Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Naona TBCCM na Channel ten tayari wako na UvCcm yao. Yaani Tbc wana vitu vya ajabu sana. Jana walikuwa full cover kwa wabeba mbeleko za Ccm wakati NCCR wakifanya kikao chao cha ndani.. Leo tukio la Chadema msiwategemee maana sio walipa kodi wa nchi hii.
Nafikiri baada ya uchaguzi itungwe sheria Tbc isiwe ina pewa ruzuku za serikali. Ipewe ruzuku na Ccm
Ngoja tuchukue nchi, watakula walipopeleka mboga
 
Niko area D watu wabugujika machozi ya furaha kwa kutaka kumuona Mh, Lissu ..aaah Magufuli yuko ICU hawezi kutoboa hata mshindi wa tatu hataingia ,nadhani hii coalition yake na Tlp ndo itamsaidia kuingia top 5
Tunza mane yako haya tarehe 28 Oktoba 2020 usilielie baada ya watanzania kuamua JPM aendelee kwa miaka 10!
 
Nina maswali najiuliza.
1. CHADEMA walisaini zile kanuni za uchaguzi?
2. Fomu zinakaguliwa kwa usahihi muda gani?
3. Kwa njni tume imebadilisha mfumo wa kulipia bank na sasa vyama vinalipia Cash?
4. Huko nyuma tumeona wagombea wakiporwa fomu baada ya kuchukua au kurudisha, Je tume imeweka utaratibu gani juu ya hili?
 
Tunaomba ambao muko kanda ya kati mtuwakilishe wengine ambao tuko nje ya jiji la Dodoma katika kumsindikiza Mheshimiwa Tundu Lissu kuchukua fomu.
Hakika ni miongoni mwa tukio kubwa litakalofanya Dodoma na vitongoji vyake kuzizima leo.
 
Niko area D watu wabugujika machozi ya furaha kwa kutaka kumuona Mh, Lissu ..aaah Magufuli yuko ICU hawezi kutoboa hata mshindi wa tatu hataingia ,nadhani hii coalition yake na Tlp ndo itamsaidia kuingia top 5
Photo plz. Tupeni raha basi
 
Sijui itakuwaje mkishindwa, duh kila kotu kwenu kama hakikuenda kama mpendavyo, basi hakiko sawa.

Mshazoeleka hakuna anayeshtuka na youote mnatakoyokuja nayo.
 
Nakubaliana na wewe , wengi wanamsifia magufuli usoni ili mkono uende kinywani ila moyoni hawapo nae kabisa.
Na mimi najenga nyumba ya gorofa 200 Kariakoo. Nina hakika hela zitaniishia katika uchimbaji wa msingi kabla hata nondo za huo msingi sijanunuwa.

Fikiria, mradi wa mabasi ya mwendokasi umetushinda juu ya kuwa nauli ni x1.5 zaidi ya daladala. Nini chengine tutaweza?
 
By the way mtu anayeleta maendeleo ila hathamini utu wa watu huyo kwangu simthamini kabisa. Tundu lisu najua hataweza hata punje kuleta maendeleo lakini atajali sana utawala wa haki na sheria, sitarajii kusikia watu wakipotea chini ya tundu lisu.Mungu atutangulie atuwezeshe.
Mkuu maendeleo ya nchi hii yanaletwa na wewe na Mimi si magufuli.Achana na propoganda uchwara za hawa wajinga wa ccm
 
Back
Top Bottom