Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Hivi hata kiswahili tunashindwa kuandika? Inakuwaje bango la kubandikwa kwenye kadamnasi kama Kariakoo mtu anaandika tumechoshwa na utitili wa kodi badala ya utitiri wa kodi? inamaana hawakuhakiki kabla ya kubandika?
Muhimu Ujumbe umefika ..
Wafanyabiashara wengi kariakoo sio wasomi ni watu wenye elimu ya kawaida tu.
 
Sina uhakika kama unanunua mafuta kujaza gari yako, weka risiti hapa yenye kodi ya VAT kituo chochote cha mafuta kwanini? sababu wameshakata meli ikifika na mzigo tu hautoki mpaka umelipiwa kodi zote

217AB442-2666-4E51-8C2B-1B8F0A869F66.jpeg
 
Habari wakuu nipo mtaa wa mchikichi huku kariakoo maduka hayajafunguliwa hadi muda huu kuna nini kwani?

Ngoja niangalie na mitaa mingine.



UPDATES...
Muonekano wa maduka mbalimbali katika soko la Kariakoo hadi saa 8.23 asubuhi huku kufungwa kwa maduka hayo kukihusishwa na uwepo wa mgomo wa wafanyabiashara wa soko hilo kongwe na maarufu Afrika Mashariki.

Wafanyabiashara wa Kariakoo wanafanya mgomo wa kufunga maduka wakishinikiza kupungua kwa kodi wanazotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Nina hakika sasa ufumbuzi utapatikana
 
Kwanza andika akitoroka anyway sijui kama nilitakiwa ni kujibu lakini nitakujibu. Ukiona mfungwa katoroka basi ujue gereza lako haliko sawa nenda kazibe kufukuza mfungwa sio suluhisho ni matokeo ua uzembe weka nyumba yako sawa hakuna wa kutoroka. Kama unataka kusema container linatoroshwa bandarini basi nchi iko katika hatari kubwa sana.
Basi ukiibiwa hauna aja ya kwenda polisi au mahakamani, yakupasa ukae kwa kutulia

Na TRA wanacho kifanya huna aja ya kulalamika hivyo ni vyema ukatulia ndugu mzalendo
 
Leo asubuhi nimefika kariakoo kwenye biashara zangu lakini nimekutana na mgomo wa maduka kutofunguliwa

Nilikuwa bungeni kwa wiki kadhaa hivyo sikufuatilia sana mambo ya biashara nikiwaachia vijana

Maduka yamefungwa ingawa baadhi ya wamachinga wanaouza matunda wanaendelea

Sijajua sababu ya msingi zaidi ya ile ya TRA kututaka tuorodheshe store zetu tunazohifadhia mali

Hakuna mfanyabiashara ambaye yupo tayari kwa jambo hilo ,Jambo lilihitaji mjadala mpana

Hakuna fujo ingawa polisi ni wengi wanatembea tembea bila uelekngoma ya watoto huwa haikeshi, Rais wa

Sisi wakinga hatuogopi moto,Kwenye hizi biashara tuna maamuzi magumu sana ambayo wewe huwezi kuyafanya na hata ukiyafanya utakosa furaha maisha yako yote na unaweza ukaishia kuona maluwe luwe
Rais Wa Sasa ameshindwa kazi, awe tu muungwana apishe wengine .
Hii ni trailer tu, changamoto zipo nchi nzima za namna hii
 
Hivi hata kiswahili tunashindwa kuandika? Inakuwaje bango la kubandikwa kwenye kadamnasi kama Kariakoo mtu anaandika tumechoshwa na utitili wa kodi badala ya utitiri wa kodi? inamaana hawakuhakiki kabla ya kubandika?
R na L ni janga la taifa
 
Soma vyema acha ubishi! Elewa pia acha ubishi!

Nenda vituo vya mafuta waulize wafanyabiashara hizo hesabu zao kwenda TRA zipo vipi?
VAT huwezi lipishwa kama hujatoza.
Kutozwa VAT liko kisheria.
Mfanyabiashara hurudishiwa VAT aliyotozwa bandarini endapo ataikusanya kwa anaowauzia bidhaa.

Tatizo huna akili
 
Najuwa hilo nilijibu tu kwa hoja ya mtu kusema kuna mipaka lakini shida kubwa hapa watu wa TRA wanajuwa kuwa kukiwa na mfumo usioingilika utaziba mianya ya rushwa watakufa njaa wanataka tubaki na hii analog mtu aweze tu kuamua kuna nini ndani ya container na gharama waamue nadhani kuna wakala wa kufanya clearance hawa wanatakiwa kuonesha 100% kuna nini na gharama zake ni zipi na viwango vya kodi viko kisheria ukiweka number kodi ni hii sasa kuwe na hali kuweka kiwango kuambatane na doc ku support gharama japo najuwa kuna ujanja mwingi mzigo wa mil 1 wanaweza kuweka laki moja hapa ndio tunatakiwa tutafute tech kuziba hii mianya kama shida kodi ni kubwa hilo na la kisera na serikali ina wajibu kuangalia. Mbona magari hakuna shida hizi, unaleta gari unaingiza model inakupa kodi hii wala huwezi kuchezea ndio maana ukija huku mitaani kwa wauza magari bei zinafanana sana.
TRA wezi sana ni wakala wa wezi wa sio wakusanya mapato kuna watu wanapitisha hela zao huko
 
Mnamkuza tu Mwendazake ingekuwa hivyo watu kama Prof Assad,Nape,Mzee makamba na mwanae, kinana hao watu wangekuwa tushazika kitambo.
Wana bahati wangefanya huo mgomo kipindi cha mwenda zake, sasa hivi tungekua tuna hesabu maiti za viongozi wa hilo soko.
 
Back
Top Bottom