Miaka michache ijayo wadogo na watoto wetu wataoa makahaba wastaafu

Miaka michache ijayo wadogo na watoto wetu wataoa makahaba wastaafu

Wanaume ndiyo viongozi na wenye kuwa na mamlaka kwenye mambo mengi

Hii ishu mpaka inakuwa hivi tatizo ni la wanaume ambao hawajitambui ndiyo wanazalisha huo Malaya sijui ukahaba,

Huyo mubaba kinachomfanya asitulie na mkewe ni nn ??? Kuna wanawake Rika la huyo mubaba anaweza date nao ambapo Kuna wajane, watalaka, ambao wameachwa na chungu nzima ya kina mama,,

Ukweli naoujua mwanamke mwenye akili timamu akiona jambo haliwezi atajiengua

Mtu hujapata mkopo wa chuo, nyumbani hawana hela utaendaje chuo kichwa kichwa ?? Kama sio kwenda kudanga??

Maadili yanaweza kusaidia endapo mtoto husika anajitambua wapo watu wamelelewa kwenye familia Bora zenye ukwasi, za kati za chini hata masikini na wakawa na maadili Ila ikiwa alijivika ngozi ya kondoo hamna kitu

Binafsi sinunui mwanamke ana shida ntampatia hitaji na sio hela

Wakulaumiwa tunaanza na sisi me ndo wateja wao
Mimi nafikiri mwanaume awajibishwe kwa makosa yake na mwanamke awajibishwe kwa makosa yake, yaani rich simp ni mkosaji na gold digger ni mkosaji.

Tukitaka lawama zibebwe na rich simo pekee ake hii maana yake tunasema mwanamke hana akili, utambuzi wala utashi binafsi. Yeye anabebwa tu kama boksi analazwa kitandani anatombwa akiwa ajui chochote. Kitu ambacho sio kweli. Wanawake wana akili, ufahamu, utashi na wanaweza kufanya maamuzi binafsi(mema au mabaya) bila influence ya mwanaume

Rich simp na gold digger wote wana makosa, and two wrongs don't make it correct. Kwahiyo kila mmoja awajibishwe bila kurusha lawama upande mwingine.
 
Kuna mama fulani wa makamo anauza genge maeneo ya karibu na mtaani kwangu. Ni mama mcheshi kiasi. Huwa napita kununua matunda kwahiyo nimezoeana nae kidogo.

Wiki kadhaa zikizozipita, wikiend moja katika kutembea tembea mtaani kwangu kusalimiana na majirani. Nikafika gengeni kwake. Nikaagiza matunda. Wakati ananifungia kuna binti alitoka nyumba ya karibu akaelekea upande wa pili wa barabara. Nikamshangaa kidogo. Tukaanza mazungumzo sasa na mama muuza matunda.

Mimi: Huyu binti ni nani, anaishi hapa mtaani?

Mama: Ndio anaishi nyumba ile pale(akinionyesha kwa kidole). Ameamia juzi juzi tu hapa mtaani. Ni mwanafunzi kapanga chumba mule ndani. Kwanini unauliza? (huku akitabasamu)

Mimi: ni binti mrembo

Mama: ni binti mrembo sana, lakini ndio hajatulia

Mimi: unamaanisha nini?

Mama: unaona ile pikipiki imepaki pale nje, ni ya boyfriend wake aliempangia chumba pale. Ana mwanaume mwingine huwa anamletaga na gari. Kuna mwingine wa tatu huwa wanakutanaga mtaa wa pili uko. Hapo yupo mbio mbio si ajabu ndio anawahi kukutana nae.

Mimi: oooh.! ana maboyfriend watatu

Mama: unajua maisha ni magumu na yeye ni mwanafunzi. Anatakiwa kulipa kodi, usafiri, kula na mahitaji yake mengine. Ni hela nyingi na mwanaume mmoja anaweza kushindwa kumtimizia mahitaji yote hayo. Nafikiri mwenyewe unaelewa.

Mimi: inaonekana unakubaliana na huo mtindo wa maisha.

Mama: unataka afanye nini, na yeye ni mtoto wa kike yupo mbali na nyumbani.

Mimi: ungekua wewe kwenye nafasi yake ungefanya hivyo?

Mama: hapana hapana hapana. Sisi wakati wetu tulikua na maadili hata maisha hayakua magumu kama sasa. Tuliishi kijamaa unaweza ukaishiws chumvi na kwenda kuomba kwa jirani ila sasa hivi kila kitu utoe hela, ndio inachangia hawa mabinti kuishi haya maisha

Mimi: na miaka ya mbeleni kuna kijana atakuja kumuoa akiwa hajui haya yote.

Mama: ndio maisha kijana wangu. Kipya kwa mtu ni kichakavu kwa mwingine.

Nikatasamu 😀😀 na kuchukua matunda yangu. Tukaagana

Siku nyingine nikakutana na demu mmoja hivi nikiwa kaunta, akanipa story jinsi yeye na rafiki wanapata hela za kujikimu na maisha.

Kwanza alitaka kuniuzia. Nikamwambia huwa sinunua sex. Napendelea mwanamke mwenye choice, sio ambae yupo tayari kulala na mwanaume yoyote akipewa hela. Akaniomba basi nimnunulie kinywaji. Nikamwambia agiza. Akavuta kiti kirefu akakaa.

Binti: Maisha yamekua magumu sana hapa nahitaji hela ya kumalizia ada ya chuo(akanitajia hela ya ada anayodaiwa).

Mimi: Hiyo ni hela nyingi. Uliwezaje kulipa ada mpaka ulipofikia sasa hivi?

Binti: Nilivyoanza chuo nilikua na mubaba. Alikua ananilipia ada na ananipa hela ya matumizi. Mwaka wa pili tuliachana. Aligundua nilikua na mpenzi wangu. Baada ya hapo maisha yamekua magumu sana. Wanaume kwa sasa hawana hela. Ngumu kupata wa kukupa mahitaji yako yote.

Mimi: sasa ilikuaje ukaanzisha mahusiano mengine wakati tayari una mwanaune anaekuhudumia mahitaji yako.

Binti: huyo mpenzi wangu nilikua nae tangu sijakutana na huyu mubaba, na nisingeweza kumuacha kwa sababu ndie ninaempenda.

Mimi: ooh.! Kwahiyo ukaushi vipi sasa baada ya hapo?

Binti: (anaanza kwa kucheka) kuna siku rafiki angu alinipigia kuniambia amepata hela ya kulipa ada. Nikamuuliza umepata sponsor wapi uko. Akaniambia hakuna mwanaume huyo sasa hivi. Huko alipo kumer inawaka moto. Amelazimika kulala na wanaume kadhaa ili apate hela

Nikatabasamu kidogo halafu akaendelea na story.

Binti: hali sio hali yaani sasa hivi inabidi tuanze tu kuwalenga mpaka nyie waume za watu.

Mimi: umejuaje kama mimi nimeoa?

Binti: huwa tunanusa.

Nikacheka kidogo na kuangalia muda kwenye saa ya mkononi then nikainuka kwenye kiti. Tukaagana. Nikalipa bill yangu na yake. Nikamwambia achukue chenchi atapanda bodaboda akiwa anaondoka. Nikasepa.
Issue ya kuoa makahaba wastaafu, kimantiki aliimaliza kuiweka sawa yule mama muuza matunda... 'kipya kwako, kwa wenziyo kichakavu'...

Makahaba walikuwepo tangu enzi za Yesu Kristu na ushahidi wa simulizi za maandishi upo.

Makahaba wanaowasanifu sana wanaume ni wale wanaojifanya ni ghali, wametulia halafu ni walokole!

Hao wanakuwa wametega vibaya sana soko la ndoa.

Mwanaume anapaparika akidhani anaoa 'wautulie', na hivi hainaga makombo baba!
 
Matunda, perfume,karanga,ndizi, juice na other small business kwa wadada ni mtindo mpya wa kufanya umalaya hii utakufanya umuone hustle kumbe nyuma ya pazia kuna black 🐈‍⬛ prostitute.......
Usi-Generalise kuna wengine wako honest kabisa na business affairs zao.
 
Sisi hata tukikesha hapa jf kukemea hiyo tabia unayoiongelea lakini kama wanawake wenyewe hawaoni ubaya wa kuongwa tutakua tunafanya kazi bure
Sasa Mkuu kama suala la wao kuhongwa linawafanya baadhi yao kuishi maisha mazuri, wewe unaona kuna uwezekano wowote wao kulikemea hilo suala kama tatizo?

Ni sisi wanaume ndiyo tunatakiwa kuachana na hii tabia ya kununua mapenzi.

Mbona liko wazi hili.
 
Mimi nafikiri mwanaume awajibishwe kwa makosa yake na mwanamke awajibishwe kwa makosa yake, yaani rich simp ni mkosaji na gold digger ni mkosaji.

Tukitaka lawama zibebwe na rich simo pekee ake hii maana yake tunasema mwanamke hana akili, utambuzi wala utashi binafsi. Yeye anabebwa tu kama boksi analazwa kitandani anatombwa akiwa ajui chochote. Kitu ambacho sio kweli. Wanawake wana akili, ufahamu, utashi na wanaweza kufanya maamuzi binafsi(mema au mabaya) bila influence ya mwanaume

Rich simp na gold digger wote wana makosa, and two wrongs don't make it correct. Kwahiyo kila mmoja awajibishwe bila kurusha lawama upande mwingine.
Ni sahihi ndiyo maana nimeweka sisi ni chanzo akini pia wanawake baadhi wasiojitambua nao ni changamoto

Makosa yapo kwa wote mshua
 
Mimi nafikiri mwanaume awajibishwe kwa makosa yake na mwanamke awajibishwe kwa makosa yake, yaani rich simp ni mkosaji na gold digger ni mkosaji.

Tukitaka lawama zibebwe na rich simo pekee ake hii maana yake tunasema mwanamke hana akili, utambuzi wala utashi binafsi. Yeye anabebwa tu kama boksi analazwa kitandani anatombwa akiwa ajui chochote. Kitu ambacho sio kweli. Wanawake wana akili, ufahamu, utashi na wanaweza kufanya maamuzi binafsi(mema au mabaya) bila influence ya mwanaume

Rich simp na gold digger wote wana makosa, and two wrongs don't make it correct. Kwahiyo kila mmoja awajibishwe bila kurusha lawama upande mwingine.
Rich simp, Hahaha, inaonekana ukikutana na wale wazee wanalipia Mabinti kwenda Dubai akifika anamshika shika halafu anarudi anamuacha binti huko aendelee kuinjoy utapatwa na hasira sana.
 
Sasa Mkuu kama suala la wao kuhongwa huwa linawafanya baadhi yao kuishi maisha mazuri, wewe unaona kuna uwezekano wowote wao kulikemea hilo suala kama tatizo?

Ni sisi wanaume ndiyo tunatakiwa kuachana na hii tabia ya kununua mapenzi.

Mbona liko wazi hili.
Anapendekeza Malaya akatae pesa na akemee wengine wasichukue.
 
Zamani wanaume walikuwa free kwenye sex na wanawake wakiiona kama taboo. Mambo ya kutunza bikra na kutokutumika.

Leo hii watu hawaulizii bikra ila wanaangalia kama binti ana mtoto.

Hii ikupe picha tu, ule mstari ambao jamii uliiweka au kupandikiza ideologies kuwa sexual freedom kwa wanawake ni mbaya sana. Umeshaanza kufutika na kwa sasa hata bila pesa. Wanawake wengi wameanza kuchukulia sex kama fun pia kwa hiyo unachokiona ndicho kitakachotokea
Ngono ni kawaida tu. Shida ni kujiuza. Mpaka mtu anaamua kujiuza, kuna namna anakuwa hajithamini. Ni wapi anapaswa afundishwe kujithamini? Ni nyumbani!

Mimi naona malezi ya watoto wa kike yaliyopo hayawezi kuwasaidia karne hii. Wanakwezwa sana. Wanapewa upekee wasio nao. Misemo kama; "Mimi mtoto wa kike nashindaje njaa" inahuzunisha sana na kuchekesha zaidi.
 
Mkuu tatizo lako una confirmation bias sana, Ku-generalize ni vibaya sana maana mada inaoenekana haina mantiki tena, hata kama tatizo ni kubwa kwa 90% still bado kuna hiyo 10%.

Mfumo wa kuhonga umekithiri sawa, unaweza kuniambia ni nani anayeufanya huo mfumo ukithiri?

Kuna kundi kubwa sana la wanaume ambao huwa wanatoa pesa ili kupata hizo huduma tena huenda wakawa wengi kuliko hao malaya wenyewe, huoni kama na wao wanachochea hiyo tabia kushamiri?

Mbona hausemi kuwa wanaume nao wamekaa kikao cha kutaka kununua mapenzi ili kuwafanya wanawake wawe bidhaa? kwanini unaona kuna tatizo kwa upande wa wanawake tu?
Kwenye kuwasilisha hoja huwa tunafanya generalization. Nilishawahi kukuambia "there is exception in everything, but exceptionality don't count when we generalize"

Pia huwa mnakosea sana kunitaka mimi niandike kwa flow mnayoitaka. Jf ni jukwaa huru kama kuna maeneo mimi siyagusi hata nyie mnawezav kuyaandikia thread. Sio lazima kila angle iguswe na Natafuta Ajira.
 
Mimi nina mawazo tofauti na Wanaume wenzangu. Naamini ni bora kuoa kahaba mstaafu kuliko kuoa bikra anayetegemewa kuwa kahaba akiwa ndani ya ndoa. Ndo maana naamini ndoa ni kwa binti ambaye amemaliza ya duniani na kuamua kupumzika kujenga familia (30+) na mwanaume ambaye ameshatuliza wenge 35+ ili ndoa iwe ni kimbilio la wote.

Ndiyo maana nasemaga ngono ni asilimia chache katika ndoa. Ngono isiwe ni msukumo mkuu wa kufunga ndoa. Ndoa itokane na hitaji la mwenzi, rafiki na ndugu wa maisha yako yote.
 
Nimekuelewa Mkuu.
 
Hahaha, kwa hiyo mkuu unaona kabisa its ok ukioa kahaba aliyeacha ukahaba huku ukijua alikuwa kahaba?
 
Back
Top Bottom