Pre GE2025 Mchungaji Msigwa atangaza kukata rufaa kupinga Ushindi wa Joseph Mbilinyi (Sugu) Kanda ya Nyasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni yeye anasema hivi, au wewe?
Si walienda mpaka kwenye mdahalo star tv kwa odemba

Maswali:
Angeshinda yeye angelalamika?

Ushindi wa ndani ya chama Ni kwa faida ya Nani?

Yeye kaongoza muda wake Ni vyema sasa Ni muda Sasa aachie akili mpya iongoze nyasa

NB.
Eg. Kikwete vs mkapa mwaka 1995 mbio za uraisi alitoa speech nzurii Nanukuu ""Tunatoka hapa TUKIWA wamoja zaidi""

Msigwa alitakiwa aseme TUMEMALIZA UCHAGUZI NA TUMETOKA HAPA TUKIWA WAMOJA ZAIDII
 
Kama asemayo mchungaji yana ukweli; hata chembe ndogo tu ya ukweli, basi huyo virusi ndani ya chama atakuwa ni hatari sana kwa uhai wa chama chenyewe. Huyo kirusi siyo wa kuchezewachezewa na kujifanya chama hakimuoni.
Ngoja twende kwenye kamati kuu
 
Msigwa alitakiwa aseme TUMEMALIZA UCHAGUZI NA TUMETOKA HAPA TUKIWA WAMOJA ZAIDII
Kwa hiyo hata kama aliona dosari, alitakiwa akubali au siyo?

Ni hivi, wewe na mimi hatujui kilichotokea katika uchaguzi huo. Haitoshi tu kusema kwa kuwa Mchungaji kishaongoza, basi asilalamike kama anaona kuna dosari hili halina maana yoyote. Kama anaona alichezewa rafu, ni haki yake kueleza hivyo na kuomba chama kiliangalie hilo analolalamikia.
 
Kura alihesabu nani? hakuwa na wakala? Au hakwenda mwenyewe kusimamia kura zake kwenye majumlisho?
Alitakiwa kuwepo hata kule wajumbe walipopewa laki tano hadi milioni; si ndivyo unavyosema wewe hapa?
 
Alitakiwa kuwepo hata kule wajumbe walipopewa laki tano hadi milioni; si ndivyo unavyosema wewe hapa?
Wewe unaamini Msigwa hajatowa pesa? au amezidiwa dau?

Kwahiyo waliompigia kura 52 wao hawakupewa pesa?

Kwanza anawadharirisha wajumbe.
 
Wewe unaamini Msigwa hajatowa pesa? au amezidiwa dau?

Kwahiyo waliompigia kura 52 wao hawakupewa pesa?

Kwanza anawadharirisha wajumbe.
Hapana, siamini hivyo hata mara moja.
Kama na yeye kata chochote na kazidiwa dau na mwenzie, sidhani kwamba hilo ndiyo iwe sababu ya kumzuia asilalamike.
Kwa upande wangu, kama ni hivyo unavyo eleza wewe, basi wote hawafai kuwa viongozi.
Kamati Kuu ya chama iwasikilize wote na kama itabainika wote wanahusika, basi chama kina jukumu la kusahihisha hali hiyo,, na siyo kuifumbia macho.

Kamati Kuu ikiruhusu upumbavu huo, basi hakunma matumaini yoyote kwenye chama hicho; kwa sababu hakitakuwa tofauti na CCM wanaowachezea mchezo huo sasa hivi.

Pesa ya waarabu itaitesa sana nchi hii sasa hivi.
 
Hata ACT sio cha upinzani kwani😁😁😭
 
Ya chadema waachie chadema mkuu
 
Hiyo ndio demkrasia tuitakayo, si mambo ya fomu moja ya uchaguzi.
 
Sasa kwa nini wachezewe akili namna hiyo kama wao ni watoto wachanga.

Maana yake ni kwamba wote wanaonekana kutokuwa imara katika wanayoyasimamia.
Urafiki wa Msigwa na ASAS una historia ndefu tangu 1980s hivyo kumfadhili siyo kumnunua
 
Naiona chadema ikisambaratika endapo itashindwa kushughulikia kwa weredi ukigeugeu huu wa Msigwa. Kuna mkono wa adui nyuma ya Msigwa.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa aliyemaliza muda wake na kushindwa katika Uchaguzi uliompa ushindwa Joseph Mbilinyi (Sugu), Mchungaji Peter Msigwa amekata rufaa kupinga Uchaguzi huo akidai ulivurugwa
-
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Msigwa amesema Uchaguzi huo ulitawaliwa na Mbinu Chafu ikiwa ni pamoja na Wasimamizi wa Uchaguzi kuwazuia Makatibu Watatu wa Mabaraza kupiga Kura kinyume na Katiba ya Chama hicho

#JamiiForums #Democracy #JFDemocracy #CivilRights
Your browser is not able to display this video.
 
Ndiyo demokrasia yenyewe hiyo. Hajatenda kosa lolote kwa kuita vyombo vya habari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…