MGOMO: Wafanyabiashara Kariakoo kufunga biashara zao kuanzia 24/6/2024 mpaka changamoto zao zitakapotatuliwa'

wafanyabiashara wameshaanza kuchezesha ukiona ivi ujue tra wameshapita kudai chao

acheni janjajanja bana lipeni kodi kiuhalisia

juzi nmenunua kitu cha 330k cha ajabu jamaa ananganganawatu kunipa risiti ya 250k[emoji15] sa huu si ufala?
Biashara hazina faida kubwa kama wengi mnavyozani hasa kwa ambao hawajawahi kufanya biashara ungeenda duka lingine Kuna wafanyabiashara wapo clear ukitaka bidhaa na risiti halali Kuna pesa inatakiwa uiongeze kinachowatesa wafanyabiashara ni VAT hiyo bidhaa uliyoinunua wewe kwa Tsh 350k kwa risiti halali ilitakiwa ununue kwa Tsh 450k
 
Baelezee papaa, wanataka maendeleo halafu hawataki kuyagharamia
 
Ila tuongee ukweli.kuna sehemu wanakwepa kodi kushinda kariakoo?unanunua kitu cha million 3 wanakupa rising ya laki 3.aladu bado wanalalamika. Mnawalea sana.
Watu wengi hamjui kuwa hiyo Kodi ya risiti haimuhusu muuzaji inakuhusu wewe mnunuzi wafanyabiashara wengi wanaikwepa vat sababu vat inapandisha bidhaa kufanya wateja wakimbie Kodi ya vat ni kubwa sana
Kama ulimununua mzigo wa million tatu vat ni 500000
 
Wakenya wenyewe waoga tu unaandaman unakimbia askari si bora ulale nyumbani tu
Wewe unayelala nyumbani na anayembana na hao askari wanaozuia mandamano nani muoga?...Watanzania waoga na washamba huwezi wafananisha na wakenya kwenye kudai haki zao.
 
kwa hyo wewe ulikuwa unataka wakate shilingi ngapi?
 
Wananchi walikupuuza na mimi nakupuuza vile vile...biashara gani ushawah fanya wewe na ukafanikiwa?
Tatizo ni TRA kudhani inaweza kuwafurahisha watu kama nyie msiotaka kulipa kodi.

Hivi unaweza jibu ata haya maswali mepesi ya kodi.

VAT threshold ya mauzo
Voluntary schemes ya kujiunga na VAT
VAT claims za VAT

Benefits za kuwa VAT registered na benefit za kuwa non registered.

Nani anaamua VAT na rate tofauti ya bidhaa, bidhaa gani kwa Sasa zina zero VAT (moja tu) zipi zina reduced rate ;ya 5% (kwa budget) iliyoisha.

Nitajie uwekezaji mmoja kwenye biashara yako ambayo unaweza ku-claim capital allowance (or depreciation costs).

Vipi biashara yako ikipata hasara, procedurę za kudai tax rebate zikoje?

That’s how stupid I think you are., hata nikikkupa week nzima uwezi jibu maswali yote hayo (dare).:

Ndio mapoyoyo mnailalamikia TRA.

TRA inahusika vipi na makato ya NSSF, NPHIF, business rates, OSHA and other nonsenses.

Lipieni kodi uwezi kufanya biashara bila ya kuelewa costs na kuzipigia hesabu

As for your nonsense in your head nimefukuzwa sijui wapi ain’t got time to respond to that
 
Ni vema polisi wakaingia mtaani kuwalinda watakaofungua dhidi ya kikosi kazi cha wafanyabiashara. Kuandamana ni jambo la hiyari.
 
Usilete ubabaishaji hapa...hivyo unavyo ongea tumecheza navyo miaka na miaka na tumevifanyia kaz...eti week unamtisha nani hapa..income tax act yote ipo kichwani...VAT act yote ipo kichwani...na vifungu vyake vyote...tukiamua kutumia loopholes zilizopo kwenye hiz acts hata mngeenda kwenye mahakama ya dunia ya wapi humfungi mtu...na mbaya zaidi ni kwamba mnatumia viterminology vya kodi kuwatisha watu...juz tu hapa officer ananiandikia fine ya failure to demand...process ya kuiandika tu kwenye computer hawezi...ni aibu naanza tena kumsaidia mwenyewe...kwa kifupi hutaniweza kwa lolote bora ukae kimya...

NB wananchi walikupuuza... usitafute uchawa....na kwa taarifa yako hayupo mtu aliyekataa kulipa kodi...fatilia nyuz vizuri
 
Dini inakujaje hapo
 
Duuuh! Una akili mgando sana wewe
NDO UKWELI NA WEWE UMETHIBITISHA. VERY WEAK. YAANI MAANDAMANO AU MIGOMO YA WATU MNALETA SUALA LA DINI? VERY STUPID KWA KWELI. MNASABABISHA KILA MTU WA IMANI HIYO AANZE KUONEKANA HANA AKILI
 
Hatari na ½
 
Kwa kifupi lipa kodi maana ueleweki unabishania nini.

Kwa TRA mtu anaelewa current VAT rate ya bidhaa anazouza, anaelewa kupiga hesabu za income tax, anatunza vitabu vyake watu kama nyie ndio mnaofaa.

Hayo mambo sio yakujisifu wewe kujua ni standard kwa hesabu za biashara.

Haya sasa elezea shida ipo wapi ya wewe kutaka kuandamana ili serikali ielewe changamoto zenu.

Au unataka kuandamana kwa sababu umeambiwa tu, kwa mtu unaejua sheria, tax rates na kuzilipa TRA hawawezi kumsumbua. Na kwa uelewa huo kama una malalamiko lazima yana msingi.

Haya sasa elezea shida yako ni nini hadi kudai maandamano kama wewe? au ndio mambo ya kufuata mkumbo.

Sijaona sababu mnataka kuandamana kwa sababu gani hasa, ni kama watu mlliotumwa tu kulalamika. Mkiulizww shida ni nini hamna hoja.

Lipa kodi
 
Waanzishe pochi la biashara kama kenya. ( Hii ni benk ndani ya mpesa) Watu walipe kwa Mpesa sio cash.
Hii itasaidie kucontrol na kujua flow of money. Kuondoa matatizo ya kutafuta chenji, kuondoa ukwepaji kodi, lakin pia kusaidia mfanyabishara kwenye savings na expenditure.
Cashless is the way ya kunusuru upotevu wa pesa, kuondoa money loundering, lakin pia kukuza biashara kwa haraka
 
CCM ilivoua elimu bora , ikazalisha kizazi cha mapoyoyo waoga, wafitini , machawa. Hakuna mtu wa kuandamana wala kugoma Tanzania.
 
Nakupa hii...fanya utafiti then utarudi hapa...fanya tafiti hii gharama ya kontena la ft 40 mfano bidhaa iwe vitenge..kutoka china to Tanzania...hilo hilo kontena na bidhaa iwe hyo hyo kutokea China to Kenya au China to Zambia..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…