Mfalme ‘akiuawa’ huwa inachukua muda mrefu sana Taifa kupona

Nani ana hiyo moral authority ya kumtambulisha?
Nchi hii ina hazina ya watu wengi wenye busara kilichoharibu ni upepo wa hivi karibuni uliotaka kila anayeongea awe na maneno ya kusifu na kuabudu kama waimba tenzi za rohoni lakini hii haimaanisha kama hawapo wenye uwezo wa kukemea
 
Chifu kama kawaida you never let us down kwa madini kama haya.

Saluti sana.

Sasa tupo wapi na twaenda wapi? hilo ndo suali la kulitafutia jibu.

Matatizo makubwa yalianzia 1984 pale Dumila, tukurudi pale, twaenda kwa mzee Horace hadi tuangalie vita vya ndani kwa ndani kwa chama, kisha tuangalie Kombe,, yule profesa alietaka tuwe na katiba mpya, Mkapa mwenyewe mpaka kifo cha JPM na sasa cha latest kwa former minister.

Na Dumila ni kwamba baada ya vita vya Kagera Tanzania ilipaswa kuamka kiuchumi hivyo akatokea mtu ambae angetunyanyua lakini akaonekana ni tishio ambalo lingefuta kabisa historia ilowekwa na wengine, I'm sorry to say this lakini hii ndivyo ilivyokuwa kwamba haiwezekani Sokoine akainyanyua nchi kiuchumi kwa kupambana na wahujumu uchumi.

Matatizo ya uchumi naamini hata weye mkulu ulishuhudia na ulikula ugali wa yanga na kupanga foleni ya kuchukua chakula kwenye duka la kaya.

Na vilevile ikawa kwa JPM kwamba asingeweza kuinyanyua nchi kiuchumi kwa kipindi chake (ingawa WB na IMF walisema tupo uchumi wa kati) wakati alieharibu hapo kabla kwa miaka 10 yupo na aona.

It's a power struggle ambayo profesa Shivji ameiongelea katika kitabu chake cha Class Struggle in Tanzania 1976 ingawa imeingia hii ya power, kwamba mtu ataka power na fedha.

Tukirudi hapohapo wa Roma tuangalie watu hawa walinyanyuka vipi tena kuwa dola imara.

Ni kwamba baada ya kifo cha Severus Alexander, ilichukua miaka mingi hadi mwaka 270 walipompata kiongozi mpya aleitwa Aurelian. Huyu alitawala tokea mwaka 270 hadi 275, miaka mitano tu. Aurelian aliingia jeshini baada tu ya kifo cha Alexander akiwa na umri wa miaka 20 na kupanda vyeo kimyakmya hadi kufikai cheo cha juu.

Aurelian afanya mambo yafuatayo huku akikabiliwa na matishio ya kiusalama kutoka nje na pia vita vya ndani kwa ndani kwenye utawala wa Roma maana ulikuwa umevurugwa:

1. Alianza kujiimarisha yeye na aina ya utawala alotaka uwepo chini yake.
2. Alirudisha heshima ya nchi au taifa Roma Empire.
3. Alijenga uchumi kuwa imara.
4. Kuzima na kutuliza machafuko na sarakasi zote zilouwepo katika maeneo mbalimbali ya nchi.
5. Kurudisha hadhi na heshima ya vyombo vya ulinzi na usalama.
6. Aliongeza ukubwa wa mkate bila kupandisha bei, "very important point".
7. Aliweka sarafu moja kama mungu wa kumuabudu kwa wanajeshi, raia, na watu wote bila kuwashurutisha kuacha imani zao na hii ni point muhimu sana.

Sasa basi, kama taifa tapaswa tutambue wapi tutampata Aurelian wetu na naamini yupo.

Mwenye kazi ya kumtafuta Aurelian nafasi yake imekuwa "compromised".

Na hapo ndipo tatizo lilipo.

Nadhani ntaeleweka.
 
Wewe jamaa unajua mambo mengi sana,uekewa wako Samia hata umeweke darasani miaka 100 yule **** hawezi kukufikia🤣🤣🤣
 
Umemaliza kisomi sana mkuu
 
Membe ilikua decoy,hili wengine tulikipata kabla bulembo hajalisema kwenye ule mikutano wa CCM baada ya uchaguzi ambao palikua na msemo wa 'ng'ombe walokatwa mkia',hata mayalla aliandika humu siku nyingi kabla kwamba mteule 2015 ni magu
 
Dola la ottoman halikuunhanisha waislam chini ya dola moja?
 
Hapo kwa Kenya wana mzimu wao wa makamu wa rais tangu nchi kupata uhuru mpk rais aliyepo leo kila wakishika nchi lazima agombane na kaimu wake,,
Dhambi ya 2021 itaitafuna nchi,, ni mtafunano
2021 COVID-19, acheni kuzua mambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…