Mhasibu wa Benki atekwa, achomwa petroli porini

Wanasema alikua church akaitwa nje

Don’t know how [emoji2368]
Ni hivi;

1. Kuna tetesi zinasema alikuwa amtambulishe mchumba wake kesho yake tu

2. Alivyokuwa kanisani alipigiwa simu na kwa jinsi Mzee alivyoongea ni kama hao watu wabaya waliiga sauti ya boyfriend wake.

3. Alivyotoka kwenda kuitikia wito wa aliyedhani ni boyfriend wake, ndio akatokomea mazima.

4. Martha alikuwa na fahamu mpaka akataja namba za baba yake, so yawezekana pia kabla hajapoteza fahamu kabisa alitoa abc kwa familia ndio maana Mzee anaongea kwa confidence kabisa

5. Wauaji ni watu smart sana, walijua kanisani kuna CCTV so wao walikaa nje mbali kabisa ili hiyo CCTV isiwaone wala kuona usafiri wao.

6. Martha aliachishwa kazi mwezi mmoja nyuma, yawezekana kulikuwa na uchunguzi unaendelea na Martha angeweza kuwa mtoa ushahidi muhimu kwahiyo.

7. Kwa Scenario ya mauaji haya, hii ni dhahiri sio wivu wa mapenzi ila ni mambo ya kazi. Wauaji ni Professional killers na lazima wamekodiwa na watu wenye mpunga mrefu kuficha traces zozote za ushahidi.

8. Branch Manager na staffs wa BOA Kahama kazi mnayo
 
Sahihi.. hii ngoma lazima ni watu wenye mtonyo mrefu wameifanya. Tena kumix alibi wamefanya kwa kutegeshea ishu za kutambulisha mchumba ili kupoteza watu maboya.

Ni dhahiri tangu anaachishwa kazi alikuwa akifuatiliwa kwa ukaribu sana huku mchongo wa kutolewa duniani ukifanyika
 
Huyu Martha Towa aliungua tarehe 3,March,akapelekwa hospitali. Amekufa tarehe 9. Kwa hiyo presumably alikuwa anazungumza na polish. And yet polisi wanasema hiki kifo ni utata mtupu.
Mkuu, umeshasema hapo kwamba "presumably"...that means inawezekana polisi walizungumza naye au hawakuzungumza naye. Lakini pia, zingatia kwamba ukiwa hai tena ICU haimaanishi kwamba ni lazima uweze kuzungumza, pengine alikuwa anapumua tu lakini hoi bin taaban.

Aidha, hata kama aliweza kuzungumza, ushahidi wa huyu mgonjwa hauwezi kuaminiwa kama ulivyo kwa kuzingatia hali yake. Lazima ushahidi huu uhusianishwe na ushahidi mwingine ili kuupa nguvu.

Sheria ni sayansi. Shahidi namba moja akishakufa huwa kuna mambo mengi ambayo yanafifisha uzito wa ushahidi wa watu wengine.

In criminal litigations the standard of proof is BEYOND REASONABLE DOUBTS. Ishu inakuja hapo kwenye kuthibitisha bila kuacha shaka. Ndiyo maana watuhumiwa wengi wa makesi ya namna hii huwa wanaachiliwa huru hata kama ni kweli wametenda kosa.
 
Nitaendelea kusema waafrika ni watu makatili kuliko jamii yoyote duniani, lakini sio wote makatili. Nisieleweke vibaya.
 
Inaitwa psychic investigation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…