Mchungaji Msigwa agoma kupanda gari za CCM, alakiwa na wana-CHADEMA

Mchungaji Msigwa agoma kupanda gari za CCM, alakiwa na wana-CHADEMA

Imebuma labda zitumike kumlipia mwingine Mbowe au mnyika msigwa ashasepa

Mkuu zimelipwa ila hajatak kuongea na waandishi
Hii ni km unakutana na demu bar mnaahidiana kulala naye.demu anakunywa bia nyingi weee ukijua unaenda kula mzigo .demu anapitia chooni huyoooo😠😠😠😠..so hapa Rais wenu alijua atakula mzigo...! Tumbafu!
 
Mh. Rais na Msigwa ni ndugu na pia ndugu wa Msigwa waliomba mchango kwa mh. Rais baada ya kujichanga na kupata 2 mil, ikabakia mil 38, Mh. Rais akatoa kwa huruma kama ndugu yake baada ya kuombwa. Sasa hapo kuna ubaya gani? Sema Msigwa ana deko sana ila atapata shida siku moja na atakosa msaada kabisa, shauri yake
Hoa ndugu wa Msigwa anawekwa ndani kila siku huko Iringa ndio waje kufanya drama huku ....siku zote Msigwa anapelekwaga Segerea mbona hawaendi kumpelekea uji ...
Siasa za Kitoto na za kumdhalilisha hata rais mwenyewe ....Tatizo Kazungukwa na watu shallow sana kiuelewa ...sasa ndio nini hii kama sio aibu tu kwa Urais
 
Pambafu kabisa nyie.. mmeonja nguvu ya umma.
20200312_183952.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa amekataa kupanda gari la serikali lililopelekwa gerezani Segerea ili kumchukua baada ya kulipiwa faini.

Awali kulitokea mzozo kati ya wafuasi wa CCM wakiongozwa na Ndugu Humphrey Polepole ambao walitaka Msigwa apande gari ya serikali kwa madai kuwa amelipiwa faini yake na Rais JPM, lakini wafuasi wa Chadema wakamtaka apande gari aliloandaliwa na Chadema kwa kuwa chama hicho ndicho kimemlipia faini kupitia michango ya watanzania.

Wafuasi hao walidai kwamba wakati Rais JPM anapeleka fedha tayari Chadema ilikua imeshamlipia Msigwa na hivyo fedha hiyo irudishwe kwa Rais ili ikafanye shughuli nyingine za maendeleo.

Kufuatia mzozo huo wafuasi wa Chadema walizuiwa kuingia gerezani humo na wafuasi wa CCM wakiongozwa na Polepole waliingia wakiwa kwenye magari ya serikali tayari kumlaki Msigwa.

Lakini Msigwa alikataa kupanda gari ya serikali aliyoandaliwa na kutembea kwa mguu hadi nje ya gereza walikokuwa wafuasi wa Chadema ambao wamemlaki kwa shangwe na sasa anaelekea makao makuu ya Chadema, eneo la Kinondoni ili kufanya mkutano na wanahabari.!
Haahaaa... What a play... Lets see how this is gonna end!
 
Mchango wa mh Rais umesaidia sana,
Chadema iliomba msaada wa michango Kwa wananchi wote Na Rais JPM kaitikia ombi lkn pia familia ya mchungaji msigwa imeomba msaada kutoka Kwa Rais Na Rais kakubali ombi, tatizo linatoka wapi?
Hongera sana Kwa Rais
Chadema walitoa account no.hela zitumwe huko ye kapeleka benki kakuta chadema wameshalipa ye akajengee daraja huko kiegeya magari yapite

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa Msigwa akiongea hovyo, tunamrudisha mahakamani, achunge ulimi wake, si anaringa tumejaribu kumsaidia hataki, sasa akienda mahakamani tena hakuna msaada tena hata akiita Magufuliiiiiii njooooooo baba njooooo Mh. Rais njoooooooo hakuna tena kumsaidia.. Shauri yake [emoji28][emoji28][emoji28]
Tutachangia tena sisi wananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nchi kuendelea sijui kama itaendelea . Jamhuri inamshtaki mtu .. anahukumiwa kutoa faini , watu wanajichanga ili wamtoe ... Halafu sehemu ya jamhuri ambao ndio walimshtaki Huyo mfungwa wanajichanga na wao wamtoe mtu waliomshitaki ... Hahaha hii nchi Mungu ndio anajua tunakoelekea...


Mungu Kama upo kweli tuondolee hizi aibu ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom