Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Wana bahati wangefanya huo mgomo kipindi cha mwenda zake, sasa hivi tungekua tuna hesabu maiti za viongozi wa hilo soko.
Ndo maana Mungu aliamua kuwatetea Watanzania. Aliua sana na yeye kwa sasa ni mifupa mitupu kaburini bila kujali kaburi lake limepambwa na kulindwa usiku na mchana.
 
Ni vizuri serikali ikatatua matatizo yanayosababishwa na watumishi wa mamlaka zilizopewa jukumu la kukusanya kodi, RUSHWA nchi imehalalishwa na viongozi ambao wameweka mbele tamaa zao binfsi.
 
Hakuna mjomba wa kuwajengea Nchi,sio lazima Kila mtu afanye biashara,Kodi ya mtumishi ni kubwa kuliko Mfanyabishara mkwepa Kodi..

Serikali ikisema isimamiwe Sheria wote mtakuwa jela Kwa uhujumu uchumi,Sasa ni ajabu hata hiyo ndogonataka msilipe.
Mtumishi yupi unayemuongelea ambaye analipa kodi kubwa kuliko mfanyabiashara mkwepa kodi?
 
Shida ya kodi Ni kwamba wananchi tunaona zinatumika vibaya

Huwa nashangaa sana viongozi wanaodharau wananchi wao Ndo wanawalisha na kuwavisha Mia Mia za machinga na watu wa hali ya chini Zinafanya wao wawe juu

Hatutaki kudharau hawa watu kabisa
 
Hii inatumika kama justification ya kuwasumbua wafanyabiashara K/Koo na sehemu zingine za biashara ktk nchi hii. But sababu kubwa ni kutaka rushwa tu, period!!!!!!!!!!!!
 
Kwa mtazamo wangu Serikali inapata kodi ya kutosha lakini haina mpango madhubuti wa kusimamia vizuri matumizi. Kodi ya wafanyabiashara iwatengenezee mazingira mazuri ya biashara. Tuna nchi ambayo tunanunua magari ya gharama kuendana na wakati kwa ajili ya wakuu wa wilaya lakini bado hatuna miundo mbinu salama ya kukuza biashara. Mfano kuruhusu watu kuendelea kuagiza bidhaa nje badala ya kuwapa ruzuku kuruhusu uzalishaji wa ndani ni kitu kibaya sana. Pia nchi yetu mfanyabiashara anaonekana ni chanzo cha mapato, inabidi tuwekeze katika mazingira mazuri ya uwekezaji ili ajira nyingi zitengenezwe. Na cha kuongeza serikali itumie vizuri Kodi ili kila mtanzania ahamasike kulipa kodi. Kwangu mimi kuona kila Landcruiser mpya ikitoka serikali inanunua bado hamjanishawishi. Ninalipa kodi ninayoona serikali inastahili na si zaidi. Na kijijini kwetu maendeleo mengi tumefanya sisi wenyewe wanakijiji kwa kuchangishana. Kwa hio sijahamasika kabisa.
 
Kama umewahi kufanya biashara kipindi cha tech za efd , Vat and the likes kuna kipindi at your will unatamani kabisa ufunge biashara kwa hiyari. Ili upumzike na usumbufu wa Tra.
Halafu kariakoo kusimama kishughuli sio jambo dogo ati.
True kabisa, wanakadiria wanavyojisikia
 
Kwan mipakani ndio hazichajiwi kodi mkuu au ulitaka kusemaje sijakupata vema?!
Kunatofauti kubwa kati ya mpakini na Bandari mkuu pale bandari kuna mamlaka nyingi sana kuna rushwa inatembea wanajua ukichelewa storeji inangezeka kilasiku boda tualipa pesa za Custom tu

lakini bandari kuna utaambiwa TPA TBS SIPING kwajili ya Delivery Order utaambiwa lipa pesa ya ukaguzi wa Mizigo utaambia lipia Lent utaambilia lipa storage mala agency fee kuna uswahili mwingi pale ukishindwa wanapiga mnada umesikia boda kuna hizo hekaheka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…