Hakuna cha kujitetea hapo.Katika basics za kufundishwa,si mtoto wa kike tu,watoto wa jinsi zote ni:-
NAMBARI ONE-kuwatambua watu na kuwasalimu kadiri ya umri.Hapo ameshafundishwa kuongea.
MBILI-kujua kujisaidia sehemu na wakati sahihi.
TATU-kujiswafi mwili na kusafisha vyombo,mazingira na nguo kulingana na anavyokua.
NNE-Kupika(kuchemsha,kutokosa,kubanika,kukaanga)vyakula na kuandaa vinywaji na matunda.
Mzazi au mlezi kushindwa kumfundisha mtoto wako mambo hayo,inaonesha ni mzembe,hujielewi,humpendi mtoto na humtakii mema katika safari yake katika jamii.
NB;Hii ni kwa families zote i.e zenye kila daraja la maisha kiuchumi.Kwake mtoto;Kama hashtuki wala kujishtukia kwamba hadi umri wa miaka 15 hajui hizo basics,naye ni boga tu anayefanana na bogus!
Mimi pamoja na kuwa mwanaume tena nunda/uninja wangu,nilipelekeshwa kijelajela na mikong'onto mingi hadi nikajua kufua,kupika,Kuosha vyombo,kufagia na kudeki kwa umaridadi.