Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Umetoa mfano wa mkoloni kupima Oyster bay, kwani tangu mkoloni aondoke serikali haipimi viwanja? Unaukumbuka mradi wa viwanja elfu ishirini hapa Dar ambapo maeneo ya Bunju, ununio, Boko, Mivumoni, Kijichi, Kibada, Mikwambe, Tuangoma, Mwanagati yalipimwa? Serikali kila mwaka nchi nzima viwanja hupimwa lakini kwa utaratibu kutrgemeana na ukuaji wa miji. Dodoma baada ya Serikali kuhamia huko vimepimwa viwanja vingi tu. Huwa husikii matangazo ya kuuzwa viwanja vilivyopimwa?
Kama huna hela ya kununua kiwanja kilichopimwa wewe endelea kupanga sio vibaya.

Dunia nzima sehemu kuna sehemu wanazoishi maskini ambazo ni slums hata US na ulaya wapo homeless ambapo ni sawa na slums tu.
Serikali imekuwa ikiboresha makazi yasiyopimwa kwa mfano kule Hananasif.
Unataka wanaoishi maeneo yasiyopimwa wanyang" anywe kwa kisingizio cha uboreshaji ! Unayajua maumivu ya kubomolewa wewe? Watu walipovunjiwa wakati wa upanuzi wa barabara ya Morogoro licha ya kuwa wamiliki wa awali walikuwa wamelishalipwa lakini watu walilalamika sana na pia walipoondolewa mabondeni. Katika maeneo hayo watu wanaendesha mfumo wao wa kiuchumi mfano kuna waliopangisha vyumba na fremu na wanalipia watoto wao vyuo vikuu na sekondari za kulipia; ukiwahamisha unavuruga mfumo wao wa kiuchumi hivyo itapelekea watoto wao kufukuzwa vyuo na shule kwa kukosa ada na familia kusambaratika.

Umeniuliza kama ninapajua Oysterbay na Masaki! Jibu lake niliwahi kuishi kwa muda ile Oysterbay original wakati nakua wakati huo Masaki ikiitwa Kichangachui. Pia umeuliza elimu yangu, ungetaja yako kwanza ili nami nitaje yangu ili ulinganishe vizuri.

Endelea kupiga kampeni kwani ni haki yako lakini ukubaliane na matokeo ya sanduku la kura bila visingizio.
 
Tunamuhitaji sana Lissu kama kioo cha uwanja wa sheria kuliko mwanasiasa.
 
Mimi sio mamlaka ni msomaji waJf ila huwa sipendi unafiki. Maoni yote ninayotoa humu ni yangu binafsi jinsi ninavyoliona jambo. Ila athari za kukosekana amani ninazijua madhara yake yanagusa jamii nzima ndio maana mtu akitaka kufanya jambo ambalo litatuathiri wote nalikemea.
Nilichosema tusubiri uchaguzi ufanyike halafu tuone kama hautakuwa huru na haki sio kuhukumu kwa confidence kuwa utaibiwa kura. Na nimekutaka ukishindwa kihalali uwe na ujasiri wa kukubali sio kupotosha umma.
 
Ndugu, #Ajira hakuna kabisa tangu 2015 hadi sasa.Ni huruma sana ndoto za graduates zimefungwa na mchawi mmoja tu! yeye akisema ndipo zinatolewa.Wenye shahada za #Ualimu masomo ya #Sanaa wanachakujifunza kwa tangu mwaka 2015.
#Dictator Never Never Never Ever and Ever again!
 
Mbona vijana wameajiriwa sana au haupo TZ!! Madaktari, Walimu, Wanajeshi etc. Wewe unazungumzia ajira gani mkuu?
 

We utopolo vipi mbona umekomaa hivyo au unaleta habari za UDP hapa ,hukumuona Naibu katibu Mkuu Mwalimu.
Au kwa kuwa vyombo vya habari mmepigwa mkwara kuripoti tukio la leo.

Endeleeni tu ngoja Oktoba tuwakomboe kutoka makucha ya mkoloni mweusi.
 

Ajira za waalimu nchi hii ziko toka enzi za mkoloni. Cdm ina itikadi yake, hivyo haina ulazima wa kushirikiana na chama chochote. Msajili wa vyama vya siasa ndio mlezi wa vyama vya siasa, na wala sio jukumu la cdm kuviunganisha vyama. Inawezekana una point, lakini una uwezo mdogo wa kuziwasilisha, tumuombe Mungu kama waalimu ndio nyie.
 
Mbona vijana wameajiriwa sana au haupo TZ!! Madaktari, Walimu, Wanajeshi etc. Wewe unazungumzia ajira gani mkuu?

Waliofukuzwa kwa vyeti fake kwa mujjibu wa serikali kama sio data za kupika ni 19,000+. Lakini ajira zilizotoka ndani ya miaka hii mitano, sidhani hata kama zimefika kujaza hao walifukuzwa kwa vyeti fake.
 
Waliofukuzwa kwa vyeti fake kwa mujjibu wa serikali kama sio data za kupika ni 19,000+. Lakini ajira zilizotoka ndani ya miaka hii mitano, sidhani hata kama zimefika kujaza hao walifukuzwa kwa vyeti fake.
Kwani lazima zijazwe zote kama zilikuwepo zingine za magumashi je??
 
NEC na polisi mnakwama wapi. Lissu anakuja kwa maandamano JPM na CCM hafanyi hivyo. Lissu anawafanyisha kazi 88 na weekend JPM hafanyi hivyo. Mkwara wa kusema asipowakuta ofisi zenu halali yao imewafanya mfyate mkia?
 

Unaongea nini dogo, unanitaka nikishindwa kihalali nikiri, nimekupa mifano ya chaguzi zote toka awamu hii iingie madarakani, kuwa haikuwa halali na uligubikwa na ushenzi mwingi tu. Lakini unataka nikiri nikishindwa, kwa hiyo mimi ndio mamlaka? Ww ni mnafiki usiyejitambua, amani ni tunda la haki, ufumbie machi haki, kisha ujifanye unajua thamani ya amani! Shubamiit.
 
Aisee huko Cdm kuna wengi watoto na Mawazo ya kitoto sana!
Ndio maana jf imejaa viroja na matusi tu badala ya hoja zenye uzito!
Imagine tunajadili hii thread 😁😁😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…