Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Sheria za ongezeko la kodi kutokana na mnyororo wa thamani , tumekurupuka , hizi ni system za kibepari hazifanyi kazi vizuri kwenye nchi zaa kijamaa .leo hii vat kwa kuepuka ugomvi na mamlaka wafanyabiashara wameziweka kama gharama ya biashara , maana ili ulipwe vat ni lazima ufanye biashara na kiwanda.
 
Punguza makasiriko
Kodi inayokadiriea na TRA ni kuwakomoa wafanyabiashara bila kujali sisi walaji.

Naunga mkono mgomo

Najua sasa wanasakwa viongozi wa mgomo kwa udi na uvumba ili wahasiwe kama walivyomfanyia unyama Ulimboka
Sina makasiriko, mgomo hauandaliwi na mawazo ya kijinga yanayopingwa kirahisi. Weka mawazo yaliyonyooka na sababu zisizo na shaka ili mamlaka ibanwe kutoa suluhisho. Sio sababu uchwara za kudai kodi ikatwe bandarini na mipakani, TRA wasiviziwe. Kwa sababu hizi hamna popote mgomo unafika.

Sababu za kugoma zipo nyingi sana na kuumiza kichwa serikali, ila wanaogoma hawana kauli nzito za kusimamisha.
 
Nani kakuambia petrol station hazilipi kodi za ndani?
 
Kodi za bandarini na dukani ni tofauti
 
Acha uongo. Kodi za mafuta ziko nyingi na hazitozwi bandarini tu. Kodi za mapato, ushurunwa halamashauri, PAYE, SDL n.k. vinatozwa nje ya bandari.
 
Sasa ndo wamegoma na hauna la kuwafanya.

Tuma askari wakawatwange hadi wafungue maduka
 
Punguza makasiriko
Kodi inayokadiriea na TRA ni kuwakomoa wafanyabiashara bila kujali sisi walaji.

Naunga mkono mgomo

Najua sasa wanasakwa viongozi wa mgomo kwa udi na uvumba ili wahasiwe kama walivyomfanyia unyama Ulimboka
Mkuu labda twende sawa , Tra ni watch dog tu , watunga sera (wabunge )ndio wenye shida , na tupo kwenye migogoro hii kutokana na sheria mbovu zilizotungwa na bunge letu tukufu.
Mapendekezo ya Tra kwenda bungeni kwa wakati fulani yanakuwa makali kutokana na usumbufu wanaoupata wakiwa kazini, ila bunge lingekuwa imara kuna baadhi ya vitu havikutakiwa kabisa kuwa sheria kama vingejadiliwa kiufasaha.
 
Bure kabisa wewe. Kwa hiyo meli ikiwa baharin ikiingia tu kwenye maji ya TANZANIA ya tanzania kwenyebahari ya hindi TRA wanapanda kwenye meli kuanza kutoza kodi
 
Wanaohimiza kulipa kodi,,wao hawalipi kodi sasa si usenge huu!!!
 
Ni kweli zina shida, ila hazijatungwa na TRA. Yani matatizo yetu makubwa ni kuongozwa na vilaza na watu wasioelewa, tatizo mara nyingi sio watekelezaji. Wafanyabishara watatumia TRA kukataa matakwa ya serikali ila serikali ndio ina shida wala sio TRA ambao ni mtekelezaji.

Serikali ikitaka kuwakataa na kuwaonyesha wanadai mambo yasiyowezekana itatafuta makosa kwenye madai yao. Waandae muswada mzuri wagome wakiwa na kauli nzito, sasa hivi ukiwatafuta utakuta kila mmoja anaongea la kwake sasa mgomo gani unafanikiwa hivyo
 
Mamlaka ya TRA haina uzi humu tuitag ione malalamiko ya wananchi? au ikiwezekana tukatoe malalamiko kwenye uzi wao.
Tuanze na bungeni , ndio kunakozaliwa matatizo yote haya. Siasa mbovu huzalisha sheria mbovu
Sheria ya uhujumu uchumi kwa mfano imetumika vibaya sana awamu ya tano ,kuadhibu wanasiasa na walioupinga utawala ule na hata hii leo Tra wakitaka kukukomoa wanakupa kesi ya uhujumu uchumi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…