Mchengerwa: Yeyote atakayejaribu kuichezea Serikali hatutamuacha salama

Fortilo

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
5,807
Reaction score
17,416
Mchengerwa ameyasema hayo akiwa Rufiji mkoa wa Pwani.

Swali.

Hivi nchi hii nani anataka kuvuruga amani?
Na Mchengerwa anadhani anatisha wengine yeye kama nani, yeye sio IGP, RPC wala sio waziri wa mambo ya Ndani.

Hii kibri anapata wapi?

"Yeyote atakayejaribu kuchezea serikali hatutamuacha salama hata kidogo, hatutakubali hata kidogo. Misingi ya taifa letu Baba wa Taifa alikwishaiandaa, na sisi vijana wa karne hii tuliopata bahati ya kushuhudia utawala wa Rais wetu wa Awamu ya Kwanza [Hayati Julius Nyerere] tumesema taifa hili litaendelea kuwa na amani na utulivu."
 
Hana maana huyo maana Rufiji kumejaa ufukara wa kutupwa hakuna barabara ya maana. Ukitoka pale Temeke Sudani kwenda Mloka unafika saa 12 jioni. Yaani kule kwetu nadhani kuna laana ya maisha. Huyo kafungia Kiredio anaonekana mkombozi kweli apambane na ufukara wa Rufiji yote halafu aje na viroja vyake. Huyu hakufaa kbs kuwa Waziri. Very bogus man.
 
Watanzania waoga hivyo alivyoongea kuna watu washatetemeka utaskia "tusameheee mh!! mamkweo anaupiga mwingi baba"!!! Mkikosea tuogope kukosoa maana hamtakubali hata kidogo???

Wewe waziri Tamisemi sio? Karne hii mwalimu kaenda kusimamia mtihani wa taifa darasa la saba analala chini manake Nini??

Naskitika sana nimegombana na mke wangu nimedraivu kwenda kumtoa akakataa Kwa woga atafukuzwa kazi, kapelekwa vijiji vya mbaliii, mwanamke mwenyewe wengine madume, umeme hakuna, analazwa ofisini Tena chini... is that fair??

Ndoa yangu Iko salama hapo? Mkeo angeenda? Au saivi yuko kwenye kiyoyozi na kitanda Cha milioni 7 Toka ulaya kwanguvu ya mamkweo na kodizetu?!!?

Mnawatesa na kuwatisha walimu/wananchi halafu mnafokafoka kama mnajua mnachofanya!!! SHAME
 
Mchengerwa ameyasema hayo akiwa Rufiji mkoa wa Pwani.

Swali.

Hivi nchi hii nani anataka kuvuruga amani?
Na Mchengerwa anadhani anatisha wengine yeye kama nani, yeye sio IGP, RPC wala sio waziri wa mambo ya Ndani.

Hii kibri anapata wapi?
Unauliza kibri anaipata wapi wakati anakemea watu wanaojaribu kuichezea salama na amani yuliyonayo?

Kwanini huwaulizi wajivuni wanaotaka kuichezea amani? Kibri hiyo wanaitowa wapi?

Au na wewe ni katika hao wanaotaka kuharibu amani ya nchi?
 
Webibi ameeleza niwatu gani specific au anatisha watu jumlajumla!! Awataje live niwapi hao anaowakusudia je niwale wapinga katiba mpya? Au niwale wanaogawa rasilimali kama bandari Kwa mikataba ya hovyo, au niviongozi wazembe wanaotafuna kodizetu? Au viongozi wanaopeana vyeo kiundugu mfano wakwe kuteuana? Au niwanaoiweka nchi gizani? Au wabunge walojiongeza posho na mishahara? Au wanaoibaga kura? Au wanaosababisha mafuta yawe shida? Au wanaopinga wizi,udhalimi na matumizi mabaya ya kodizetu?
Niwepi haswaaa??? inaonesha umelewa vyema! Au Nivile huyu ni mwenzio ktk Imani basi unashedadia...
 
Webibi ameeleza niwatu gani specific au anatisha watu jumlajumla!! Awataje live niwapi hao anaowakusudia je niwale wapinga katiba mpya? Au niwale wanaogawa rasilimali kama bandari Kwa mikataba ya hovyo, au niviongozi wazembe wanaotafuna kodizetu? Au viongozi wanaopeana vyeo kiundugu mfano wakwe kuteuana? Au niwanaoiweka nchi gizani? Au wabunge walojiongeza posho na mishahara? Au wanaoibaga kura? Au wanaosababisha mafuta yawe shida? Au wanaopinga wizi,udhalimi na matumizi mabaya ya kodizetu?
Niwepi haswaaa??? inaonesha umelewa vyema! Au Nicole mwenzio ktk Imani basi unashedadia...
Yeyote.
 
Kule Kibiti na Rufiji kulikuwa "terrorist safe haven"...

Mh.Mchengerwa anaongelea wale magaidi waliokita kambi huko na kutaka kutuchomea moto nchi yetu.....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Unauliza kibri anaipata wapi wakati anakemea watu wanaojaribu kuichezea salama na amani yuliyonayo?

Kwanini huwaulizi wajivuni wanaotaka kuichezea amani? Kibri hiyo wanaitowa wapi?

Au na wewe ni katika hao wanaotaka kuharibu amani ya nchi?
....ni katika haohao

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mathalani hivi Mbowe ni wa kumbagua mh.Rais kwa UZANZIBARI wake ?!!

Hii si "bigotry" kweli ?!!

Nini madhara ya baguzi hizi?!!!

Havoc

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mchengerwa ameyasema hayo akiwa Rufiji mkoa wa Pwani.

Swali.

Hivi nchi hii nani anataka kuvuruga amani?
Na Mchengerwa anadhani anatisha wengine yeye kama nani, yeye sio IGP, RPC wala sio waziri wa mambo ya Ndani.

Hii kibri anapata wapi?

View attachment 2747361
KWANI WEWE Fortilo ULIKUWA NA MPANGO WA KUIVURUGA AMANI YETU WATANZANIA?, KIPI KIMEKUCHUKIZA?
 
Hana maana huyo maana Rufiji kumejaa ufukara wa kutupwa hakuna barabara ya maana. Ukitoka pale Temeke Sudani kwenda Mloka unafika saa 12 jioni. Yaani kule kwetu nadhani kuna laana ya maisha. Huyo kafungia Kiredio anaonekana mkombozi kweli apambane na ufukara wa Rufiji yote halafu aje na viroja vyake. Huyu hakufaa kbs kuwa Waziri. Very bogus man.
Mmechukizwa kweli wenye malengo ya ugaidi na wote msioitakia mema Tanzania yetu.
 
Back
Top Bottom