Mfanyabiashara Maarufu wa Tanzanite, Erasto Msuya apigwa Risasi na kufariki papo hapo!

Mfanyabiashara Maarufu wa Tanzanite, Erasto Msuya apigwa Risasi na kufariki papo hapo!

Huyu jamaa alikuwa tajiri sana kwwenye jiji la Arusha alikuwa wa pili kama sio wa tatu alikuwa na hotel kubwa nyuma ya triple A alikuwa na vogue evogue. Alikuwa na ndege binafsi

Arusha kwa promo mpo juu hawa mabilionea wenu hawa mnawapaisha sana.
 
Tumechoka na hawa mabilionea wa Arush
a. Mtu anamiliki guest house, bajaj, bodaboda, na Vitz utasikia naye ni bilionea. Aaaaaaagh it sucks
 
.............., nikikumbuka ile ndege ya bilionea bob, lol! kweli Arusha mji wa mabilionea na hasa ukishaweza kuwa na uwezo wa kugawa ofa ya bia na nyama choma

Arusha kamji kadogo sana mtu akiwa na pesa za ofa za bia basi mji mzima anajulikana fikiria tajiri Wanyama wa k.koo angefia Arusha
 
Imebaki historia sasa. Soon atafukiwa kwenye mchanga kamw walala hoi wengine wanavyofukiwa
 
sio arusha tu, hiyo ni kila mahali ipo, pesa mwanaharamu, lakini kwa hili sio mke wa mtu wala nini, watu wa mererani kwa wanawake wanajulikana hatukatai lakini kwa Erasto hapana, sio kwamba na yeye alikuwa hana wanawake alikuwa nao lakini kwa hili la leo picha ni huyo mnyakyusa!

Huyo CHUSA kumbe ni MYAKYUSA ndio mnamshuku kuwa ndio kanfanyizia huyo marehemu?
 
TRA wangehamishia nguvu za ukusanyaji wa kodi Arusha nina uhakika hela za umeme vijijini zingepatikana bila kutoza walalahoi wa mbamba-bay kodi ya simkad
cc. EMT
Nchi hii ina uwezekano wa kukusanya mapato mengi kama serikali itaamua tatizo ni pale wanasiasa wanapounda urafiki na wafanyabiashara wakubwa kwa kuwa nao karibu pindi wanapotaka michango mbalimbali ya maendeleo na mingine ya kawaida ambayo kimsingi kwa serikali makini haikutakiwa kuwafuata raia kuomba support. Kwa kuwa hawa jamaa nao wanataka sifa na kuonekana pia fursa nzuri kwao ya kuwa karibu na wananchi wanajitahidi kwa hali na mali kutoa ili mwisho wa siku wakiwa na shida tena zile za kuvunja kanuni wanakuwa wanafuata hawa viongozi wetu na kupindisha kidogo, alikuwa alipe milion 600 atalipa milioni 90 na kuwapa tip kidogo hao wadau wake.

Naikumbuka TAKUKURU enzi hizo ikiitwa taasisi ya kuzuia rushwa chini ya Augustino Buruda ilikuwa ukipewa zawadi lazima wakushughulikie kwa kupokea rushwa lakini siku hizi tunaambiwa takrima. Hata hawa wanaochangisha harambee kutoka kwa marafiki zao ipo siku wakichukua madaraka makubwa kama binadamu inakuwa ngumu kuwatosa moja kwa moja hawa jamaa anaowaita marafiki zake ikiwa imetokea wamekiuka baadhi taratibu
 
Utakuta bilionea mwwnyewe kodi alikuwa analipa mil.3
 
Tumechoka na hawa mabilionea wa Arush
a. Mtu anamiliki guest house, bajaj, bodaboda, na Vitz utasikia naye ni bilionea. Aaaaaaagh it sucks

hata mimi hapa ar. wanaamini ni bilionea ingawaje najijua mali zangu zote hazifiki bilion...ar noma vogue cruza na hotel kidogo tayari unaitwa billionea.....j
 
Arusha kwa promo mpo juu hawa mabilionea wenu hawa mnawapaisha sana.

Heri yetu sie jiji letu la Mwanza linaendeshwa na wananchi wote kwa ujumla ambapo mgawanyo wa rasilimali upo kulingana na juhudi zako na ndio maana hata mwananchi wa chini nae anajiingizia kipato kulingana na urefu wa kamba yake, tatizo la Arusha kuna watu wachache wameubeba mji kutokana na shughuli zao za kiuchumi huku wengine wakiwa wana-milki mali kiana tu na kuwafukuzia kwa mbali ila ninachowapenda wanajua kuzitendea haki ela kwa kuzifanyia vitu vya maana hata ukimkuta kwake kweli unasema huyu ni tajiri na ndio maana unaona hizo promo mkuu
 
Huyu jamaa alikuwa tajiri sana kwwenye jiji la Arusha alikuwa wa pili kama sio wa tatu alikuwa na hotel kubwa nyuma ya triple A alikuwa na vogue evogue. Alikuwa na ndege binafsi

Mods nakuombeeni toeni huu uchafu ni kujaza thread tu na server kuwa busy, mtu m1 anaanzishiwa uzi kila sehem kwa vyanzo vya tetesi.
 
Tumezoea Arusha ukimiliki gesti haus ni bilionea

ni kweli kabisa ubilionea unategemeana na mahali husika,mi mwenyewe kijijini kwetu najulikana kwa jina la bilionea namiliki kacorrola nilikanunua 7m,nina pikipiki 2 bodaboda,alafu nikifika pale kijijini najikakamua nanua kama kreti 10 za soda(laki130) kwa baadhi ya wanakijiji hasa nyakati za sikukuu,ninaeshimika balaa pale kijijini adi kuitwa bilionea.

kwa iyo ata arusha nao wana vigezo vyao vya kumuita mtu bilionea,dar nao wana vigezo vyao na pia kuna vigezo vya kimataifa.
 
Huyu jamaa alikuwa tajiri sana kwwenye jiji la Arusha alikuwa wa pili kama sio wa tatu alikuwa na hotel kubwa nyuma ya triple A alikuwa na vogue evogue. Alikuwa na ndege binafsi

Kwani bilionea wa kwanza Arusha ni nani? Bob Sambeke au yule genius wakili msomi?
 
Pika hata vitumbua, ukifikisha pesa taslim 2bn wewe ni bilionea.
Haijalishi umepataje pesa hizo, upotoshaji uko wapi hapa?! Tatizo mnakuja na hoja nyepesi, si kila Bil ni lazima amfikie Gates kwa mabilion, hata vidole havilingani lakini vyote ni vidole.
Ukimiliki bilioni zaidi ya moja wewe ni Bilionea, acheni ligi na wivu wakimaendeJANA!!

Kwa hiyo wazimbabwe woote ni mabilionea?
 
Back
Top Bottom