Lily Tony
JF-Expert Member
- Feb 6, 2019
- 3,198
- 4,191
- Thread starter
- #81
Kaka miti asante kwa pongezi na kuni appreciate.Mama miti kwanza hongera upo vizuri!
Nahitaji miche ya cadamia ila nipo mwanza nina wasiwasi kama itastawi vizuri maana naiona sana lushoto milimani huko kwenye baridi halafu huku sijawahi kuiona. Nahitaji ushauri wako Mama miti.
Mimi ni mwenyeji wa Lushoto milimani hivyo zao hili ninalifahamu vizuri,lipo sana maeneo ya Sakarani kwa mapadri😊.
Zao hili lina soko sana hasa kwa nchi jirani ya Kenya,,kg 1 ya kadamia ni sh elfu 20 na hata mafuta yake yana soko.
Kenya pia zao hili lipo lakini wanapendelea zaidi mali ya Tz sababu Cadamia za Tz zinalimwa bila kutumia madawa,ni za asili na zina mafuta mengi.
Cadamia zinastawi maeneo yenye baridi na mvua za kutosha,pia ardhi iwe na unyevu.
Miche yetu inaanza kuzaa baada ya mwaka 1 mpaka miaka 2.
Karibu sana boss wangu