SI KWELI Meta yatangaza Mabadiliko ya Sera kwenye Mtandao wa WhatsApp kwa Mawasiliano Binafsi pamoja na Makundi Sogozi kuanzia Machi 22, 2024

SI KWELI Meta yatangaza Mabadiliko ya Sera kwenye Mtandao wa WhatsApp kwa Mawasiliano Binafsi pamoja na Makundi Sogozi kuanzia Machi 22, 2024

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Meta Fake.jpg
 
Tunachokijua
Zaidi ya watu bilioni 2 kutoka nchi zaidi ya 180 hutumia WhatsApp kufanya mawasiliano na marafiki au familia, wakati wowote na mahali popote.

Programu hii maarufu ya ujumbe wa papo hapo inayomilikiwa na kampuni ya Meta, ilianzishwa na Jan Koum na Brian Acton mnamo mwaka 2009, lakini baadaye ilinunuliwa na Facebook (ambayo sasa inaitwa Meta) mwaka 2014 kwa thamani kubwa ya dola bilioni 19.

Kwa sasa makao yake makuu yapo Meta Way, Menlo Park, California 94025, Marekani.

Kuzuka kwa Madai ya kubadilika kwa Sera za Matumizi ya WhatsApp
Kumekuwepo na ujumbe unaosambaa kwenye Makundi sogozi ukibainisha kuwa kampuni ya Meta imebadili Sera za Matumizi ya Mtandao wa WhatsApp.

Madai haya yameonekana pia kwenye Mtandao wa X Machi 21, 2024 ambapo taarifa zake zimehifadhiwa hapa na hapa.

Baadhi ya madai hayo ni kuanzishwa kwa utaratibu mpya wa kurekodi simu zote pamoja na nakala za rekodi za mawasiliano zitahifadhiwa. Aidha, WhatsApp, Facebook, Twitter, Instagram na mitandao mingine ya kijamii itafuatiliwa.

Ujumbe huo unaenda mbali zaidi kwa kubainisha kwa Polisi wataanza kufuatilia mawasiliano ya watu kupitia Mtandao huo kisha watatoa taarifa pamoja na kufungua kesi za uhalifu wa mtandaoni kwa kila mtu atakayechapisha ujumbe wenye utata.

Kwa upande wa makundi Sogozi, Sheria hii mpya inaonesha kuwa iwapo ujumbe utakuwa na alama moja ya tick itakuwa na maana Ujumbe husika umepelekwa.
  • Alama mbili za bluu kumaanisha Ujumbe umesomwa.
  • Alama tatu za bluu kumaanisha Serikali imechukua note ya ujumbe.
  • Alama mbili za bluu na moja nyekundu kumaanisha Serikali inaweza kuchukua hatua dhidi yako.
  • Moja ya bluu na mbili nyekundu kumaanisha Serikali inachunguza taarifa yako.
  • Alama tatu za nyekundu kumaanisha Serikali imeanza kuchukua hatua dhidi yako na utapata wito wa mahakama hivi karibuni.
Ukweli wa Madai haya upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia vyanzo vyake vya kuaminika umebaini kuwa suala hili halina ukweli.

Aidha, JamiiCheck imefahamishwa pia na Kampuni ya Meta kuwa taarifa hii ni Uzushi hivyo watu wanapaswa kuipuuza.
Mtu ana kaa na pumbu zake ana tunga li ujumbe lirefuu halafu ni upuuzi mtupu halafu ana kuja mpuuzi mmoja nae asie jua kuchuja taarifa ana lifowadi ilo liujumbe lina sambaa kila kona!!!
Kwamba serikali hii ya jamhuri ina uwezo wa kusoma jumbe zako za whatsapp🤣🤣
 

Attachments

  • Screenshot_20240323-200818_Chrome.jpg
    Screenshot_20240323-200818_Chrome.jpg
    365.2 KB · Views: 17
Habari ya Muda Huu,

Ndugu yangu naomba uniazime Macho na Muda wako kwaajili ya hili ninaloliandika Kuhusu Usalama Mitandaoni..

Mabadiliko ya Sheria Mpya za Mawasiliano kwenye WhatsApp na Simu za WhatsApp Audio na Video.
Ambazo Zinatarajia kuanza Kesho Ijumaa.


✍️ machafuko 🙏🇹🇿💪🔰💪
Sasa huu ujinga umeandika wewe au umefoward?

Ni bora huu ujinga ungebaki nao hukohuko kwenye magroup yenu ya WhatsApp kuliko kuleta huku kuthibitisha na wewe uwezo wako wa ubongo kuchanganuwa mambo ni mdogo Sana.
 
Hakuna mtu anayeweza kuhack Instagram wala whatsup unless umempa credentials zako mwenyewe iwe kwa hiyari, trick au kwa nguvu. Acha kudanganywa, by the way ahsante kwa taarifa
Hii taarifa ni uzushi, imeanza kutembea wiki 3 sasa
 
Nimeona ikienea kwenye Mitandao ya kijamii hiii habari JAMII CHECK tusaidieni

Kutakuwa na mabadiliko muhimu juu ya sheria mpya za mawasiliano kwenye mitandao ya kijamii WhatsApp ( simu za sauti na video) ambazo zitatekelezwa kuanzia kesho Tar 10-11-2024:-

01. mawasiliano yote yatarekodiwa
02. Nakala za record za mawasiliano zitahifadhiwa
03. WhatsApp, Facebook, Twitter X, Instagram,Ticktock, na mitandao mingine ya kijamii itafatiliwa.
04. Vifaa vyako vitakuwa vinaunganishwa kwenye mfumo wa wizara.
05. Jitahd usitume ujumbe wowote ambao ni mbaya ulio kinyume na maadili.
06. Wambie watoto wako, ndugu zako, jamaa, marafiki, na watu unaowafahamu kwamba wanapaswa kuwa makini kwenye mitandao ya kijamii
07. Usitume machapisho au video mbaya dhidi ya serikal kuhusu siasa au hal yoyote ya sasa.
08. Ni kosa kuandika au kutuma ujumbe mbaya kuhusu suala lolote la kisiasa , kidini kufanya hivyo kutakusababisha kukamatwa bila waranti.
09. Police watatoa taarifa kisha kufungua kesi za uhalifu mtandaoni, ambalo ni jambo serious.
10. Jihadhali usitume ujumbe mbaya na kila mtu azingatie hili na uchukue tahadhali.
11. Wanachama wote wa vikundi (Groups) wanapaswa kuwa makin na hili.

TAARIFA MUHIMU KUHUSU SHERIA MPYA ZA WhatsApp

1:- Alama moja ya blue☑️ ➡=ujumbe umepelekwa.
2:- Alama mbili za blue☑️☑️ =ujumbe umepokelewa.
3:- Alama mbili za blue☑️☑️ = ujumbe umesomwa.
4:- Alama tatu za blue☑️☑️☑️ = serikali imechukua note ya ujumbe.
5:- Alama mbili za blue☑️☑️ na moja nyekundu☑️ = serikali inaweza kuchukua hatua dhidi yako.
06:- Alama 1 ya blue☑️ na mbili nyekundu☑️☑️ = serikali inachunguza taarifa zako.
07:- Alama 3 nyekundu ☑️☑️☑️ = serikali imeanza kuchukua hatua dhidi yako na utapata wito wa mahakama hivi kalibuni.

KUWA NA RAIA MWEMA TUMIA MITANDAO KWA UANGALIFU NA MUNGU ATAKUWA PAMOJA NA WEWE BALIKIWA SANA ........
 
Back
Top Bottom