1. Ni Kitu gani cha Kimaendeleo unadhani Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli haijafanya na Yeye akishinda atakifanya?
2. Ni kwanini anahusisha Tukio lake moja kwa moja na Serikali na kamwe si Maadui zake wengine labda nje ya Siasa?
3. Je, ana Uadui wa Kisiasa tu au ana Chuki Binafsi dhidi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli?
4. Je, CHADEMA ya sasa ni Taasisi au ni ASASI tu yenye Umiliki wa Kudumu kutokea Mkoani Kilimanjaro aliko Muasisi wake?
5. Je, akishinda Urais ataendelea kubakia na Msimamo wa Rais Magufuli na CCM yake Serikali ihamie Dodoma au atautengua upesi?
6. Je, Watanzania wanahitaji Mabadiliko ya Katiba au Misingi ya Kimaadili yenye Utashi mwingi wa Kiuwajibikaji na Kiutendaji?
7. Je, ni kweli kwamba hulka ya Wapinzani wa Tanzania hasa wa CHADEMA ni Kupinga tu kila Kitu na hakuna Jema CCM imelifanya?
Nakukubali sana tu Dada yangu Farhia Middle na Wewe unalijua hili kutokana na 'Uwerevu' wako, ila sijui leo kwanini umeniangusha Kimaswali hivi.