Mfanyabiashara Maarufu wa Tanzanite, Erasto Msuya apigwa Risasi na kufariki papo hapo!

Mfanyabiashara Maarufu wa Tanzanite, Erasto Msuya apigwa Risasi na kufariki papo hapo!

Hivi ule uzi wa mabilionea wa Arusha v. Dar ulienda wapi?

Manake Arusha kila anayekufa/kuuawa ni mfanyabiashara "maarufu" au "bilionea/milionea". Nadhani ni vizuri tukawa na version yetu ya Forbes ikilenga zaidi Arusha.
 
huyu jamaa alikuwa tajiri sana kwwenye jiji la arusha alikuwa wa pili kama sio wa tatu alikuwa na hotel kubwa nyuma ya triple a alikuwa na vogue evogue. Alikuwa na ndege binafsi

picha?
 
labda awe amekudhulumu wewe, kwa tunaomjua vizuri hana hiyo tabia kabisaaaa atakuwa ameianza kwako.

thank you... kuna watu wana kaugonjwa ka kuropoka full time, afadhali umempa z uso akakojoe alale
 
Uwekezaji gani mbona hutaji? Compressor, Generator, Baruti au? Maana hata hao wanaApollo hawalipwi mishahara maana ni vibarua tu na hawalipi kodi.

Billionair gani utamuhesabia ambae halipi kodi? Zinakutosha kweli mkuu au unazo za kuvukia barabara?

Huwezi kumfananisha na Bakhresa hata robo ambaye ana wafanyakazi wanakatwa kodi kama yeye na ujue ana mchango wa uchumi katika taifa lako tofauti na Marehem ambaye ana vibarua ambao ni wanajaza choo nyumbani mwao.

naona hauna elimu ya madini, kwaiyo tafuta wa kujibishana nae,mwanaume gani unakua unatoa ufafanuzi wa vitu usivyovijua? hakuna mtu atakayekusifia kwa kujaribu kuukwepa ukweli.mimi nikuache uendelee kulumbana.
 
angalia slide show hapa chini, evaluate roughly atakuwa na vitu vya jumla ya Tsh ngapi.
Nadhani kidogo anaweza akavuka 1bn, lakini sijui alikua na madeni au hana, hivyo siwezi kusema yeye ni billionaire au la.

- Home
 
Kila mfanya biashara arusha bilionea!halafu hawajui kuutumia ubilionea wao!cha ajabu unaitwaje na mtu anakuambia mkutane porini hivyo nawe unaenda?huyu alipaswa awe na ofisi na biashara ifanyike ofisini,vinginevyo angeenda polisi kuomba escort kwa safari yake hiyo.Unakuwa na vipesa mbuzi halafu unakuwa mtumwa haina maana bora uwe lofa
 
Matajiri wanaosapoti mabadiliko mbona kama vile ndo wanasakamwa? Hii vipi jamani?
 
naona hauna elimu ya madini, kwaiyo tafuta wa kujibishana nae,mwanaume gani unakua unatoa ufafanuzi wa vitu usivyovijua? hakuna mtu atakayekusifia kwa kujaribu kuukwepa ukweli.mimi nikuache uendelee kulumbana.

We ndo boya aisee,,hembu nipe elimu yako ya uwekezaji wa mashimo local ukiondoa vitu kama Baruti, Compressor, Generator au vibarua kutolipwa mishahara ambayo sio kufananisha mgodi kama ya AFGEM/TANZANITE ONE. Nifahamishe mkuu.
 
Kila mfanya biashara arusha bilionea!halafu hawajui kuutumia ubilionea wao!cha ajabu unaitwaje na mtu anakuambia mkutane porini hivyo nawe unaenda?huyu alipaswa awe na ofisi na biashara ifanyike ofisini,vinginevyo angeenda polisi kuomba escort kwa safari yake hiyo.Unakuwa na vipesa mbuzi halafu unakuwa mtumwa haina maana bora uwe lofa

Bilionea hana hata vi bodyguard mbuzi? Mabilionea wa Arusha vichekesho sana aisee.
 
stata mzuka mkuu naomba hawa watoto wa Arusha watupe orodha ya mabilionea wote wa Arusha tuwe nayo ili ikitokea kafa tusianze kuulizana ulizana maswali.

Bilionea anaenda kufanya biashara porini,hana mlinzi yupo yupo tu labda ni kauza Ngada kwasababu ndo zao kufanya biashara porini.

Alafu nilivyowasoma vijana wengi wa Arusha hapa ukiwa na Vogue we ni bilionea ukiwapa tips sijui wewe bilionea!!

Bilionea hata katika orodha ya walipa kodi Arusha hayupo?!Narudia tena watoto wa Arusha tembeeni muone watu wenye pesa zao.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hao ni wakuja tu hata hawanipi shida kamji kenyewe Town ni kuanzia kama Magomeni na M/Mmoja utaacha kufahamika kweli? Ndio maana Billionair wanawajua hadi watoto wao wadogo ambao wako shule ya msingi, Billionair anakufa hana hata athari katika uchumi wa taifa zaidi ni familia yake na wapambe wa kununuliwa nyama choma na bia.

Wameshawataja wenyewe maBillionair wao kama huyo Benson,,yaani hadi kicheko kwakweli mtu anamiliki Duka la Electronics nae Billionair.

Nimekaa Arusha Njiro maeneo ya Tanesco kwa miaka 16 nawajua vizuri sana. Kujisifu kwiiingi kumbe ushuzi mtupu.
 
Last edited by a moderator:
Poleni familia ya Erasto Msuya. Hii habari inasikitisha sana Mungu awape furaja kipindi hiki kigumu cha Msiba.
 
chama ya wabongo ni magumu,
siamini kama wauwaji hawapo humu jf,
Mamndenyi
Mambo yanasikitisha sana yote ni kumuachia Mungu; hatujui nini kimetokea; maisha siku zote ni kujifunza nadhani tukio hili ni moja ya mafunzo wanaJF wanatakiwa kujifundisha namna ya kuishi na jamii inayowazunguka!
 
Last edited by a moderator:
chama ya wabongo ni magumu,
siamini kama wauwaji hawapo humu jf,
mamaNdenyi
Maisha ni safari ndefu inasikitisha sana kuona binadamu amekatishwa safari yake ghafla namna hii; ni kumuachia Mungu tu ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho. Natumai wanaJF wamelichukulia tukio kama elimu ya maisha jamii inayakuzunguka inaweza ikawa tamu kama embe dodo na inaweza kugeuka ikawa chungu kama shubiri!
 
Last edited by a moderator:
Kifo cha Erasto na mjadala kuhusu utajiri wake ni fursa nyingine kwa WTZ kujifunza zaidi juu ya elimu dunia...binafsi imenishangaza sana kujionea dhana ya ubilionea/umilionea inavyowasumbua wengi hususani walio nje ya jiji la Arusha kutokana na yafuatayo: kwamba ubilionea
@ unahusishwa na ukubwa wa mji
@ ni kuwa organized (ofisi,wapambe etc)
@ ni kwa personality fulani the likes of Bakhresa Dakote nk
@ Upatikana ktk mji mkubwa mfano Dar na si kwingineko
@ ni lazima utokane na structured business...na si individual (sole)
@ ni lazima kufahamika na TRA kama mlipa kodi mkubwa
@ ni sharti uorodheshwe ktk jarida la Forbes na au kutambulika duniani kwa ujumla
@ unatokana sarafu maarufu duniani mfano $,£,€ nk.
@ hauwezekani ktk sarafu mfano ya TZS na Zim Dola.
@ unatokana tu na kufanya aina fulani ya biashara na si kila biashara
Nk

Naamini hapo juu ni baadhi ya dhana potofu juu ya ubilione. Ukweli ni kwamba michango inayoendelea hapa inawaweka wengi ktk daraja la chini kidogo linapokuja swala la "general knowledge"..wengi wana vyeti "vizuri" lakini inapokuja kwenye tafsiri ktk maisha halisi kwa kweli kuna tatizo. Binafsi napenda kuamini kuwa wengi wa wanaochangia hapa jukwaani ni watu informed au wanapashwa kuwa hivyo inapokuja maswala madogo kama who is a millionaire/billionaire?
 
Back
Top Bottom