Utafiti lazima kuna watakaokubali na wapo watakaokataa. Hata ukifanya utafiti wa walio tayari kufa, wengi watakataa ila wapo watakaosema wapo tayari.
Lakini ikitokea ukawa katikati ya kundi la wanaotaka kujiua wakati wa utafiti wako, utahitimisha kuwa dunia nzima inataka kujiua? Hizi ndo factors zinazopinga generalization.
Hoja ni kwamba, kundi la wanaokataa haliwakilishi kundi la wote waliobaki. Na hakuna njia sahihi humu JF ya kusema wanawake watakataa sababu sample inayotumika ni ndogo sana kuwakilisha wanawake wote.
Humu JF makundi yote ya wanawake hayawawezi wakilisha wanawake wa Tanzania. Labda tuseme wa JF.
Sasa, neno "mwanamke" likitamkwa halimaanishi mjini tu, JF tu, vyuoni tu, ni identity ya wanawake wote ndo maana nasema exception wakati wa kuleta hoja ni muhimu kama si lazima.
Mfano, Kuna kundi kubwa la wanawake huko porini wala halijui JF ni nini achilia mbali smart phone, na hili linawakilishwa na hawa hawa waliopo humu?