Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Analia jinsi mkewe anavyompenda na kupata mke nzuri wa umbo tabia na mcha MunguKwani analilia nini jamaani. Mi niko nyuma mwenzenu.
Itakua alimkuta bikra.
Emotional wapi mgogo mshamba huyu anawdhalilisha wagogo wenzie sikatai kulia imo kutokana na uzito wa jambo lililokukuta kwa wakati huo au hata kinafki tu ili upate kitu fulani ila sio hadharani hivyo ili iweje? Ionekane anajua sana kupenda ama nini!Jamaa yuko very emotional dah
Kaniskitisha sana.
Si kila Mwanaume ana uanaume, wengine wana uvulana, niongeze sauti bandugu?Hamna mwanaume mule... anatudhalilisha sana
Nasema hiviiiii tena naandika vitu kutoka ndani ya Moyo wangu wala sio unafiki wowote
MC PILIPILI ana haki ya kulia (narudia tena ana haki) acheni nyie haya maisha watu tunapitia mambo mengi sana,watu tumetengwa na wazazi,watu tumetengwa na ndugu,tumetengwa na jamii,tumetengwa na hadi wanyama pori.
inafika wakati mtu unaamua kuingia porini ili uliwe na simba au mnyama yeyote mkali ili tu UFE uliwe upotee katika hii dunia,lakini ajabu unaingia porini unapishana na simba face to face hakugusi,unapishana na Chui face to face hakugusi.
Unalia sana sana unamuuliza Mungu kwanini sasa sifi kama hata hawa wanyama wakali hawanimalizi wananipita kama hawanioni,Mungu kimya,unafuta machozi unarudi uraiani kuendelea na ratiba zako kwa hali ya kutengwa hivyo hivyo.
From nowhere anatokea MWANAMKE anakwambia CONTROLA nakupenda, CONTROLA nimekuchagua wewe pamoja na yote hayo,nipo tayari kuonekana wa ajabu kukusaidia,nipo tayari kuonekana nisiefaa kukusaidia,nipo tayari kufanya lolote na chochote CONTROLA nakupenda from deep inside my heart.
Aseee mimi kama CONTROLA kilio nitakachoangusha hiyo siku hamna wakuweza kuninyamazisha,ntaomba mniache nilie na kweli ntalia,narudia tena ntaliaa[emoji24][emoji24], ntalia sana.Wingi wa machozi yatakayonitoka hiyo siku hakuna mtu yeyote duniani kawahi kulia hivyo.
Acheni MC PILIPILI alie acheni kabisa, nasema acheni jamani maisha haya tunapopita hapaelezeki,maisha haya majaribu tunayopita hayasimuliki,ugumu wake hamna njia nyepesi nitakayoweza wasimulia mkaielewa, halafu anatokea mtu hajulikani hata katokea wapi tena MWANAMKE pamoja na kujua historia yangu halafu anatamka maneno aliyotamka mke wa mc pilipili.
Tena sio tu anayatamka kimoyomoyo ila anayatamka wazi na peupe kwenye media Aseee mc pilipili ni nani asitoe chozi[emoji24][emoji24],ninapoandika huu ujumbe nimevaa uhusika wa mc pilipili kanirudisha nyuma sana (nimedondosha machozi) yes nasema hivi muacheni MC PILIPILI hamna anaemjua kuliko yeye ajijuavyo.
Muacheni Muacheni he is a real Gentleman tena nasema he is one among Few of his Type. Pole pilipili,Pole sana.
Mnao ona cha ajabu sana napenda tu kuwapa taarifa kuwa "mnamtukana mamba kabla hamjavuka mto" (hasa wanaume)
nimesema hasa wanaume kwa sababu ipo siku 1 leo hii unajiona mzima unatype una record voice note,una move from hapa to pale,Yes ni haki yako sana "kumuona mc pilipili wa ajabu,haki yako".
ila itafika siku 1 haya maisha its like a circle yana rotate taratiibuu itafika time yatakukuta yaliyomkuta mc pilipili,yatakukuta yalio wakuta watu walio paralyse,utakua umelala kitandani unatoa haja zote hapo hapo,miguu ina vidonda vinaoza,maisha yako ni ya shda, mama baba wamekukimbia, ndugu majirani wamekukimbia,Umebaki peke yako kitandani unaugua.
Atatokea mwanamke kama huyo mwanamke wa mc pili pili atakwambia Njopino nakupenda, Saoka nakupenda Kizzy Wizzy nakupenda kwa hali yako hiyo hiyo,nitakupenda na ntahakikisha unainuka tena kitandani,mwanamke huyo atapambana kufa na kupona hadi utasimama tena juu,utaanza kutembea.
Then baada ya kupona Mungu si athumani utaitwa mahali utaambiwa bwana flani sema kitu kuhusu mke wako,nakuhakikishia wewe unae mcheka mcpilipili leo ukiambiwa sema kitu kuhusu mke wako,kabla hujasema "A" machozi yataanza kushuka yenyewe[emoji24],na yatashuka kuliko yaliyomshuka MC PILIPILI.
Nawambia hivi ndugu zanguni wote mnao muona mc pilipili wa ajabu hapaswi kulia Mnakosea,Mnakosea na nipende tu kuwambia kuwa THIS IS LIFE (tupo sana tuombe uzima).
☺Acha uwongo we Nabii feki wa hapa Jamii Forum.
Imeandikwa wapi kuwa ni lazima umtegemee Mwanadamu 100%?
Mungu ndiye wa kumlilia sababu ndiye ashikiliaye kila pumzi ya Binadamu.
Usihalalishe ujinga kwa kigezo cha kusaidiwa na Binadamu anayepita na wakati tu bali jitegemeze kwa Mungu asiyedhuriwa na muda yani yeye ni Alfa na Omega(mwanzo & mwisho) sababu Watu wanaweza kukutenga na kukukimbia ukiwa katika shida lakini kamwe Mungu hawezi.
Hapa sasa umenena vyema.CONTROLA,
Sasa huko kwenye media si ndiko watu wanako pretend kwa sana na show off?!
Yani ulitegemea iwe kinyume chake?!
Siyo kila yanayofanyuka kwenye media wanamaanisha , fahamu hivyo.
Wengine kwenye macho ya watu wanajidai kupendana lakini wakiingia ndani ya nyumba kulala kila mtu na chumba chake [emoji108][emoji108][emoji108]
Kuwa uyaone mdogo wangu!
Wala usijilinganishe na mtu mwingine au ku admire life style ya mtu au watu fulani siku ukija kuujua ukweli wa maisha yao utachoka mwenyewe!
Tafuta kumjua Mungu , soma au fanya kazi kwa bidii, heshimu watu wote, jifunze kuwa na tabia njema itakayo kuwezesha kuishi popote na mtu au watu wowote .
Kuwa tayari kukiri makosa unapokosolewa na kuwa tayari kujifunza kubadilika ndipo utakapopata kibali machoni pa Mungu na wanadamu.