Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Hoja ya kuviziana nimekubali uko sahihi. Hoja nyingine mbili haziko applicable.

Kwanza, mafuta ya Tanzania yanapitia sehemu moja, Kigamboni. Yanashushwa sehemu moja hivyo ni rahisi kufuatilia kila kitu na wakati huo kafuatilie mfumo wa uagizaji wa mafuta wa bulky purchase utajua kwanini makato yake ni sawasawa. Mfumo huu huwezi utumia kwa muuza simu, huyu kanunua Oppo from China, huyu kanunua used Google Pixel from Dubai, huyu Apple from US.

Pili, Dubai sio Tanzania na ni exception duniani kufanya biashara. Mfumo wao ni mzuri kukaribisha wageni na uchumi wao umetengenezwa hivyo kuwa business hub na biashara zao zote kama real estate, bandari kubwa duniani, airport kubwa, hospitality, Fly Emirates & Fly Dubai inaungana kufanikisha mfumo huo wa uchumi. Kuna nchi nyingi sana tunaweza iga ila sio Dubai, gharama za kuifanya Dubai iwe vile tukizitaka mtakatwa kodi ya zaidi ya 50% na mtakimbilia kulima mihogo muachane na biashara.
 
Hao fanya wanatoza elfu 5 tu nayo ni kodi?
 
Hivi hata kiswahili tunashindwa kuandika? Inakuwaje bango la kubandikwa kwenye kadamnasi kama Kariakoo mtu anaandika tumechoshwa na utitili wa kodi badala ya utitiri wa kodi? inamaana hawakuhakiki kabla ya kubandika?
Hili tatizo linaanzia kwa viongozi wetu.

Hakuna orientational ya kiswahili tena unapoomba kazi
 
ACHA WAITAMBUE SAWASAWA.

KWENYE CHAGUZI SINDO WAO HUWA WANAVAA KIJANI NA KUJINADI KUIPENDA SISIEM.


KAMA WANA MAPENZI YA DHATI NA HII NCHI WASIWACHAGUE SISIEM NDO TUTAJUA HAWATANIIII
 
No upumbavu mtupu kutaka mjue mpaka stoo za watu, hii nchi ya hovyo sana yaani mnataka kodi mpaka stoo!!!

Nipo kkoo hakuna mtu aliefungua labda machinga tu
 
Huko ni kutaftana ubaya. TRA mwisho dukan tu. Kufatana store hairuhusiwi
 
Ulikuwa bungeni unafanya nini!?
 
Huu ni ukweli na ndicho serikali inacholenga kuzuia
Serikali imezoea mabavu badala ya kuwaelimisha wahusika.

Haya sasa mukwara na maneno ya OLE WENU imekuwaje sasa?

Kodi ndiyo inayoendesha nchi. Kuikusanya kana kwamba ni vita na unyang'anyi ni kujipalia makaa
 
Hayo makato yana taratibu zake za kukatwa. Sio kwenye risiti. Kama wewe sio mfanyabiashara huwezi kujua.
Wewe bwana najuwa kila kitu sasa ngoja nikupe darasa kidogo, hawa Kariakoo wafanya biashara umewasikia wanalalamikia kodi za Manispaa au kodi ndogo ndogo za ndani? kodi za mapato ni issue nyingine ni makadirio tu na huwa kama unaona kodi kubwa unaongea nao mnafikia njia sahihi japo shida kubwa ya wafanya biashara kukwepa kutoa risiti hili mimi nalipinga sana ni lazima tuwe na tamaduni za kutoa risiti inasaidia kuja kulipa mapato unakuwa na backup sahihi hii ni shida nyingine, malalamiko ni huko kukimbizana mitaani na wenye mizigo container limetoka basi kama limetoka bila kulipiwa basi wafanyakazi wa TRA au bandarini kuna shida hawaaminiki weka mfumo mtu hawezi kutoa kitu bila kulipiwa. Kodi za nje huku zina changamoto lakini tulipo sio pabaya sana tulikotoka. Kuwa na kodi moja kwa kila kitu kama kwenye mafuta wanakata kwa pamoja halafu wanawagawana huko.
 
Tukiachana na yote kkoo kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi. Watu wanafanyia biashara za mamilioni stoo.

kkoo wanaouza kwenye frem ni maskini tu wale wanaouzia kinyemela stoo ni matajiri wa kutupa sijui nani kasanua mchongo huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…