Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Mbwa aina ya Bulldog wajeruhi familia

Habari za Asubuhi Team. Usiku wa kuamkia Tarehe 8/1/2023 majira ya saa Nne usiku Familia ya Ndugu yetu Nicholaus Kunju ilishambuliwa na Mbwa na kuisababishia madhara Kwenye sehemu mbalimbali za miili yao,walio shambuliwa ni Mke wake pamoja na watoto.Walikuwa Mbwa wawili aina ya Bulldog ambao anawafuga kwa ajili ya ulinzi nyumani kwake Usagara.

Mbwa hao walimshambulia binti yake wakati ametoka nje usiku huo wa saa Nne akiwa amesindikizwa na kaka yake mara baada ya uvamizi huo kijana mwingine na mama yao walitoka kutoa msaada lakini Mbwa hawakuwatii na kuwashambulia wote.

Wote walioshambuliwa na Mbwa sio wageni kwa Mbwa hao kwani wamekuwa wakiwahudumia kwa chakula.

Baada Familia huo kujinusuru na kukimbilia ndani Mbwa waliendelea kuwa wakali na hapakuwa na uwezekano wa kuwapatia huduma majeruhi kwani hakuna alieweza kuingia wala kutoka ndani ya uzio.

Wakati haya yanatokea Kunju alikuwa kazini zamu ya usiku na alipigiwa simu kujulishwa juu ya tukio huku na kuambiwa mmoja wa majeruhi ana hali mbaya.

Tulibahatika kufanya mawasiliano na Polisi kituo cha Misungwi ili waweze kufika eneo la tukio waue Mbwa ili msaada kwa majeruhi Upatikane.

Kwa ushirikiano na Zombwe na Lenox tulifanikisha kumtoa Kunju Kazini ili akashiriki uokoaji.

Polisi walifika Nyumbani kwa Kunju majira ya saa saba usiku wakitanguliwa na watu wa Maliasili na wafanikiwa kuwapiga risasi Mbwa wote wawili na Majeruhi wakapelekwa Hospilali ya Cf kwa Matibabu.

Majeruhi wote wanaendelea vizuri.Shukrani kwa wote walioshiriki Kwenye utatuzi bila kumsahau Sheik Abdallah Omari.

View attachment 2867407View attachment 2867408
Hawa ni Bulldog pekee duniani wenye mikia mirefu kama wa mamba.
Duuh poleni,walikuwa na kichaa?!
 
Usiku wa kuamkia leo Tarehe 8/1/2024 majira ya saa Nne usiku Familia ya Ndugu Nicholaus Kunju ilishambuliwa na Mbwa na kuisababishia madhara Kwenye sehemu mbalimbali za miili yao,walio shambuliwa ni Mke wake pamoja na watoto.

View attachment 2865985
View attachment 2867418
Walikuwa Mbwa aina ya Bull dog ambao anawafuga kwa ajili ya ulinzi nyumbani kwake Usagara, Mbwa hao walimshambulia binti yake wakati ametoka nje usiku huo wa saa Nne akiwa amesindikizwa na kaka yake, mara baada ya uvamizi huo kijana mwingine na mama yao walitoka kutoa msaada lakini Mbwa hawakuwatii na kuwashambulia wote.

Wote walioshambuliwa na Mbwa sio wageni kwa Mbwa hao kwani wamekuwa wakiwahudumia kwa chakula, baada Familia hiyo kujinusuru na kukimbilia ndani Mbwa waliendelea kuwa wakali na hapakuwa na uwezekano wa kuwapatia huduma majeruhi kwani hakuna alieweza kuingia wala kutoka ndani ya uzio.

Wakati haya yanatokea Kunju alikuwa kazini zamu ya usiku na alipigiwa simu kujulishwa juu ya tukio huku na kuambiwa mmoja wa majeruhi ana hali mbaya, Tulibahatika kufanya mawasiliano na Polisi kituo cha Misungwi ili waweze kufika eneo la tukio waue Mbwa ili msaada kwa majeruhi Upatikane.

Kwa ushirikiano na Zombwe na Lenox tulifanikisha kumtoa Kunju Kazini ili akashiriki uokoaji. Polisi walifika Nyumbani kwa Kunju majira ya saa saba usiku wakitanguliwa na watu wa Maliasili na wafanikiwa kuwapiga risasi Mbwa wote wawili na Majeruhi wakapelekwa Hospilali ya Cf kwa Matibabu.

Majeruhi wote wanaendelea vizuri, Shukrani kwa wote walioshiriki Kwenye utatuzi bila kumsahau Sheik Abdallah Omari.

C & P FROM X
- Pdizaina05
Utasikia wanawake

"Wanaume wote ni mbwa tu" 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
bahati ni kwamba meno ya bull dog hayana ncha kali kama german sherfad au rottweiler,meno yao yapo kama punje za mahindi,,lakini kiuhalisia bull dog hawana akili wala kumbukumbu nzuri,na ni wazito sana wakati kuwafundisha,ni mbwa niliobahatika kuwafundisha lakini kichwani hamna ki2 tofauti na german shrfad
😂😂😂😂😂😂😂vilaza
 
Kuna matunzo ya kuwapa(tokea wakiwa wadogo) sema wabongo hatufatilii ni ujuzi kabisa unaitwa dog handling, hapo hatujazungumzia mafunzo(training).

Ukiona mbwa anasumbua, kapata malezi mabaya.

Itoshe kusema wabongo hatuwezi fuga hawa mbwa wakubwa wakubwa wakali, ni process.
Mbona wa bongo wengi tu wanafuga Germany Shepherd na hawana shida. Wako very calm na mbwa wazuri sana kwenye ulinzi. Hao pitbull ni hatari sana
 
Daah watu wanafuga Simba bila kujua hao sio mbwa wa kawaida na wana nguvu mno niliwahi kuona jamaa alimfunga na mnyororo wa kawaida kwenye pick up yake nyuma akamwacha baadae yule Bulldog alitoka kama ajafungwa kitu na kuruka nje ya gari bahati nzuri aliemfata kumjeruhi alimchapa risasi bila kujiuliza ilikua maeneo ya Centurion na muhuni aliondoka kama hakuna tukio lililotokea..
Nna ndoto ya kumfuga simba aise

Ova
 
Nilipokua.kijana mdogo kwetu nimefuga sana mbwa hawa wa kawaida.Sasa hivi nimekua baba wa familia nimefuga Germany Shephard...jike..ana miaka 2 sasa.Nimekuja kugundua kuna utofauti mkubwa sana nikilinganisha na hawa wengine....yuko composed, hapanick, habweki ovyo ovyo, royal.muda wote anakuangalia straight machoni kama vile anasubiri umwambie kitu.Akibweka mishindo miwili tu mtu wa kawaida lazima a-feel.
Nawaza nitafute Rotweiler dume, nimix
Sikushauri Mkuu Rottweiler sio mbwa wa kutegemea kiusalama ni aggresive sana, likitokea jambo hawezi kufikiri sawa sawa yeye ni kukamata na kurarua, tofauti na German shepherd au Belgian Malinois.

Ushaona wapi jeshi likitumia Rottweiler na ndugu zake kina pitbull, boureboule na bulldog. Marekani na South Africa alijaribu watumia miaka ya 1960/70s ikabuma.

Ni sawa na utumie Chihuahua kwa ulinzi 😂😂😂 ni mbwa sawa ila sio mbwa mlinzi.

Kuna mbwa wa show off pitbull na nduguze
Kuna mbwa wa ulinzi G shepherd na B Malinois
Kuna mbwa wa mapambo wakina Chihuahua na midoli wengine
 
Bulldog ni wanyama wa mwituni sio wa kukaa maeneo ya makazi ya watu. Kwenye report za uvamizi wa mbwa kwa wamiliki wao, Bulldog wanaongoza. Wenzetu nje baadhi ya familia wameshaanza kutemana na hii breed.
Mbona mnatumia jina la Bull dog katika kesi isiyo muhusu? Huyo sio Bull dog, huyo ni Pitbull. Bull dog hawapo aggressive hivyo na wengi ni wastarabu.
 
Hao mbwa kama unamfuga hakikisha unafuata masharti yake kuanzia mda wakula, aina ya chakula, mazoezi, tiba, na watu maalumu wakuwahudumia ukikosea kidogo tu ni hasara kwako na familia, mbwa wa matajiri hao, wengine tufuge tu Hawa wanao zurura Koko beach
Hawa mbwa mimi sishauri mtu kufuga kwasababu wanashida ya kuwa aggressive haraka. Mfano unaweza mtrain kwa kumdisiplini atii maagizo yako fresh tu ila siku ukafanya nae mzaha wa kumtania kidogo tu au ukafanya kitu ambacho si cha kawaida kwake na hajakipenda atakuzingua sasa kosea umpe nafasi ya kukubali akuzingue hapo ndipo utajua haujui akisha kukosea adabu mara moja ataongeza tena na tena.
 
Back
Top Bottom