Mfanyabiashara Maarufu wa Tanzanite, Erasto Msuya apigwa Risasi na kufariki papo hapo!

Mfanyabiashara Maarufu wa Tanzanite, Erasto Msuya apigwa Risasi na kufariki papo hapo!

Akili ndogo kumiliki pesa nyingi nalo ni tatizo jamani.
 
Duh, kuna picha moja ipo hapa jamvini iangalie na ufananishe na unachokisema!

Mfanyabiashara mkubwa wa madini na hotel jijini Arusha anayefahamika kwa jina la Erasto Msuya amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi. Hali hiyo imetokea eneo la KIA wilayani Hai.
Habari zaidi zitawajia.
 
sio tetesi tena, ni kweli Erasto hatunaye, sitaki hata kuamini kabisa kabisa, walikuwa na ugomvi mkali na "chusa" natamani kutiririka ila basi tu, duh duh
ha haaa, umbeya hauna posho... nitiririkie mimi kwa pm, lol!
poleni sana rafiki kwa huo mziba, maana naona umeguswa haswaaaa, pole sana.
RIP
 
kuwakamata wahusika ni kazi rahisi tu kwa hili
watatrace mawasiliano yake katika mitandao ya simu na hata sauti wataisikia aliempigia
watakagua pia maganda ya risasi na kujua nani mhusika
poleni familia.
 
Ndio yeye, alikuwa anatoka Mererani alipofika eneo liitwalo Majengo ndipo akavamiwa na kupigwa risasi nane akafia palepale. Alikuwa ametoka kununua mzigo mkubwa sana (madini) wamechukua. Jeshi la polisi mikoa ya Kilimanjaro na Arusha linawasaka watuhumiwa

Dah! Nilikuwa sijaelewa bado...... Sasa nimekuelewa!

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi
AMEN!
 
Sisi wazee wa kudadavua mambo ebu tujuze kidogo katika maisha yake alikuwa mfuasi wa chama gani cha kisiasa ikizingatiwa ukiwa na vijifedha basi moja kwa moja unakuwa mfadhiri wa chama hicho. Zaidi ya yote nawapa pole wafiwa R.I.P Erasto Msuya.

unataka kumaanisha magamba wapo nyuma ya hili?
 
unataka kumaanisha magamba wapo nyuma ya hili?
Kama alikuwa upande ule lolote linawezekana kwani hawa jamaa kwa sasa kumpoteza mfuasi mmoja wa kule ni sawa na wale wanaosema kujilipua na kuua muizlael 1 unaenda peponi moja kwa moja.
 
Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama vile kivuli, wala hakai kamwe. AYUBU 14: 1 - 2

kabisa tuishi kwa utayari na kwa kumtumaini muumba wetu tuyafuate na kuyatii mafundisho.
 
Well, mimi nasikitikia familia yake. Hata hivyo niseme tu kwamba pamoja na kwamba sijui chanzo cha kifo tunatakiwa tujihadhari na dhuluma na tena wake za watu. Haya mambo mawili yamekuwa ni chanzo cha vifo vingi vyenye utata. Tunapaswa kufahamu kuwa kama ni dhuluma hata ukiua hutapata ulichokuwa unadai. Hata kama ni habari za wanawake unaweza kuua wengi. Dawa ni kuheshimiana na kuwa na mazungumzo. God help us. Amen!

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Inasikitisha sana!kwa nini Binadamu tumekuwa na roho za kinyama?ila wajue ukiua kwa panga nawe utauawa kwa panga.mungu ailaze mahala pema peponi.Amen.
 
Hao wengine mnawalalamikia kila siku humu ni polisi?

Lema pamoja na wabunge wa Chadema wanatakiwa wajiudhulu haiwezekani kila siku matukio ya kuuliwa raia yanaongezeka.

Nyani haoni kundule,leo tu DSM kuna mwalimu wa UDSM kapigwa risasi na kufa,unasemaje huko nako?
 
Forbes wanamjua? Kina Slim wataitwa nani sasa? Mfano mi nina nyumba yangu nimeijenga kwa Mil.100 utaniita Millionair?

Mkuu huyo ana hela za kawaida tu,,,inaelekea hata kaka yangu Hussein Gonga siku akifa nae mtamuita Billionair maana nae ana ofisi zake hapa Tanzania HUGO zinadeal na Tiles na pia maghorofa yake hapo Arusha karibia na stand anayajenga,,ni sawa ana hela lakini namuona ya kawaida tu.

Basi Tanzania kama ndo hivyo tuna maBillionair kuliko hata Saudia na Marekani.

sidhani kama inamjua erasto lkn pia usipende kuleta ubishi usio na maana ktk Tsh tule alikuwa ni billionea na ktk united states dollars ni millionea
 
Tajiri maarufu mirerani na arusha maarufu kwa jina la erasto ameuliwa leo alasiri na watu wanaodhaniwa ni majambazi na kutokomea kusikojulikana.. Tukio hilo limetokea maeneo ya kia njia ya kwenda mirerani ambapo bw erasto akiwa kwenye gari lake aina ya ranger rover ndogo new model alipigwa risasi na majambazi hao na kufa hapo hapo.. Police wanaendelea na uchunguzi zaidi..
 
Ndiyo huyo jamaa, nikweli amefariki kwa kupigwa risasi 8 kwa mujibu wa jamaa aliyeko karibu na eneo la tukio. Na inasemekana hawajachukua kitu chochote kwenye gari lake.
Amepigwa risasi nane?au nimeelewa vibaya?
 
Back
Top Bottom