Mfumo wa Jeshi la Polisi ubadilishwe, Unakandamiza na kunyanyasa Wananchi hasa wa daraja la chini

Polisi Mahakamani Uhamiaji kote huko ni RUSHWA tupu RUSHWA ni ADUI wa HAKI.
 
Ni kweli Polisi wanatuhumiwa sana kunyanyasa ila kukamata mtu na kumshikilia bila kosa kwa muda mrefu huku wakimpiga huwa ni ngumu mno kutokea... na mara nyingi ikitokea utakuta mtu alikutwa eneo ambalo sio sahihi... kwa mfano maandamano au polisi wameenda kukamata wahalifu maeneo hayo wakakukuta labda unapita zako.
 
Sasa mkuu ,Mimi pale juu si nimesema pole kwa yote na pia nimekuadi wakikupiga tena lazima na Mimi niingilie tuwapige ?
Sasa ukianza kumtukana tena afande wangu hapa nitahama upande wako nihamie kwa afande ili tukudake tukung'ute tena
 
Sasa mkuu ,Mimi pale juu si nimesema pole kwa yote na pia nimekuadi wakikupiga tena lazima na Mimi niingilie tuwapige ?
Sasa ukianza kumtukana tena afande wangu hapa nitahama upande wako nihamie kwa afande ili tukudake tukung'ute tena
Hebu jaribu uone. Just give it a try..
 
Pole mkuu. Mimi sio "njagu" bali ni raia wa kawaida sana. Habari za modern Policing zipo nchi nyingi za Ulaya na ipo kwamba ukifanya kosa ambalo ni la faini papo kwa hapo unalipa na kupewa receipt ya EFD mnamalizana. Hakuna cha Kituoni. Hapa bongo ni maneno meeeeengi, ubishi tele na rushwa vimetamalaki.
 
Welcome to my ignore list..
 
Kaka umeniponza aisee ,ona rafiki yangu nimetania kidogo akahisi nakutetea wewe ambaye ni Askari kwa mawazo yake ,Sasa kaniweka ignore list ,dah .
Naumia nitampata wapi rafiki Kama huyu hapa duniani 😂
 
Bora ukutane na jambaz sugu litachukua ulichonacho litasepa police wataondoka na roho yako police hawa wana tamaaa sana wako radhi wafanye chochote wapate ela ila mungu hadhihakiwi
 
Sijui tatizo lipo wapi ila polisi wanakandamiza haki za raia kwa kuwaweka ndani bila ya sababu za msingi hata kwa makosa yanayodhaminika na wakati mwingine kwa kesi za madai, kuna tatizo kubwa bado kwenye mfumo wetu wa haki jinai, tunaongeza msongamano wa wafungwa na mahabusu wakati wanatakiwa waende wakazalishe na kujenga nchi
Nilisoma makala moja kwamba home affairs ya southafrica imelipa watu bilions kwa sababu kama hizi sijui kwanini mfumo wetu usirekebishwe
 
Sheria inataka umueleze mtuhumiwa kosa lake kabla ya kumkamata ,ni uvunjaji wa sheria na hata katiba unapoamua kumnyima mtu uhuru wake na kumdhalilisha
 
Kituoni uliambiwa una kosa gani ?
Je ulitokaje kituoni kwa kudhaminiwa au kuruhusiwa bila masharti yoyote ?

Ni kweli hukuwa unajua lolote kuhusu eneo hilo ? Je wahusika wamewahi kukuomba radhi kwa yaliyotokea ?
Pole Sana
Kituoni walinipeleka baada ya kuona nimepata majeraha na watu wameanza kudadisi pale njiani. Tulipofika kituoni pale KISASA tulimkuta askari mmoja wa makamo mweupe kidogo, mwembamba mrefu. Waliaongea nae kidogo tu wakaondoka na pikipik yao SINORAY. Baada kama dakika ishirini yule askari wa kituo aliniruhusu bila maandishi wala maelezo yeyote. Kiufupi baada ya kutoka pale kituon sikufanya chochote wala kumwambia yeyote mpaka leo hii, kwa kuhofia kupoteza muda na fedha. Namwambia tu afande FRED na mwenzake mfupi, mweusi ana mwili kidogo kuwa sitowasahau KAMWE na NIMEMUACHIA MUNGU.
 
Pole sana
 
Rais aliunda Jopo la kurekebisha haya so inatakiwa kihoji utekelezaji wa mrejesho wao umefikia wapi?
 
Mbona inaeleweka Polisi huzingatia Taratibu zilizowekwa kisheria katika Utekelezaji wa majukumu yao. Wewe ilkuwaje?
Polisi hawajawahi kuzingatia taratibu zao, wao hutumia vitisho na mikwara pamoja kumuweka mtu selo ili atoe pesa au ndugu zake watoe pesa.
Wakiona pesa au dalili kwamba pesa zinatolewa hapo ndiyo utaona tone inabadilika wanakuwa friendly na kuanza kujichekeshachekesha kama mabwege, unaona mtu anaitwaitwa kutoka selo akae kwenye benchi au anapitiwapitwa hapo selo kuulizwa kama yuko poa.
Wanazingua sana, mchawi wao huwa ni pesa au ipigwe simu kutoka mamlaka za juu wapigwe mikwara hapo ndiyo huwa wanaanza kutafutana na kuhaha.
 
Imefika mahali ni afadhari ukutane na jambazi huenda anaweza akaingiwa roho ya huruma sio hawa polisi wetu wana unyanyasaji mkubwa sana aisee sina hamu na hawa watu hasa akisha jiona kabeba bunduki na kavaa jezi anajiona ni mungu.
Askari polisi wana roho mbaya zaidi ya majambazi, kukiwa na issue mbaya inayowahusu wakajua kuwa wewe unaifahamu wanakuua bila hata ya kujiuliza mara mbili lakini jambazi anakuwa hatari pale anapokuwa kwenye operation zake nje ya hapo they're cool dudes.
 
Safi sana hii 👆 👆 komenti. Polisi wakikusoma ndipo wanaanzisha mikwara. Lakini ukikomalia msimamo wako watajirudi kwani nao kama binadamu wengine wanayo hofu ya "huyu anapata wapi ujasiri na kushupaa hvi"? Cha msingi ni wewe kutoogopa kuwekwa selo. Selo zimejengwa kwa ajili ya watu; na watu ni mimi na wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…