Mdude Nyagali, siasa zako sio nzuri. Jirekebishe


Umeandika mengi from nowhere. Uliweza kuiona comment #8 pia?

Kumbuka nimeonyesha walichofanya CCM ni jinai. Pia nimeonyesha mafanano ya aliyofanya Mdude na yule bwana wa Zanzibar.

Ninakazia Mdude hajafanya kosa lolote kisheria. Kama mnaona lipo mpelekeni mahakamani.

Ikiwapendeza zaidi na mwingine huyu hapa:



Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Upo sahihi kabisa, mtu kafanya ujinga na wewe mstaarabu na mwenye busara unafanya ujinga huo huo tena! Huu ni upumbavu ambao wenye busara hawawezi kuuafiki.

Nilitegemea chadema yenye watu busara basi wasiige mambo maovu yaliyofanywa na uongozi mbovu uliopita!

Ila sasa kama wao ndo wanafanya waliyokuwa wanayapinga basi, uongozi wa mama ndo sahihi na chadema ndo waovu!

Haiwezekani uilichokuwa unapinga wewe ukapata nafasi ukaanza kufanya ujinga huo huo!! Ni upumbavu huu,
 
CCM ni tembo na msamba wake ni wa tembo chadema ni bata mwenye msamba wa Tembo kwa sasa.
msirudie!!
Jingalao:Vipi unakumbuka ule wimbo wenu wa CCM unasema ,"Wembe ni uleule ushindiii*2"
Pia Kuna msemo Huwa unasema "Mwenzako akinyolewa zako tia maji"

Nazani mdude lengo lengo lake alimaanisha kuwa Mheshimiwa Rais Wetu Samia asifate njia ambazo sio nzuri kutoka kwa mwendazake katika uongozi wake na kuonya ikiwa hatafata katiba katika kuongoza basi mdude hatanyamaza na atamkosoa kama alivokua anamkosoa JPM.
 
Chadema isipojitenga na watu aina ya Mdude itakuja kuwa chama cha hovyo kuwahi kutokea!

Aidha wamfunde namna kutengeneza hoja au waachane naye kusimama kwenye majukwaa. Otherwise anawavua nguo na kuwaacha na aibu!

Tunategemea chadema ya akina Dr Slaa inayojenga hoja nzito ambazo ukizitoa basi watu wanona uzito wa jambo.

Sii hoja za matusi. Tunahitaji katiba mpya ila si kwa kumtukana mkuu wa nchi!

Tutoe hoja nzito ambazo kila mtu ataona umuhimu wa hiyo katiba mpya na siyo matusi! Jitengeni na watu aina ya mdude au mfundisheni kujenga hoja na siyo matusi!
 
Nimekuwa nawasapoti CHADEMA kwa siasa zao Ila matusi yanayotupwa humu kila hata tunaposhauri japo wengine hayupo CCM inakuwa matusi tu, basi waendelee sasa . Enough with ujinga.

Kuna wakati wanapaswa kutumia busara sio kila wakati tutukanane tu. Na sio kila anayeshauri ni CCM
 
Hivi ni lini maccm yaliomba radhi kuhusu kauli hii ya huyu taahira!?


 
Vipi kuhusu maovu ya kutisha nchi nzima ya yule dhalimu mwendazake na washirika wake maccm waliwahi kuomba radhi kwa Watanzania!?


 
Hivi ni lini maccm yaliomba radhi kuhusu kauli hii ya huyu taahira!?

Unajua ukiwa umevua nguo na ukawa upo beach unaogelea na chizi akaja akachukua nguo zako wewe usitoke kwenye maji na kuanza kumkimbiza.

Ukirogwa kutoka kumkimbiza atakayeonekana chizi ni wewe mzima unayemkimbiza chizi kweli.

Naamini nitaeleweka ndugu zangu.
 
Vipi kuhusu maovu ya kutisha nchi nzima ya yule dhalimu mwendazake na washirika wake maccm waliwahi kuomba radhi kwa Watanzania!?

Kumbe mkuu akili yako ni sifuri kwa hiyo kwa kuwa unavyoona wewe mwendazake hawakukufurahisha na walikuwa dhalimu kwa hiyo ni sawa kwa watu wengine nao wafanye ujinga? kweli SACCOS mumeishiwa! ujingawenu hauwafikishi kokote ,tunataka sera za siasa safi,huko kufukua makaburi na kuwataka watu waishi kwa visasi hakuwasaidii, wewe baki na kuhoji ya mwendazake,kila kitabu kina zama zake.
 
Mfano wako hapa hauna mashiko Mkuu, hapa tunaongelea maisha ya Watanzania chungu nzima waliombambikiwa kesi, kufukuzwa kazi kidhalimu, kuvunjiwa nyumba zao kinyume cha sheria, kuporwa bilioni zao na wengine kupotezwa bila hata miili yao kuonekana pamoja na ndugu zao kuipigia magoti Serikali lakini Serikali imekuwa kimya bila msaada wowote. Kwanini hili la Mdude lipewe uzito mkubwa sana kuliko dhuluma na udhalimu wa kutisha uliofanywa kwa Watanzania wengi tangu 2015?

 
Mdude aombe radhi amefanya kosa gani kisheria?middle class wa nchi hii wanatia aibu,woga umewatawala mpaka mnaogopa kivuli chenu,ningependa mtu aandike kosa hapa la kisheria alilolifanya Mr.Mdude then tujadili,kuna clip ya President Samia aliyobeza kupigwa risasi kwa Mr.Lisu mbona hailalamikiwi humu au President yupo above law?kama huna mada ya kuleta humu kaa kimya sio kuja na utumbo kama huu na kuchokonoa vitu vya kuleta hasira na visasi.
 
Kwa hiyo una admit kuwa kulikuwa na uonevu huko vyuma mpaka kutaka suluhu au unatakakutuambia nini!?
 
Umewahi kuwashauri hao machizi waliokimbia na nguo?
 
Kiukweli huyu MDUDE ameji aibisha sanaa, yaan mama kamuonea HURUMA ila li jamaa lilivyo JINGA halina hata shukrani ...kheri arejeshwe tu tena gerezani MPUUZI sanaaa yule
 
Kauli ya mdude kama imeichafua kiasi hicho chadema ,,,, je kauli za akina Kibajaji? Akina Kessy? Akina Goodluck? Si nizaidi sana hao maana huko ndo kuna mrundikano wa watu wa ajabu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Ila maccm yanaogopa kusimama nayo kwenye uchaguzi huru na wa haki kwa sababu wanaijua hatima yao hivyo wameona mtutu wa bunduki ndio kipenzi chao cha kuwavusha dhidi ya Chadema.

Chadema bado sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…