Mfanyabiashara Maarufu wa Tanzanite, Erasto Msuya apigwa Risasi na kufariki papo hapo!

Mfanyabiashara Maarufu wa Tanzanite, Erasto Msuya apigwa Risasi na kufariki papo hapo!

Ndiyo huyo jamaa, nikweli amefariki kwa kupigwa risasi 8 kwa mujibu wa jamaa aliyeko karibu na eneo la tukio. Na inasemekana hawajachukua kitu chochote kwenye gari lake.
Hiyo ni nia kamili ya kuhakikisha hanusuriki! RIP
 
Afadhali hata wewe kidogo umempa heshima yake watoto wa Arusha wanamuita Bilionea!
 
Usijekuta niwale watoa kucha na kung'oa meno bila ganzi wako kikazi pande zahuko,Wamehisi hayuko upande wao!!Maana hawana dogo!Wanakutafuta taraatibu na hawaogopi maana ndio kazi yao!Eti wamekimbia na mali?Usijekuta nikupoteza lengo tu!Poleni wafiwa,Mungu nizaidi ya Mwanadamu na analipa hapahapa wala sio mpaka uende aliko.Kwakweli nilazima tuangalie pande zote huyu nimfanyabiashara wapili anauwawa maeneo yanayofanana nakwastaili inayofanana!


attachment.php

attachment.php
[/QUOTE]
 
hebu jipange vizuri utupe habari kamili.
tait ndio nini?
huyo mtu ana hadhi gani huko Arush hadi apewe hadhi JF jukwaa la siasa?
 
Breaking newssssss

Watu wa Arusha kuna taita wa madini kapigwa risasi jioni hii, taita huyo akiitwa Msuya, kapigwa na wabaya wake baada ya kuingia mtego wa kumwita boma area wafanye biashara akaenda mbio sehemu hiyo akitoka KIA. Nyie wenzetu wa Arusha tuelesheni zaidi.
Hii sio breaking news. Jizoeze tabia ya kupitia post za wenzio kabla hujaja na ya kwako. Habari ipo tangu mida ya lunch hii


Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Lema Polisi?Tafakari unapotumwa!Sio iwe umeingiza siku!
Hao wengine mnawalalamikia kila siku humu ni polisi?

Lema pamoja na wabunge wa Chadema wanatakiwa wajiudhulu haiwezekani kila siku matukio ya kuuliwa raia yanaongezeka.
 
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ampumzishe kwa Amani. Amina!

Hayo ndiyo maneno mnayotumia kumtania Mungu. Kumbuka Mungu hadhihakiwi kwa maana kila apandacho mtu ndicho atakachovuna!!! Mwanadamu anapokufa bila kutubu dhambi zake bila kujali cheo chake au dini yake, halali yake ni jehanamu kwenye moto wa milele. Huko hakuna kupumzika kwa amani bali ni kilio na kusaga meno. Salama ya kila mwanadamu ni kukimbilia kwa Yesu mapema kabla hajafa!
 
kwanza umechelewa kuripoti, pili unaripoti kishabiki sana, tatu inaonekana una njaa kali sana... vuta pumzi soma JF hiyo habari ipo kwa masaa kadhaa sasa

RIP rafiki Erasto
 
sio tetesi tena, ni kweli Erasto hatunaye, sitaki hata kuamini kabisa kabisa, walikuwa na ugomvi mkali na "chusa" natamani kutiririka ila basi tu, duh duh
Funguka shemeji yangu maana JF napenda kwa kupata vitu mang'anyu
 
Mabilionea wa kanda ya kaskazini wanapukutika daily aisee. Nakumbuka hata Bishanga alipokuja hapa Arusha alifikia pale kwenye lodge yake SG Resort. Pia ndiye mweny Mezzaluna Hotel.

Kuna tatizo gani Arusha? Ni watu kutafuta hela bila utaratibu au kudharau uwezo wa watu wengine na kuwaonea ili mradi hela ipatikane? Hizi si habariu njema sana...
 
Hao wengine mnawalalamikia kila siku humu ni polisi?

Lema pamoja na wabunge wa Chadema wanatakiwa wajiudhulu haiwezekani kila siku matukio ya kuuliwa raia yanaongezeka.

Na IGP Mwema afanye nini? Kwani blue guard au green guard ndio wanaolinda raia? Lets be objective! Issuekama hizi si za kisiasa...ni za kijamii na tuliangalie tatizo kwa mapana zaidi kuliko siasa uchwara tunazopigana nazo siku hizi maana wengine sio wana siasa.
 
Hao wengine mnawalalamikia kila siku humu ni polisi?

Lema pamoja na wabunge wa Chadema wanatakiwa wajiudhulu haiwezekani kila siku matukio ya kuuliwa raia yanaongezeka.

Huyo bwana keshaanza kuleta utani kwenye iSsue ya maana,wenzako wana majonzi
 
Back
Top Bottom