Mchungaji aliedai Corona ni kagonjwa kadogo mbele ya Mungu, amefariki kwa Corona

Mchungaji aliedai Corona ni kagonjwa kadogo mbele ya Mungu, amefariki kwa Corona

yah yupo sahihi na huo ndo ukweli na utabaki hivyo milele
allah akbar
Huyu alikaidi maagizo ya kuzuia mikusanyiko mikubwa zaidi ya watu kumi ili kujilinda na kutoambukizana. Huyu alitaka waumini wake wasiogope coronavirus akidai Mungu atawalinda na hivyo waendelee tu kama zamani. Alichosahau huyu Askofu ni kwamba Mungu anakutaka ujilinde, Mungu hajaribiwi.
 
Binafsi ninaona yuko sahihi kwa 100%, kwa sababu ameendelea kumuona Mungu ni mkuu katikati ya vitisho vya kufa kwa Corona.

Katikati ya mambo yote, Mungu atabakia kuwa Mungu. Na katika mambo yote Mungu ni mkuu.
Hakuna anayepinga kwamba Mungu ni Mkuu, huyo atakuwa ni mfuasi wa shetani. Lakini kama unajua kwamba unachofanya ni hatari, halafu unakifanya kwa kumjaribu Mungu, huna tofauti na shetani mwenyewe.
 
Huyu alikaidi maagizo ya kuzuia mikusanyiko mikubwa zaidi ya watu kumi ili kujilinda na kutoambukizana. Mungu anakutaka ujilinde na siyo kumjaribu.
Kama alikaidi kujiepusha na mikusanyiko wakati wataalamu wakimuonya, maana yake iliutafisiri vipaya uweza wa Mungu na ukuu wake dhidi ya COVID 19. Na hapo ni haki kwake kuvuna alichopanda.

Mungu hawi radhi na wapumbavu, na Mungu anasema mwanadamu akiyakosa au kuyakataa maarifa, kitakachompata ni kuangamia. Na katika hilo Mungu awezi kusimama kukutetea, maana umeyakataa maarifa, ambayo ni yeye aliyaleta.

Tabu kubwa sana ni kuwa, washika dini wanajaribu kumtenganisha Mungu na Maarifa(sayansi), wakati Mungu mwenyewe anasema kumfuata yeye ndio chanzo cha maarifa (sayansi).
 
But his death doesn't change the truth of what he said. He may be weak in faith of what he said but I don't think someone here believes COVID19 is too big for God to handle unless you're Pagan.
Matthew 4:5-7
5 Then the devil took him to the holy city and had him stand on the highest point of the temple. 6 “If you are the Son of God,” he said, “throw yourself down. For it is written:

“‘He will command his angels concerning you,
and they will lift you up in their hands,
so that you will not strike your foot against a stone.’[c]”

7 Jesus answered him, “It is also written: ‘Do not put the Lord your God to the test.’[d]”
 
Haijalishi kama imemuua na haikufaa kuhusianisha maneno yake na hill lililotokea lkn tunajua wafuasi was yule muovu wapo Ila hawatoshinda!! itabaki hivyo Mungu ni mkubwa kuliko jambo lolote.

Sema hizi nchi ambazo watuwake wanakula wanyama wa ajabu ajabu zikemewe maana wanaleta maradhi yasiyoeleweka duniani.... Congo wanakula sana.

mambwa,manyani,mbilikimo wamezua ebola kisha hawa wachina wala majoka, konokono, polo, mambwa wamezua covid 19 inabidi tuwaweke sawa wale vitu OG wastuletee majanga kwa tamaa zao..
 
Mag3,
EeenHee, Mag3 leo anatoa somo.

Mtu anaona 'an 18 wheeler' linakuja mbio, yeye anakaa katikati ya barabara, na kuwahimiza wenzake wasiogope kwa kuwahadaa tu kwamba Mungu ni wao?
Wanazo nguvu za kumwamrisha Mungu afanye wanavyotaka wao?

Wengine wanadhani wanaweza kumhonga/kumpa rushwa Mungu - eti mikusanyiko kwenye nyumba za ibada hawaoni kuwa ni hatarishi kwa raia wao!
 
Mungu anafanya yote ili mapenz yake yatimizwe, no matter tutakufa au tutaish
Sizani kama kunahaja ya kuogopa kifo bali ni upumbavu kufa kizembe na ni dhambi pi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umekosea sana!! Bado COVID -19 ni kagonjwa kadogo sana mbele ya Mungu. COVID -19 ni ugonjwa mkubwa sana mbele ya wanadamu lakini si mbele ya Mungu.
Bado hatujaelewa sana, yawezekana kabisa covid-19 ikawa ni pigo toka kwa Mungu kwa ajili ya uovu uliopo duniani. Ndio maana Rais wetu Mheshimiwa sana Dr Magufuli alinukuu maandiko akasema " Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu wakijinyenyekesha na kutubu dhambi zao ........".
Hapo Mungu ameweka masharti: Lazima kujinyenyekesha na kutubu!! Chini ys hapo pigo lipo pale pale!! Kwa hiyo jambo la kwanza ni kujinyenyekesha na kutubu kisha kukiri ukuu wa Mungu juu ya pigo hili kuwa kakorona ni kadogo sana kwa Mungu.
Tatizo watu hawataki kutubu! Katika mazingira hayo ni kujidaganya kudhani kuwa Mungu ataonyesha ukuu wake katika shida zako.
Mahali pengine kwenye Biblia panasema: "Mkono wa Mungu si mfupi hata asiweze kuokoa bali MAOVU yenu yamewafarakanisha na Mungu wenu"
Umefanya kosa kubwa sana la kumchokoza Mungu kwa kujaribu kutoa picha kwamba kwa kuwa huyo mchungaji smefariki basi kcovid-19 ni kubwa au ina nguvu kuliko Mungu.
Ushauri wangu: Tubu kwa dhati na Mungu atakusamehe. Vinginevyo utajua mwenyewe!!!
Na wewe subiri ukudake ndipo utajua kama kutubu kwako kulisaidia au hapana,nyie ndio Kibwetele
 
Hatukatai Mungu ni mkuu kuliko korona ila usimjaribu Mungu mbona ni Mkuu kuliko njaa lakini tunakula shinda njaa basi ili Upime ukuu wa Mungu,Mungu siyo wa kuonja. Fuata kanuni za maisha
 
Bado haibadilishi ukweli kuwa Mungu ni mkuu sana, na si wa kulinganishwa na corona.
Mungu ni muumba wa mbingu na nchi na viumbe vyote vilivyomo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daud Bashite Naibu Rais yeyea anaamini Ndumba kupitia majini vinazuia corona, kakubali kutoa mapesa mengi kwa Le mutuz kwenda kumletea waganga wa kienyeji kibao eti watamsaidia kuzuia corona, le mutuz anakula pesa za Daud Bashite kwa njia haramu
hahahaha,, mjini mipango

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1419301
Askofu Gerald Glenn wa Kanisa la New Deliverance Evangelistic Church, Virginia USA.​

Kwa habari zaidi bonyeza hapa chini...

Gerald Glenn: Bishop who said 'God is larger than this dreaded virus' dies of Covid-19
Aisee umeileta hii on time. Baada ya kuingalaia kwenye TV nilikuwa pia nataka kuileta kwa maana ya kukumbushana kuwa kwenye mambo haya tusikubali kudanganywa wa wahubiri uchwara wasiokubaliana na sayansi. Hata pope Francis siku hizi hafanyi mahubiri mbele ya watu wengi, yeye ni mwanasayansi (Chemist), lakini hawa ambao ukishaingia kanisani wanapitisha bakuli tena la nguvu ambapo makusanyo hayajulikani yanakwenda wapi ni wa kuogopa sana. Wao wanataka watu waende kanisani na kuacha sadaka kuliko jambo jingine lolote. Kuna mmoja aliwaambia wafuasi wachangishe hadi anununue private jet.
 
Mungu ni yuleyule Jana, Kesho na milele, Hafanyi kazi yake Kwa mashinikizo ya watu, Ajibu asijibu bado ni Mungu tu, useme ni Mungu asiyeshindwa ama la, Bado Yuko vilevile na Wala hajawahi kuwa na upendeleo, vitu Vyote aliumba yeye na hivyo hivyo Hana mashariti pindi anapovuna mazao yake, uwe unamwamini au kutomwamini atakuvuna Tu!!! Haleluuuya
 
Back
Top Bottom