Tumemsikia sote wakati anatamka hiyo kauli, Mimi mwanayanga nikimwambia Mh. Job Ndugai "Jana tumekunyoa kwa wembe" itakuwa nimekosa staha?
Mama alisema "Ukinizingua , nakuzingua" .. Je ina tofauti na kauli ya Mdude kuwa "Akizingua na yeye atazinguliwa kama walivyomzingua mtangulizi"
Ni kweli hatujui wembe alioumaanisha Mdude kwenye hiyo Kauli, Kama anasema Wembe waliomnyolea JPM ndo watautumia. Je, ni kweli JPM alinyolewa Nywele kama mnavyotaka kumaanisha?. Kwa hiyo "Mtoto akililia wembe aachwe ajikate" nayo haijaelewekaga kwa jamii yetu pia?
Tuache kujipendekeza sana. Tatizo letu sisi ndo yale mambo ya utu wa kiafrika ambayo tunayalazimisha. Kijana amemwambia hivyo Rais wa nchi, siyo mama yake kama inavyotaka kuonyeshwa. Nyumbani Mkubwa akosei , lakini unapokuwa mtumishi wa Umma ni lazima ukosolewe, kutahadharishwa na kusifiwa pia ikibidi. Kama hujajiandaa kwa haya usiombe nafasi ktk ofisi.
Tujiulize Staha ni kumpa mashtaka ya uongo na kumtunza gerezani siku 414? Mdude leo anaonekana 'drug dealer' mtu ambaye havuti hata sigara, nani amemuomba radhi? Halafu mnataka kumpangia jinsi ya kutoa maoni yake na hata hisia zake mnataka kuziratibu... Nyie hisia zenu nani anaziratibu?
Ieleweke wazi ukiwa ofisi ya Umma, kubali kukosolewa, kusemwa, kuhadharishwa. Muradi Katiba na sheria za nchi zisivunjwe.
ANAYEONA MDUDE AMEKOSEA, ANAWEZA KWENDA MAHAKAMNI KUMSHITAKI AU KUPATA TAFSIRI YA KISHERIA
Ukisikiliza hii nyimbo , jiulize hiyo "Mbwai na iwe Mbwai" ni nini?. Ndo staha?. Lakini kiuhalisia ina maana nyingi na inaweza isiwe hiyo ya shari tunayohisi imemaanishwa na waimbaji.