Mgeni nyumbani ambaye ni kero, mzigo na anataka kuiendesha nyumba kuwazidi hata wenyeji?

Sijui kama wewe imewahi kukutokea, lakini kwangu ndicho kinachoendelea na uzalendo unaanza kunishinda. Ni hivi, nina ndugu wa kume wa mke wangu, ana changamoto za kimaisha na kiuchumi, tunamhifadhi hapa nyumbani kwa muda, ajipange na kisha tuangalie namna gani tunaweza kumsaidia asimame kwa miguu yake mwenyewe.

Maisha si kusaidiana? hata vitabu vya Mungu vimesisitiza kusaidiana wakati wa shida, lakini kinachoendelea sasa nyumbani ni kwamba mgeni wetu amekuwa kero, amekuwa mzigo na natamani aondoke hata leo kabla hata hajasimama kwa miguu yake mwenyewe.

Tumejitahidi kumpa hifadhi na mahitaji yote muhimu, pazuri pa kulala, chakula cha uhakika, matibabu na mahitaji yote ya lazima. Anapiga kinywaji kama hana akili nzuri almost kila siku, analalamika hata baadhi ya vyakula havipendi hata kama nyumba nzima ndicho kinacholiwa kwa watu wote, ana demand apewe aina fulani ya milo, anataka 'pocket money', yaani ...

Kama umeshawahi kuwa na mgeni kama huyu kwako hebu tupe uzoefu wako!
Yamekwisha nitokea mkuu.
Tena alikuwa ndugu yangu kabisaa!
Tatizo lilianza pole pole baada kukaa ya miezi miwili.

Mara mamsap akaniambia mgeni anamgongea hausi geli hodi uchi chumbani kwake.

Nikamuonya mgeni, akasema shetani tu!

Baada ya mwezi hausi geli akaona kero zinazidi usiku, mgeni anataka kum rape!

Usiku huo hausi geli akapiga simu kwao kulalamika,unajua tena tunawachukua watoto wa majirani zetu kijijini.

Mimi sina hili wala lile, asubuhi nikapigiwa simu toka kijijini, mbona mwataka kumchafua mwanetu?

Kwa kweli nilitahayari, nilikasirika na nilifura.

Jamaa yangu nikamfokea kama mtoto mdogo!

Yeye akaniambia naondoka, sikumjibu lakini nikaona heri!

Cha ajabu mgeni alikuwa na ndugu zake wa damu, tena wawili mjini, lakini hakuenda huko, akarudi kijijini.

Mpaka leo nashangaa, lakini nilifanya vema kumtimua kiaina.
 
uyo ndio tabia zake ndio mana washkaj wote tumemnawa analawama kama nn tena usiombe awe kvant atakulalamikia washkaj waliomfelisha mara magar yake n kero tupu
 
Bila kusikiliza utetezi wa upande wapili siwezi comment hapa...
 
Kwani mmeshindwaje kabisa kulimaliza humo ndani?

Akiwa ndugu wa mume, mwamume asimame na kumueleza ukweli wa maisha na akiwa ndugu wa mke basi mwanamke asimamie show.

Wageni wa familia ni wapitaji tuu hawawezi kuwa na control ambayo nyie wenyewe hamjairuhusu
Unakuta mwanamke anakaushia upuuzi kama huu na Ukimwambia ashughulike nao anakuona kama unamfitinisha na ndugu zake. Ukifanya maamuzi magumu anaweka kisasi kuwa na wewe ndugu yako akija basi lazima alipizie.

Ndugu wanaharibu sana ustawi wa familia bora. Unakuta maza anakuja kaa kwa binti yake zaidi ya miezi sita, sasa hapo unategemea kutakuwa na usalama kweli?!
 
Mama kukaa kwa mkwewe miezi2 bila sababu ya msingi, sio ugonjwa wala matatizo eti anakunwa bia🤔🤔

Unamruhusu kwa upendo kabisa na nauli.... ambebe mama yake warudi kwao nyumbani akakae na mama yake hadi hamu iwaishe ndio arudi nyumbani kwaķe
 
Mimi shemeji yangu wa kiume alitaka kuniletea za kuleta nikamnywea Konyagi nikamuangushia jumba bovu alfajiri yake alkafungasha mpaka Ubungo

Kuanzia siku hiyo heshima na amani
 
Sijui kama wewe imewahi kukutokea, lakini kwangu ndicho kinachoendelea na uzalendo unaanza kunishinda. Ni hivi, nina ndugu wa kume wa mke wangu, ana changamoto za kimaisha na kiuchumi, tunamhifadhi hapa nyumbani kwa muda, ajipange na kisha tuangalie namna gani tunaweza kumsaidia asimame kwa miguu yake mwenyewe.

Maisha si kusaidiana? hata vitabu vya Mungu vimesisitiza kusaidiana wakati wa shida, lakini kinachoendelea sasa nyumbani ni kwamba mgeni wetu amekuwa kero, amekuwa mzigo na natamani aondoke hata leo kabla hata hajasimama kwa miguu yake mwenyewe.

Tumejitahidi kumpa hifadhi na mahitaji yote muhimu, pazuri pa kulala, chakula cha uhakika, matibabu na mahitaji yote ya lazima. Anapiga kinywaji kama hana akili nzuri almost kila siku, analalamika hata baadhi ya vyakula havipendi hata kama nyumba nzima ndicho kinacholiwa kwa watu wote, ana demand apewe aina fulani ya milo, anataka 'pocket money', yaani ...

Kama umeshawahi kuwa na mgeni kama huyu kwako hebu tupe uzoefu wako!
Sijawahi na Wala sitegemei kuwa na mgeni wa design hii kamwe.

We jamaa utakuwa mzembe Sana na inawezekana mke wako ndiye kichwa Cha familia.

Kama wewe ni mume na ndiye kichwa Cha familia usingetakiwa kuleta bandiko Kama hili hapa.

Watu wengine mnadhalilisha Sana great thinkers na post zenu za kipuudhi.

Fukuza huyo mpuudhi haraka Sana na mke wako akileta za kuleta mrudishe kwao aende na huyo kaka yake akadiscus vizuri na wazazi wake Kama wewe uliwatolea mahari yeye na kaka yake.

Watu wengine mnajirudishaa nyuma kwa kulea wajingawajinga Kama hao
 
Sijui kama wewe imewahi kukutokea, lakini kwangu ndicho kinachoendelea na uzalendo unaanza kunishinda. Ni hivi, nina ndugu wa kume wa mke wangu, ana changamoto za kimaisha na kiuchumi, tunamhifadhi hapa nyumbani kwa muda, ajipange na kisha tuangalie namna gani tunaweza kumsaidia asimame kwa miguu yake mwenyewe.

Maisha si kusaidiana? hata vitabu vya Mungu vimesisitiza kusaidiana wakati wa shida, lakini kinachoendelea sasa nyumbani ni kwamba mgeni wetu amekuwa kero, amekuwa mzigo na natamani aondoke hata leo kabla hata hajasimama kwa miguu yake mwenyewe.

Tumejitahidi kumpa hifadhi na mahitaji yote muhimu, pazuri pa kulala, chakula cha uhakika, matibabu na mahitaji yote ya lazima. Anapiga kinywaji kama hana akili nzuri almost kila siku, analalamika hata baadhi ya vyakula havipendi hata kama nyumba nzima ndicho kinacholiwa kwa watu wote, ana demand apewe aina fulani ya milo, anataka 'pocket money', yaani ...

Kama umeshawahi kuwa na mgeni kama huyu kwako hebu tupe uzoefu wako!
Mkuu umejiridhisha kuwa sio shoga?
 
Tatizo sio huyo mgeni...tatizo ni nyinyi wenyeji.

Mgeni yoyote akija kwangu lazima kuna taratibu za nyumba atazikuta na kuelezwa hata kama ni ndugu wa karibu sana nahakikisha nitatumia mbinu za kumueleza au kufanya asome taratibu zangu bila hata kumwambia.

Huyo mgeni wenu anafanya hivyo kwa sababu hakuelezwa taratibu zenu mlipompokea.Na hii sio kwa mgeni tu... binadamu yoyote ninayehusiana nae lazima afahamu taratibu zangu.. hata boss anayekulipa mshahara au mume/mke/jirani/rafiki... lazima wafahamu taratibu zako. (nini unataka na nini hutaki...) Tofauti na hapo utakuwa unaishi duniani maisha ya ajabu ajabu sana

Remember;
No one can make you inferior without your permission
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
eti anaomba poketi money hahaha,.... mimi yupo hapa toka mwezi wa 6 mwaka jana hataki kazi yoyote, ukiondoka unamuacha na remote ukirudi na remote umeme ukikata anaenda kulewa.....sahizi amejifunza angalia cartoon ukimkuta na mtoto burudani tu

na ni mwanaume mkubwa 44years, alikuwa huko mtwara amerudi ndio yupo hapa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aisee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mimi nikienda kwa watu hata nijisikie uvivu vipi lazima nijikaze nifanye kazi.
Dah wamepata pa kupumzikia...nyumba ina watoto 4,nahangaika na watoto wadogo, nahangaika na watu wazima pia[emoji1787][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
As If wapo hotel...... Kwangu hayo hayawezekani ! Nakupangia kazi kama wewe huwezi jituma.... Failure to do so uende tu[emoji23]
 
Acha tu
Naugulia maumivu..yaani asbh niwahangaikie..mchana nikimaliza mihangaiko yangu nawakuta wanasubiri nitoe vyombo mezani vyombo walivyonywea chai niliyowawekea mwenyewe,nikaoshe,niwapikie,wale[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Huu upole mnautoaga wapi? Siku hizi bangi zangu zinavyonipeleka puta mbona wangeniachia laana
 
Aisee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mimi nikienda kwa watu hata nijisikie uvivu vipi lazima nijikaze nifanye kazi.
Dah wamepata pa kupumzikia...nyumba ina watoto 4,nahangaika na watoto wadogo, nahangaika na watu wazima pia[emoji1787][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Ukiacha kuwapelekea maji ya kuoga nini kitatokea? Maji si yanajulikana yalipo? Au unaowazungumzia ni wazee?
 
Kuna watu mna roho nzuri..yani mgeni anapewa mpaka pocket money?pathetic
 
Back
Top Bottom