bachelor sugu
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 2,689
- 3,651
Ila kiukweli hata mm nina gundu na mikeka ya watu mpaka nilishaacha kutembelea mkeka wowote naouona huwa nashuhudia tu Won won ila nikijipanga niruke nayo lazima niliwe kichwa.Nilikuwa naona Professa akiweka humu mikeka yake, siku moja nami nikasema acha nijiunge Meridian nipige pesa kupitia nyota yake.
Akaweka mkeka wa kwanza nikakopi na kupaste, mwisho wa matokeo ikawa ndo hivyo tumepoteza. Nikapiga moyo konde nikaweka tena mwingine alioweka pia ikawa ndo hivyo.
Akakaa kama siku mbili hajaweka mkeka, siku alipoweka nikaruka nao ila wapi ni mwendo wa kupigwa tu. Mwisho nikasema acha nifanye yangu. Nikaanza kubet mwenyewe kwa mawazo yangu nikawa nakula muda mwingine napigwa.
Jana nimekaa na kusaka pointi 15 na zikawin, leo nisaka 22 najua zitawin.
Kwa sasa hata nione humu fixed match siwezi kukopi nitakomaa na akili yangu.
Na wewe unayeleta humu mkeka omba nisiukopi [emoji23] [emoji23] [emoji23].
Anyway ni imani tu wala hakuna mwenye gundu ktk hili ni upepo tu ukikaa vibaya.
ODDS 10 hizo mwenye imani na atembee nazo wenye pressure tuziangalie kwa macho tu tykutane Lumumba aka Kijanini.