Mgogoro ndani ya Simba unafukuta, Mo na bodi yake wasusa, Simba yasafiri Kwa njia ya barabara kuelekea Tabora

Mgogoro ndani ya Simba unafukuta, Mo na bodi yake wasusa, Simba yasafiri Kwa njia ya barabara kuelekea Tabora

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,871
Reaction score
39,881
Baada ya suluhu ya mgogoro wa derby huko Ikulu Dodoma umekuwepo mgogoro mkubwa kwenye timu ya Simba

Bodi ya Simba na mdhamini mkuu Mo Dewji hawakufurahia uwakilishi wa viongozi wa Simba ambapo wengi walikuwa wazee wa Simba akina Dalali na Hasanoo

Wazee hao wa Simba hawakuwa na hoja au matakwa Yao ya kuwasilisha mbele ya Rais, TFF na bodi ya ligi zaidi wao waliburuzwa na kukubali kila jambo la Yanga

CEO wa Simba Bi Zubeda na viongozi wengine waandamizi hawakujulishwa kuhusu kikao hicho

Maamuzi ya hicho kikao ilikuwa kuhairishwa mechi hadi 25 June, hili limewaudhi wengi

Leo Simba wamepanda SGR asubuhi kuelekea Dodoma na baada ya hapo watapanda basi kuelekea Tabora ambapo watatarajia kufika Tabora saa 11 join na mechi ni kesho, hapa Kuna athari za uchovu wa safari utaathiri timu

Mo amesusa amesema hatatoa support yoyote na anaombwa Simba apigwe mechi zote kutia ndani mechi ya derby

Mangungu ameachiwa timu na anaendesha kiugumu

Tuombe Mungu huu mgogoro uishe salama
 
kwani mo anatoa msaada simba ama ipo kisheria umiliki wake

anasusa vp ikiwa mikataba imesainiwa ama anajiamulia tu kutoa na kuacha kutoa hela
Kwani jukumu la Mo ni kutoa pesa? Pesa huwa anatoa kana hisani tu kwa team ila majukumu yake kama mmiliki mwenza (japo bado mchakato unaendelea) hayajumuishi kutoa pesa za safari. Ndomana kuna budget ya team.
 
ndo nauliza kama kuna budget ya timu sasa mo izo pesa anatoa za nini kwamba akiacha kutoa timu ina athirika
 
Huu unaweza kua mtego nawashauri yanga wasiamini sana hiki wanachokisikia
 
Back
Top Bottom