Mfumo wa Jeshi la Polisi ubadilishwe, Unakandamiza na kunyanyasa Wananchi hasa wa daraja la chini

Huo ujinga sasa hivi hawawezi kunifanyia kmmae zao. Nitaua mmoja na mimi wataniua..
Hahaha,
Mkuu, tema mate chini.
Hujaingia kwenye 18 zao tu.
Watakufanyia vizuri tu na utakuwa mpole kama siyo wewe vile.
Hata majambazi sugu walioshindikana hukamuliwa kilaini sana wakidakwa na hao jamaa
 
Ingawa askari wa chini ana hiyo division iv lakini Waziri ana degree, IGP na wakubwa wengine ndani ya jeshi hilo pia wana elimu nzuri tu iweje waruhusu upuuzi kwenye jeshi hilo?
Je hawauoni?
 
Mwaka 2021 nikiwa matembezini mchana pale Dodoma mtaa wa makulu kuelekea yalipo makao makuu ya TANESCO na REA nilisikia sauti ya mtu akiniita. Kuangaza vizuri walikuwa ni askari POLISI wawili wakiwa eneo lililojificha kidogo chini ya mti. Walikuwa na pikipiki nyeusi aina ya SINORAY. Nilipoona ni POLISI nikajua ni amani labda wanataka msaada wa jambo, nikaenda. Nilipofika nikashangaa wanaanza kuniuliza maswali mengi kuwa nimetoka wap? Naenda wap? Kufanya nini? nk. Nilijibu kwa kujiamin kwani sikuwa na shak. Ghafla mmoja akafungua kibegi alichokua nacho kikiwa na mafungu ya majani mabichi na kuniuliza huu mzigo wa nani? Nilipatwa na hofu kuu kwani sikujua chochote. Katika kujitetea na hasira nikajikuta NASHAMBULIWA kwa makofi na kupigwa ngwara. Kiukweli nilipata naumivu makali sana. Wakanifunga pingu kisha wakaanza kunisachi. Baada ya hapo walinichukua na kwenda kunidampo kituo cha polisi KISASA kisha nikaachiwa. Wote nawafahamu kwa sura na huwa nawaona sana barabarani. Mmoja anaitwa FRED. Nimemuachia MUNGU!
 
Unachiongea una uhakika nacho ? Mimi nimewahi kuja kukamatwa na mpelelezi kwa kuhisi kufananishwa ,kusaini document km shahidi wakati sijui chochote ,wakanionyesha picha ya jsmbazi la Arusha hiko kuko kuwa nilimdhamini wakati sijui chochote wala simfahamu mtu ,baadae akatoka nje akawa anaongea na cm ,akasema huyu siye namsikia ,polisi mwenyeji akamwambia mtishie tupate hela aisee nasikia yote ,akaingia na kunambia sasa itabidi twende wote arusha ,au toa 1M aisee nilisikitika sana ikabidi nitoe ili niachiwe hakuna watu wenye roho mbaya na tamaa ya pesa km polisi halafu angalia maisha yao duni sana
 
Pole sana mkuu. Wewe uliinunua haki yako. Kwani ukikomaa nao na hadi wakakuweka mahabusu unaona shida gani?? Unatoaje 1m kizembe hivo?
 
U

Unaishi nchi gani definitely sio Tanzania
Naishi Tanzania hii hii na vituko vya polisi navifahamu na yamewahi kunikuta. Mm sio mgeni hapa. I have a lot of experience vide these thugs.
 
Siwatetei hao jamaa. Ninachosema hapo ni kwamba zipo taratibu. Kama taratibu zimekiukwa ndo shida inaanzia hapo. Hoja ya wafanyabiashara kuuawa
au dereva wa tax n.k. ukifatilia kwa makini utagundua kuna SIRI fulani haiwekwi wazi. Polisi sio vichaa watoke na silaha ambayo hutolewa kwa utaratibu halafu kwenda kum'ua mtu fulani specific kati ya watu wengine wooote wanaopishana nao njiani. Never. Hiyo kubali usikubali ni syndicate.
 
Kituoni uliambiwa una kosa gani ?
Je ulitokaje kituoni kwa kudhaminiwa au kuruhusiwa bila masharti yoyote ?

Ni kweli hukuwa unajua lolote kuhusu eneo hilo ? Je wahusika wamewahi kukuomba radhi kwa yaliyotokea ?
Pole Sana
 
Kwanini usimwambie mtu kosa lake ni nini zaidi ya kuendekeza ubabe wa kijinga?? Ulaya hakuna upuuzi kama huu..
Nani alikudanganya eti Ulaya hakuna mambo hayo? Wewe unaiita kazi ya wenzio ni Upuuzi. Utaratibu unamtaka mtuhumiwa aambiwe Tuhuma zinazomkabili akiwa Kituoni. Mtuhumiwa akiwa kituoni Anaweza kuzikanusha (Sio kukataa) tuhma dhidi yake na akatoa maelezo(Statement) ya hali anavyoijua kuhusu tuhuma hizo. Hayo maelezo anaweza bado kuja kuyakataa pale Mahkamani kwa sababu katika kuandika Maelezo kuna kile kinaitwa "maswali ya kipolisi" i.e. maswali ya kukerehesha na kulazimisha kitu fulani kiandikwe halafu baadaye anakutaka usaini kana kwamba ni maelezo Huru uliyotoa ww..
Hakuna ubabe endapo utazingatia Sheria. Unapokataa kwenda kituoni ndipo hapo shida huanzia.
 
Kituoni uliambiwa una kosa gani ?
Je ulitokaje kituoni kwa kudhaminiwa au kuruhusiwa bila masharti yoyote ?

Ni kweli hukuwa unajua lolote kuhusu eneo hilo ? Je wahusika wamewahi kukuomba radhi kwa yaliyotokea ?
Pole Sana
Pole sana mkuu. Mimi niliwahi kujikuta mahabusu pale Iringa mjini (1997) kwa kisa cha kubeba redio yangu niliyoitoa kwa fundi. Nilibeba redio hiyo baada ya fundi kukamilisha matengenezo na niliibeba bila wasiwasi katika mfuko wa nguo mithili ya hand bag.
Nilitembea nayo hadi nikaingia eneo la kuuzia mitumba jirani na hapo stend ya mabasi. Akatokea kijana wa makamo mmoja akanisalimu na kuanza kuulizia kutaka kuiona redio yangu. nilimashangaa kwamba redio zimejaa madukani kwa nini asiende kuziona huko? Kijana alijitambulisha kwangu kwamba yy ni Polisi na hivyo anahitaji kuikagua redio yangu. Nilimkubalia ila kwa masharti kwamba Ukaguzi ukafanyikie Kituoni. Tuliongozana hadi Kituoni na hapo nilimruhusu aikague redio. Baada ya ukaguzi, kama utani hivi, akanikabidhi kwa askari waliokuwa hapo kaunta kwamba niandikishe maelezo kuhusu redio hiyo ni mali ya nani na nimeipataje.
Muda ulikuwa umeenda (jioni sana) na hivyo niliwekwa mahabusu ili maelezo yachukuliwe kesho yake. Nililala mahabusu kimasihara hadi asubuhi. Asubuhi nilijidhamini mm mwenyewe ili kupata nafasi kwenda Ofisini kutoa Taarifa ya yaliyonikuta. Sikupigwa wala siku sukumwa kuingia humo ndani - chumba cha mahabusu. Asubuhi katika maelezo niliambiwa tuhuma dhidi yangu ni kupatikana na redio inayodhaniwa ni ya wizi.
Ila kwa kweli Maswali ya Polisi yalinifanya nifike mahali Hasira zikapanda.
 
Pole Sana ,tena Sana kadhia Kama hizo zimewakuta wengi hasa ikiwa vijana wanahitaji hela ya maji .

Ninachojua na kuamini ulitoka mahabusu na kuruhusiwa bila masharti wala hela yoyote ni kipindi hiko bado uadilifu kazini ulikuwa juu Sana ,tofauti na Leo vijana wamevamia kada ni hapo wao kila kilichopo mbele yao wanaona ni noti ya elfu kumi .

Pole sana
 
Jaribuni tena kunidhalilisha kama mlivyofanya Tunduma mwaka 2015 muone nitakachomfanya mmoja wenu. Wapuuzi wakubwa nyie. Kazi kukalia ubabe wa kijinga tu na vitisho kwa raia pumbavu zenu ili wawape hela muende kunywea beers jioni.

Nendeni Ulaya na Marekani mkajifunze Modern Policing..
 
Upo sahihi kabisa. Mfumo wa sasa siyo service oriented Bali ni wa kikoloni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…