Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(CHADEMA) ajiuzulu na kuhamia CCM

Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(CHADEMA) ajiuzulu na kuhamia CCM

Shida yake ni kuwa waziri na hawezi kuwa waziri akiwa upinzani. Sio mbaya, Magufuli atakupa uwaziri kama ulikuaidi kabla ya kuhamia Ccm.
 
Huyu jamaa siamini kama atakuwa na uthubutu wa kupita kwa ndugu zake wakurya lazma wamngoe kichwa
 
Ukiona Baba familia yake imemshinda na kuamua kuhamia familia ya jirani ujue anaenda kuolewa. Hawezi kuwa na kauli. Watanzania wengi hawataki kutatua matatizo yao wanakimbia kimbia tu kama wakimbizi. Mimi ni mtanzania huru natoa mawazo huru, Povu sitaki mkuu.
 
Upinzani wa kweli Tanzania utasimama pale wanaojiona wana hatimiliki ya upinzani watakapokufa na kizazi kipya kutoa mawazo mapya. Ila kwa hali hii ya kuona chama fulani ni mali ya mtu fulani ikiendelea bado upinzani utakuwa na safari ndefu sana..
 
Kamanda mmoja kavua gwanda. Kachoshwa na sanaa za kimjinimjini.

Mzee Lowassa aliongea kiutu uzima akiwaambia waache na muonekano wa wanaharakati na waanze kuwa wanasiasa halisi.

Kama kawaida yao wakatanguliza ubishi wa kitoto. Ni kama vile wanafurahia siasa za kebehi na mizaha, huku pesa ikitafunwa vilivyo.
 
Wanaojielewa wote wanakuja CCM wale ambao hata kuandika Zinjanthropus hawajui ndio watabaki wakiburuzwa na mwenyekiti wa maisha.mtukufu sana Freeman aikaeli Mbowe Mangi mtetezi wa Wachaga
 
Angemalizia hivi 'najiondoa ila uchaguzi nitagombea tena" another silly drama from cheap political prostitutes!
 
Watakuja hapa kusema kanunuliwa
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Mwikwabe Waitara, atangaza kuniuzulu CHADEMA na kuhamia CCM. Kajiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

> Asema sababu ni kutofautiana na viongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA baada ya kuhoji kuhusu matumzi ya luzuku pamoja na demokrasia ndani ya chama

> Ameeleza kuwa alihoji matumizi ya Milioni 237 za ruzuku kwani mpaka sasa CHADEMA haina Ofisi Kuu, ya Kanda wala Mkoa

> Mwenge wa Uhuru umekuja kuzindua miradi ya maendeleo niliyoipigania lakini naambiwa usiende pale na mimi shida yangu haikuwa CCM pale ilikuwa ni mradi niliopigania

"Leo nimejiondoa rasmi CHADEMA kwahiyo mimi sio Mbunge tena, nimetupa jongoo na mti wake" amesema Mwita Waitara

“Mimi nataka niende mahali ambako kuna kazi za kufanya,” Waitara amewaambia waandishi na kuongeza kwamba anatamani kuwa Waziri Kamili.


Habari zaidi....

Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara amejiuzulu uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM leo Jumamosi Julai 28, 2018.

Waitara ametangaza uamuzi wake huo leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisi ndogo za CCM Lumumba mjini hapa, akiwa sambamba na katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.

Kwa uamuzi huo wa Waitara ambaye alikuwa CCM kabla ya kujiunga Chadema, jimbo la Ukonga linabaki wazi.

Waitara amekuwa mbunge wa pili wa Chadema na wa tatu wa upinzani kuhama chama na kujiunga na CCM.

Wengine wa Dk Godwin Mollel (Siha) na Maulid Mtulia (Kinondoni).
Ukiona Baba familia yake imemshinda na kuamua kuhamia familia ya jirani ujue anaenda kuolewa. Hawezi kuwa na kauli. Watanzania wengi hawataki kutatua matatizo yao wanakimbia kimbia tu kama wakimbizi. Mimi ni mtanzania huru natoa mawazo huru, Povu sitaki mkuu.
 
1.Mzee Sumae
2.Lowasa
3.Bulaya

Lengo lao wote ni kudhan kwa mda huu ni marais na mawaziri
 
kwa jinsi hali ilivyo 80% ya wabunge wote wa upinzani watahama, maana wasipohama uhakika wa kurudi tena mjengoni 2020 ni 0.001%
 
kama kuna mbunge wa upinzani anaetaka kuendelea na ubunge wake ahamie CCM mapema kabla ya uchaguzi mkuu
 
Back
Top Bottom