Interlacustrine R
JF-Expert Member
- Jan 22, 2022
- 7,186
- 14,274
Kufa utakufa tu hata usipoumwa hata ufanyeje, zikifika zimefika tu na haina namna maana ni sheria ya aliyekuumba.nani sasa wa kuachana na mwenzake,
ww ndio uachane na kwenda kumuona kama hautaki kulipa.. uumwe hadi ufe
Sawa bwana dakitariAcha kuziingilia Private Hospitals, Hujalazimishwa kwenda kwao, Elekezeni shutuma zeni kwenye Goverment mana hao ndio wajibu wao kukutizameni nyinyi.
No ni 60,000/= awe muhindi, mzungu au hata mweusimilioni miatano
Lengo hasa la consultation fee ni nini? na je what if kila Fani wakijiwekea utaratibu huo wa consultation fees? maana wote wameingia darasani na wamesota.Tafsiri yake kila mtu anapaswa achunge Afya yake Kwa umakini ili Kupunguza gharama Kama hizo.
Pili, Gharama ya kumuona Daktari haipaswi kuondolewa Ila inatakiwa kuwa Affordable kulingana na Hali za Watu husika.
Hospital ziwekwe kulingana na hadhi za watu.
Kumuona Daktari lazima ulipie ili ujue umuhimu wa kutunza Afya yako mwenyewe.
Kama unaona gharama kumuona Daktari basi yakupasa uzingatie sana mambo ya Afya ili kuepuka Gharama.
Magonjwa mengi yanatokana na uzembe, na siku zote uzembe ni gharama.
Kwahiyo hiyo fee imewekwa kupunguza magonjwa/wagonjwa?Labda useme kuwe na kiwango kimoja kwa nchi nzima...
Ukiondoa hiyo fee, mahospitali yatafurika wakati bado uwiano wa daktari mmoja kwa wagonjwa ni mkubwa...
Hio consultation si ni kazi yake, si analipwa kwenye mshahara! Sasa consultation fee ya nini? Wizi tuu!Elewa kwamba matibabu yanaanzia pale kwenye maongezi ndo anajua shida ni nini achukue vipimo gani aje atoe matibabu gani
Ni kazi yake.. na analipwa kwenye mshaharaKitu usichokijua ni kwamba kuonana na Dr ni muhimu Zaid maaana ni yeye atakayekuandikia vipimo kama inabidi, ni yeye utamrudishia vipimo akusomee majibu, ni yeye atakuandikia dawa kulingana na majibu ya vipimo vyako pia hata kama hatokuandikia vipimo Wala dawa atakushauri vizur tu nayo ni matibabu, Sasa kwann umuone bure?
Lakini ukitaka kujiepusha na hiyo consultation fee ya Dr unaruhusiwa pia kwenda hospitali yeyote ( za serikali excluded) na vipimo vyako ukalipia ukapima na majibu ukapewa ukaondoka nayo ukijua utampelekea nani.
Hachukui yeye hio hela inaingia kwa waliomuajiriHio consultation si ni kazi yake, si analipwa kwenye mshahara! Sasa consultation fee ya nini? Wizi tuu!
Mshahara wa daktari ni 1.48Mje unafaham mshahara wa daktari kianzio chake kinampita mwalimu wa degree zaidi ya mara4?
Kumuona mwanasheria ni 50000/= kabla ya chochote. Hiyo ni consultation fee.Hapo issue siyo kumuona Daktari.
Unacholipia Ni consultation fee.
Yaani kupima vital signs ( pressure, air tract, Breathing rate na kumwelezea Daktari unavyojisikia, halafu akakupa USHAURI na matibabu yake kwa kukuandikia.
Akishakuandikia hiyo 'Kumuona Daktari inaishia hapo"
Na ni special kuliko taaluma yeyote. Kama unaona siyo special njoo usome.Sijasema madktari sio muhimu bali madktari hujiona wao ndio special kuliko wengine na watu kudhani madaktari wanajua kila kitu kuhusu tiba, mnapenda mtukuzwe muonekane ni watu muhimu kuliko wengine kisa tu
nyie madktari mnajua kila kitu.
Kuna siku nusu tupoteze maisha ya bi mkubwa wangu kama nisingejiongeza na kubaki kutegemea mawazo ya daktari ambaye nilishaona kabisa alikuwa anacheza na uhai wa mtu.
Acha uongo. Madaktari hawapati hiyo hela na wala siyo kwaajili ya kumuona daktari. Madaktari tunafeli sana kujieleza.Mleta mada una tafsiri potofu kuhusu gharama ya kumuona Daktari. Kiuhalisia ile sio gharama ya kumuona Daktari bali ni gharama ya kutibiwa na Daktari. Kuonana na Daktari kwa lengo la kutibiwa ndio msingi wa huduma zote za matibabu kwa mgonjwa, na pesa unayolipa ndio inalipia muda wake, juhudi zake na akili yake itakayo tumika kutambua ugonjwa wako na kupangilia matibabu ya ugonjwa wako na wagonjwa wengine. Gharama hizo hutofautiana baina ya hospitali na hospitali au Daktari na Daktari. Kwa hospitali za umma (serikali) ile pesa inaingia kwenye mapato ya serikali na kwa hospitali za binafsi ile pesa inaingia kwenye hospitali husika, Daktari yeye hulipwa na taasisi husika kwa mapatano binafsi.
Consultation fee ni sawa nchi nzima.Naona wangepunguza au iwe sawa hospital zote ukitoa kabisa kutatokea usumbufu kila mmoja atataka kumuona daktar mwingine Hana ugonjwa ambao n serious lakin atataka kumuona Dr
Hujawahi fanya kazi au kupata shida.Lengo hasa la consultation fee ni nini? na je what if kila Fani wakijiwekea utaratibu huo wa consultation fees? maana wote wameingia darasani na wamesota.
1. Mfano, wahasibu- Degree ya kwanza + miaka ya CPA.
2. Wanasheria wasomi - Degree ya kwanza + miaka ya Law School.
3. Maafisa manunuzi - Degree ya kwanza + miaka ya kupata CPSP
4. Maafisa Utumishi- Degree ya kwanza + Mitihani yao ya utumishi.
Utakuta hata hao walio kwenye kada nyingine wamesoma miaka almost the same kama hao madaktari.
Nikweli naunga mkono, consultation fee ifutwe.
Mkuu naomba nikuone pmNenda JKCI Muhimbili
Kumuona daktari ni 35000. kwa consultansion isiyo zidi dk 10
Dawa ni balaa
Dawa ya gout 45000 mtaani 22000
Elenopril ya BP 15000 mtaani 7500
Huo ni mfano mdogo tuu na hospital inapewa ruzuku na mishahara inalipwa na serikali
Ukienda kwenye vipimo Kama huna bima katafute dawa mbadala ni balaa tupu
Mganga wa kienyeji analipwa mshahara toka kwenye kodi ya nani! Tuanzie hapo.Mkuu kumuona mganga wa kienyeji tu unalipia sembuse mtu alie ingia na kusota darasani miaka 6 au zaidi? Itabidi hata tukiwapigia simu tulipie maana tunawasumbua mno.
Mifano uliyotoa ni endapo umepata huduma hizo katika mfumo wa private.Hujawahi fanya kazi au kupata shida.
Maeneo yote hayo imetaja wanalipa consultancy fee.
Kumuona mwanasheria kukushauri ni 50000 unatoa papo kwa papo. Na sijawahi ona mwananchi analalamika na hizi zinalipwa bila shuruti.
Mwanasheria kucertify cheti kimoja ni 20,000 bila hiyo hupati huduma. Sijawahi ona mwananchi analalamika.
Ukienda kwenye firms za wahasibu unalipa consultant fee, ukienda kwenye firms za Manunuzi unalipa. Sema wewe hujui. Na ni hujui kwasababu hizo huduma so kila mtu atataka. Na anayetaka hizo huduma ni mwenye pesa haoni shida. But huduma za afya ni mtakuja kuanzia masikini hadi tajiri lazima mje tu. Ndo maana vitu vidogo mnaona vikubwa but ukienda kwa mwanasheria kule au consultation kwaajili ya projects unalipa tu.
Na ukiona hivi ujue ndo umuhimu wa hiyo huduma. So chutama na omba iboreshwe
Ila afya mnaona ni kitu cha bure. Duniani kote huduma za afya ni very expensive ukisema uendeshe kwa hivi mnataka. Ipo siku utapakwa Mavi ya mgonjwa badala ya spirit.
If you think health is expensive try ignorance.
Sijatoa mfano huo ndo ukweli wa matumizi yake. Tena kwa serikali ndi6kabisa hiyo hela daktari hapati hata sent 1. Hiyo yote ni mapato ya serikali pure. Na matumizi yake ni kama nimetaja hapo ukiondoa mshahara kwa private.Mifano uliyotoa ni endapo umepata huduma hizo katika mfumo wa private.
Niambie sasa dr aliyeko payroll ya kodi yetu hiyo fee ya nini? Si kama pesa haitosh serkali iongeze kwenye mshahara yeye afanye kuhudumia kama mtumishi? Kama ilivyofanyika malipo ya gari kuingizwa kwenye mafuta.