Brilliant internationary
JF-Expert Member
- Feb 8, 2017
- 301
- 193
Nenda salama msalimie makonda
Zitto angalijiunga na CCM wakati huo baada ya kutimuliwa kama mbwa na akina Mbowe, sasa hivi angalikuwa mbali sana kisiasa na kimaisha. Uwaziri hangaliukosa, hata uwaziri mkuu pengine angalikuwa ameukumba. Sasa ona leo anavyopata taabu sana na ubunge 2020 ataambulia kapa!Sasa na huyu tumwite msaliti au mjuzi zito aliyapigania hayo akaitwa msaliti aondolewa chamani lakini hakwenda cc
Akumbukwe zitto naomba tumuangalie zito ndio mpinzani wakweli alitukanwa sana akaitwa msaliti lakini aliendelea kuwa mpinzani nabado anajitahidi kuunganisha upinzani wasaliti nazani mmewaona sasa tatizo letu mtu akihoji kitu anaitwa msaliti sasa huyunadhani atakuwa kanusa kitu kabla hajafanyiwa kama alivyofanyiwa z ito amewawahi nakukichoma chama chadema nccr cuf act kiundwe chama kimoja rasilimali zote zavyama bilakuangali nani mdogo nani mkubwa zikusanywe tuanziehapo nahakika tutatoa maajaabu waache wajazane hukonafasi nichache nahakika kunawengine wazamani Kule wataondoka tutapata upinzani wanguvu tu
Wewe mchagga acha ujinga wa kutajataja makabila ya watu kwa ujinga wa chama chako!!MWITARA: Tuna tatizo kubwa sana hapa kwetu! Huko alikokwenda ndiko atahoji Ruzuku, ndiko ataonyeshwa mahesabu ya Ruzuku! Ndiko atahoji , atamhoji Magufuli asiyoyapenda? Rubbish Mwaitara! Nilikuwa na imani na Wakurya kama wakurya, anyway,,,,,
Sioni ajabu kwani kabla ya kwenda chadema alitokea huko huko
Mbowe anahusika na nini?Yaani nyakati tunazo hitaji upinzani wenye nguvu ndiyo unaporomoka kwa kasi.Inabidi Mbowe aachie fikra mpya ziendeshe mambo.
Mkuu hawatakuelewa hawa nyumbuzzz subiri mapovu.Hakika Mbowe somkubali na genge lake la ukabila.
Mbowe ameshindwa kujenga chama kwa sababu amezungukwa na watafuta maslahi watupu wa kabila lake.
Chadema ikitaka ipone isambararishe huu mfumo wa ukabila. Haiwezekani chama kikubwa chenye wapiga kura mil. 6 na ruzuku kubwa kiporomoke kwa kazi hii.
Kuna makabila wameweka maslahi mbele na sio utaifa.
Mbowe fanya mabadiliko kwenye idara zako na ulsbidhi chama kwa Fikra mpya.
Sayansi ya siasa imewashinda.
Tumeshauri Mara nyingi kuwa Chadema kiachane kugombana na serikali wakati huu ili kipate muda wa kujijenga kimiundo mbinu badala ya kukimbizana na makesi mahakamani.
Chadema kina wanasheria wasio na busara wanaowapotosha kwa malengo ya kupata kazi lakini sio lengo la kujenga chama.
Hivi Chadema kinashindwa kuwafunda Viongozi wake hasa wabunge na madiwani nmna ya kufanya kazi za maendeleo kama Meya wa jiji la Arusha bila kujichanganya na kukivuruga chama?
Kwa nini mbunge akatazwe kushirikiana na serikali wakati fedha za maendeleo zinatoka serikalini?
Chadema kisipobadilika kitapotea na kurudi kama 2005. Watu wameshakolea kauli mbinu ya maendeleo hayana chama na hiyo ndiyo gia ya CCM kuwaambia wananchi kuwa hawa hawataki maendeleo zaidi ya maandamano.
Kahoji bungeni 1.5bn hakupata jibu na hakukimbia.Kahoji 280m kakosa jibu kakimbia.Twende kazi,kumekucha!!!!!!Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Mwikwabe Waitara, atangaza kuniuzulu CHADEMA na kuhamia CCM. Kajiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
> Asema sababu ni kutofautiana na viongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA baada ya kuhoji kuhusu matumzi ya luzuku pamoja na demokrasia ndani ya chama
> Ameeleza kuwa alihoji matumizi ya Milioni 237 za ruzuku kwani mpaka sasa CHADEMA haina Ofisi Kuu, ya Kanda wala Mkoa
> Mwenge wa Uhuru umekuja kuzindua miradi ya maendeleo niliyoipigania lakini naambiwa usiende pale na mimi shida yangu haikuwa CCM pale ilikuwa ni mradi niliopigania
"Leo nimejiondoa rasmi CHADEMA kwahiyo mimi sio Mbunge tena, nimetupa jongoo na mti wake" amesema Mwita Waitara
“Mimi nataka niende mahali ambako kuna kazi za kufanya,” Waitara amewaambia waandishi na kuongeza kwamba anatamani kuwa Waziri Kamili.
Habari zaidi....
Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara amejiuzulu uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM leo Jumamosi Julai 28, 2018.
Waitara ametangaza uamuzi wake huo leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisi ndogo za CCM Lumumba mjini hapa, akiwa sambamba na katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.
Kwa uamuzi huo wa Waitara ambaye alikuwa CCM kabla ya kujiunga Chadema, jimbo la Ukonga linabaki wazi.
Waitara amekuwa mbunge wa pili wa Chadema na wa tatu wa upinzani kuhama chama na kujiunga na CCM.
Wengine wa Dk Godwin Mollel (Siha) na Maulid Mtulia (Kinondoni).
Na mumeo Mbowe je atarudi lini dada yangu?Mkuu umenena vema kabisa Waitara karudiana na Ex wake. Kichefuchefu kirefu sana kuona hali hii inashangiliwa kama vile habari mpya tena ya muujiza [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Watanzania hatujakata tamaa, nchi yetu imestaarabika na namna pekee ya kubadilisha jamii ni kupitia siasa. Sasa kama mpaka leo kuna watu wanapita bila kupingwa kwasababu kamati kuu ya taifa haijateua mgombea wa upinzani wafikiri wananchi tutafanyaje?Waliokata tamaa ni viongozi wa CHADEMA au Watanzania? Kwa nini unafikiri this is about viongozi wa CHADEMA?
Na mumeo Mbowe je atarudi lini dada yangu?
UCD wote hatuko kama wewe. Mimi siyo Mchaga, Mimi sina chama , CDM siyo chama changu katu. wala CCM siyo chama changu. Naangalia mustakabali wa vizazi vya sasa na vijavyo. Huyo Polepole ni takataka kama mwitara. msikilize, nitaitoa kila mara inapobidi kuonyesha kuwa ni njaa ndiyo inamsumbua Mwitara na Popole. just listenWewe mchagga acha ujinga wa kutajataja makabila ya watu kwa ujinga wa chama chako!!
Hili swala la ruzuku limekuwa likijadiliwa hapa muda mrefu sana na limewaondoa wengi hapo Chadema lakini wanachama wanaendelea kulifumbia macho tu; litawaondoa wengi sana.Hiyo siyo dalili nzuri kwa chadema 2020.