataonyeshwa mahesabu ya Ruzuku! Ndiko atahoji , atamhoji Magufuli asiyoyapenda? Rubbish Mwaitara! Nilikuwa na imani na Wakurya kama wakurya, anyway,,,,,
 
Mbunge wa Ukonga, MWITA WAITARA amesema anarudi CCM kwa sababu anautamani uwaziri kamili.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari leo Julai 28, wakati akitangaza uamuzi wa kuhama CHADEMA na kurudi CCM, kwa sababu yeye ni mwanasiasa na Mbunge na kwa kuwa sasa ni Waziri kivuli, hivyo anatamani kuwa waziri halisi.

“Mimi nataka kufanya kazi nataka niende mahali ambapo kuna kazi za kufanya. Nitoe wito kuna vijana wanaangalia kutoka Tarime kwenda Kakonko mimi ni ndugu yao niwaambie wasitumike watu wana mipango yao,” amesema.

Waitara amesema sababu watumishi wa umma wamekuwa na nidhamu tangu awamu ya tano ilipoingia madarakani.

“Kuna mabadiliko makubwa na sekretarieti imebadilika, Mwenyekiti wa chama ni mwingine, watendaji na mawaziri spidi ni kubwa, wanatoa majibu kwa wananchi na watu wanasikilizwa,” amesema.

Amesema mazingira ya sasa ni salama zaidi kuliko huko alipohama na hiyo ni sababu yake ya kwanza.
 
Last edited by a moderator:
Inasikitisha
Wanaojiita washirika wa maendeleo, Wanakuwa waharibifu wa Mali za umma
Hivi kutofautiana na wenzako ndio ulitie taifa hasara??
Na kama ni kweli Ofisi za chama kingine za nini?
Daaah TANZANIA yangu
 
Write your reply...mbona kila anayejiuzuru anatotoa sababu zinazofanana, RUZUKU, UONGOZI, DEMOKRASIA

Hii ndio Sumu inayo takiwa kupandwa na inayo endelea kupandwa na kuenea kwa kila Raia ili kuifuta Chadema ,option hii CCM ndio wameiona kama ndio sahihi.Ila wajue tu kama hatutokuwa na Upinzani Imara basi tutarajie kurudiana sisi kwa sisi na kuumizana zaidi sababu ya Hali ile ile ya Ubaguzi.
 
Kilichopo nikwamba Uchaguzi ujao Hakuna mBUNGE wa upinzani atarudi Bungeni so ila anaetamani kurudi Bungeni hatabaki Upinzani huyo Waitara ni mwanzo tu! Maana tutashuhudia mengi Mungu atupatie uzima tu
Jipe matumaini urefushe maisha yako.
 
Hahaa...

Mwalimu wangu wa A' LEVEL kipindi hicho aliwahi kutuambia kuwa, SIASA ni utapeli wa kuwatumia wananchi kwa manufaa binafsi.

Poleni mnaowategemea wanasiasa.

Kipindi kile demokrasia ilivyokuwa na uhai kidogo, (2015) , nilikuwa nawaona akina mama wakikata mauno na kuimba mapambio ya kisiasa.

Hali za akina mama hao ni hali hatari za umasikini wa kutisha.

Toka hapo nikajifunza kuwa SIPASWI KUMUONEA HURUMA MTANZANIA YOYOTE KWA UMASIKINI ALIONAO.
 
Hakika Mbowe somkubali na genge lake la ukabila.
Mbowe ameshindwa kujenga chama kwa sababu amezungukwa na watafuta maslahi watupu wa kabila lake.

Chadema ikitaka ipone isambararishe huu mfumo wa ukabila. Haiwezekani chama kikubwa chenye wapiga kura mil. 6 na ruzuku kubwa kiporomoke kwa kazi hii.

Kuna makabila wameweka maslahi mbele na sio utaifa.

Mbowe fanya mabadiliko kwenye idara zako na ulsbidhi chama kwa Fikra mpya.
Sayansi ya siasa imewashinda.

Tumeshauri Mara nyingi kuwa Chadema kiachane kugombana na serikali wakati huu ili kipate muda wa kujijenga kimiundo mbinu badala ya kukimbizana na makesi mahakamani.

Chadema kina wanasheria wasio na busara wanaowapotosha kwa malengo ya kupata kazi lakini sio lengo la kujenga chama.

Hivi Chadema kinashindwa kuwafunda Viongozi wake hasa wabunge na madiwani nmna ya kufanya kazi za maendeleo kama Meya wa jiji la Arusha bila kujichanganya na kukivuruga chama?

Kwa nini mbunge akatazwe kushirikiana na serikali wakati fedha za maendeleo zinatoka serikalini?

Chadema kisipobadilika kitapotea na kurudi kama 2005. Watu wameshakolea kauli mbinu ya maendeleo hayana chama na hiyo ndiyo gia ya CCM kuwaambia wananchi kuwa hawa hawataki maendeleo zaidi ya maandamano.
 
MWITARA: Tuna tatizo kubwa sana hapa kwetu! Huko alikokwenda ndiko atahoji Ruzuku, ndiko ataonyeshwa mahesabu ya Ruzuku! Ndiko atahoji , atamhoji Magufuli asiyoyapenda? Rubbish Mwaitara! Nilikuwa na imani na Wakurya kama wakurya, anyway,,,,,
Maadili na Utanzania havianzii na kuishia kwenye ufuasi/ushabiki wa vyama tu. Maadili na Utanzania vimejikita kwenye tunu za Kitaifa, mojawapo ikiwa ni kupingana na ubaguzi wa aina yoyote ile. Huwezi kuibagua jamii ya Kitanzania kwa unalohisi kuwa ni kosa la unayemhisi kuwa ni mwanajamii hiyo eti kwa sababu jina lake linasshiria hivyo. Mjadala bila ya ubaguzi unawezekana.
 
Kanunuliwa ndio na akajipanga kwa njia io ya kuelezea ruzuku. Ingekuwa Bora Kama angeeleza you hayo akiwa ndani hata angeitisha waandishi wa habari na kueleza then tuone chama ingemfanya nn. Anakuja kuyaongea baada ya kuvuta bulungutu. Amevuta mamilioni za bunge na gari juu. Bado miaka miwili anapata shangingi lingine na 2020 anapata lingine halafu hapo tunashangilia badala ya kujiuliza Ni hasara kiasi gani ametutia
Kwa hiyo na Nyalandu alinunuliwa na chadema? Ili ayaseme aloyasema?
 
Naamini hichi ndicho kilichomtoa Kinana CCM. Mtu anashawishiwa kuhamia CCM eti anahakikishiwa pia uteuzi wa mwaka 2020! Eti wanasainiana kabisa kuwa mkataba unaisha mwaka 2025.

Siasa ya wizi wizi huku tukisema tunayakataa majizi. Haya nenda kamhoji Magufuli kuhusu ruzuku ya CCM.
 
Ameona mbali sana anajua kushinda tena Ubunge akiwa upinzani itakua ngumu 2020 bora ajiengue mapemaaaa...
 
Back
Top Bottom