Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 22,502
- 48,479
Mkuu, ukichunguza kwa makini nadhani suala la fursa sawa huku majukumu yakibaki vile vile lina mchango mkubwa.Ndiyo maana mmomonyoko wa maadili umekuwa Mkubwa miongoni mwao
Naihurumia taasisi ya ndoa, maana ipo vitani kwa muda sasa 🙌
Mfano: jamii ina mabinti 6 na vijana 6, wote wanasomeshwa kupigania fursa 6 za kipato. Meaning fursa 6, watu 12.
Katika hao watu 12, ikitokea mabinti 3 wakazipata fursa it means Fursa 6 zimeenda kwa mabinti 3 na vijana 3.
Mtihani unakuja jamii inapotaka vijana wafunge ndoa huku kijana na binti wakibeba tamaduni zile zile kuwa kijana ahudumie familia kikipato, binti atunze mume na watoto.
Sasa:
Mabinti wapo 6.
Wenye elimu wapo 6.
Wenye kipato wapo 3.
Vijana wapo 6.
Wenye elimu wapo 6.
Wenye vipato wapo 3.
Embu tengeneza scenario ambayo kila binti anaingia kwenye ndoa na kuhudumiwa kikipato huku akimuhudumia mume bila shida kama jamii inavyotegemea.