Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Umechanganya auntie achana na wa Millard ayo huyu mama bonge wa vitenge wa kontena 15 zilizokamatwa na tra
Aaaaah....Kumbe ndivyo Auntie?
Basi nikajua ndiyo huyo wa kwa Millard...
Halafu huyo wa Vitenge Kariakoo ni maarufu sana..
 
Uzalendo wenu ni wa kiwango Cha juu sana.

KATIBA mpya inaandikwa Kwa Wino wa Dhahabu.

Hatimaye wanaoonewa wameweza kushirikiana kupaza sauti kupinga uonevu katika mfumo wa Kodi kandamizi.

Mungu wa Mbinguni awabariki.

Amen.
Wale ni wafanya biashara na mambo zao. Msitake kubaka initiatives za wengine
 
Ni mara ya kwanza nashuhudia mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo, soko letu pendwa (baadhi). Vilevile mkutano kama huu wakitema cheche mbele ya Serikali. Hakika, kodi ni msingi wa maendeleo.
Roving Journalist shukran kwa thread na link
Na nadhani wamevumila wamechoka...
Wafanyabiashara wa Kariakoo ni watu waelewa sana..
Nilipewa Stori ya Issue za Vilemba Kariakoo nilichoka...
 
Swala la kodi ni la kitaifa. Inabidi lifundishwe mashuleni ili kuwajengea Watanzania uelewa wa umuhimu wa kulipa kodi na masuala yote ya kikodi yanavyotakiwa kufanyika.
Somo la kodi lingeanzia chini kabisa primary huko.
Kama hujasoma mambo ya uhasibu na uchumi mambo ya kodi yanakupita kushoto, matokeo yake ukiingia uraiani mambo unakuta vururu kabisa yaani tofauti na mategemeo yako.
 
Kariakoo ndiyo taswira ya uchumi wa sekta binafsi ya wafanyabiashara wazawa nchini. Changamoto,kero na matatizo wanayokutana nayo katika kuendesha biashara zao, ni kielelezo tosha cha vikwazo vya kibiashara kwa wajasiriamali wazawa nchini kutokana na utitiri wa tozo na kodi mbalimbali. Waziri mkuu, mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha, zinaathiri mpaka maisha ya mwananchi wa kawaida kwa kuwa ndiye mlaji wa mwisho. Natarajia hautashughulikia tu kero za wafanyabiashara wa kariakoo. Sekta ya wajasiriamali wazawa inahitaji mabadiliko makubwa ya kisera na kimfumo.
Aluta continua...
 
Wale ni wafanya biashara na mambo zao. Msitake kubaka initiatives za wengine
Wanalalamikia mfumo wa ukusanyaji Kodi unaokandamiza ukuaji wa biashara na Uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa Kwa ujumla.

Hivyo ni suala la kikatiba.
 
Hakuna chochote Magufuli alikuwa anawatuma kunyanganya mali za watu
 
Back
Top Bottom