Mimi nawalumu sana BAVICHA kuhusiana na Mdude Nyagali. Katoka jela badala wamfanyie vipimo kamilifu vya kiafya (ikiwezekana hata nje ya nchi) na kumtafutia mwanasaikolojia ili akae sawa kiakili na kimwili na apumzike walau miezi miwili/ mitatu hivi ili apate utulivu. Wao mbio wametoka nae Mbeya kuja naye Dar kwenye kongamano walichokumbuka ni kumnunulia nguo na viatu. Kwa hili hata wakina Mbowe wanapaswa kulaumiwa walipaswa kuwaelekeza BAVICHA nini cha kufanya kuhusiana na Mdude. Kwa watu makini waliomwona Mdude akihutubia jana watakiri kuwa jamaa bado hajakaa sawasawa. Mdude ni mzungumzaji mzuri lakini hachugui maneno ya staha matokeo yake watu wenye busara wanamuona kama mhuni tu. Ushauri wa bure kwa viongozi wa Chadema wamuweke kijana chini wamfundishe namna nzuri ya kuchagua maneno wakati anahutubia kwani katiba mpya inahitaji kila mtanzania ashiriki kuanzia wazee, vijana n.k. Iwapo ataendelea kutuma lugha za kukwaza kama jana alivyotumia juu ya raisi wa nchi kwa kweli nina uhakika kuna baadhi ya kundi la watu mtawakosa kwenye harakati zenu za kutafuta katiba mpya kwani wote mtaonekana wahuni tu. Tunahitaji sana katiba lakini tunahitaji sana tufike kwenye hiyo katiba kwa amani na tukiwa wamoja kama tulivyo sasa bila kujali rangi, dini wala kabila zetu kwani siku zote sisi watanzania ni watu wa amani sana.
Mungu iabariki Afrika. Mungu ibariki Tanzania.