Mikeka: Wazee wenzangu wa kuweka mzigo, karibuni tubashiri mechi za leo

Labda kama kuna faida unayoipata huko sawa endelea kukomaa mpaka kieleweke ila kiukweli paripesa cyo binafsi nilifuta li-app lao... na kuna Salio niliwaachia maana huko kutoa na kuweka ni kisanga,

Ila kama kweli uko siliazi na pesa unatia kweli na cyo demo akaunti hebu onyesha upendo kwa wadau kwa kuingia kwenye kampuni zenye kueleweka!!!

Ila kama ni demo akaunti sawa komaa ila unawaumiza watu mmoja wao ni mm na siongei kinafki
 
Haya nitajie kampuni za mrusi ambazo hazina changamoto na za kueleweka zaidi ya 1xbet, PARIPESA, Helabet, Betwinner, 888STARZ, melbet nk. Ambapo kwenye kampuni hizo zote hapo juu nazitumia kubetia. Ukinitajia ambayo huwa haina changamoto kwenye suala la malipo nitajiunga nalo rasmi leo hii, na Deposit na kuanza kuleta Code zake hapa.
 
Mkuu kwani mpaka leo hujatoa hela yako? Mbona kuna wana wengi tu humu walikumbwa na changamoto za kutoa hela wakavumilia na wametoa hela zao? Mkuu labda kama una changamoto nyingine. Ila usijali mkuu tuombeane kheri na tuendelee kumpiga kanji.
 
Parmatch
 
Mkuu Paripesa HAIPO Tz kwasababu haijasajiliwa kufanya biashara Tz, haina vibali vya kufanya biashara hiyo hapa Tz na wala haina ofisi hapa Bongo kama ilivyo 888starz, 1xbet, 22bet
Hizo njia za kuweka kwa Mobile payment ni janja janja tu ndio maana leo zipo kesho hazipo.
Sio kwasababu unaweza ku access online basi ukadhani ndio inaruhusiwa kisheria...... hapana
Lazima isajiliwe, iwe na ofisi na domain name lazima iwe .co.tz na sio .com or whatever

Angalia kampuni kama Betpawa, Betway, Wasafibet Betika, mkekabet nk nk
Zote zina ofisi bongo zina tumia .co.tz na ni lazima ziweke namba za usajili wa bodi ya bahati nasibu Tz kwenye website zao, na wakikudhulumu unakwenda kuwashitaki bodi na unapata haki zako

Paripesa kama inafanya vizuri Nigeria ni kwasababu imesajiliwa huko kihalali na inafuata sheria za huko lakini sio Tz

Katika kampuni zote za Mrusi angalau mwenye unafuu ni 1xbet ukitumia wakala muaminifu ingawaje nayo bado ni njia ya panya vile vile.... unaweza kushinda parefu na hawakulipi na huna pa kwenda kuwashitaki maana wanafanya biashara kimagendo nje ya utaratibu

Kama nia yako ni kutoa TIP za ushindi basi endelea hilo ni jambo la kheri kabisa, lakini kama nia yako ni kuwafanya wajiunge huko waje kutapeliwa kisa unapata cha juu acha huo uhuni
 

Attachments

  • 943EEF44-FF2D-499D-9436-360B2E5F5204.jpeg
    141.6 KB · Views: 2
  • 04355124-3081-4974-A55F-13D4AD05D3F8.jpeg
    132.1 KB · Views: 3

Hii Hapa Mkuu ipo Tanzania. Mwezi uliopita kama unakumbuka ilikuwa kama ukishinda kuna makato ya kodi ila baada ya kushauriwa waliongea na serikali kodi ya makato ya ushindi wanalipa wao.
 
Mkuu nia ni kumpiga kanji. Na kuna siku TUNASHINDA na kuna siku tuna lose kama ambavyo kila mmoja hupitia.
 
Hii Hapa Mkuu ipo Tanzania. Mwezi uliopita kama unakumbuka ilikuwa kama ukishinda kuna makato ya kodi ila baada ya kushauriwa waliongea na serikali kodi ya makato ya ushindi wanalipa wao.
Mkuu ndio maana nasema haya ni makampuni ya kitapeli
Hao wahuni hawajasajili Tz isipokua wemeweka kiunganishi fake cha .co.tz kwenye search na wakati uki bofya hiyo link inafunguka .top na sio .co.tz

Hebu soma hapo uone hiyo kampuni imesajiliwa wapi ?
 

Attachments

  • 6E5618A0-749A-484D-9758-04BFE3052CCA.png
    189.5 KB · Views: 5
Nimegonga nao ung'eng'e wa kutosha naona hata wao PariPesa hawana majibu kama wapo kihalali Tz au la!
Hivyo muwe makini na hela zenu mlizo ziweka huko, hawakawii kusema "this website is currently not available in your region"
 

Attachments

  • Screenshot_20241019-085618_PariPesa.jpg
    171.7 KB · Views: 6
Mkuu nia ni kumpiga kanji. Na kuna siku TUNASHINDA na kuna siku tuna lose kama ambavyo kila mmoja hupitia.
Mkuu tuufunge huu mjadala

Binafsi napenda mtu anayetoa tips zinazo wasaidia wakamalia kama unavyofanya wewe

Lakini sipendi kuona mkamalia anaingizwa kwenye matatizo zaidi wakati ku win bet tu ni kipengele halafu akitaka kutoa hela yake anaanza kuzungushwa

Mimi nimetoa angalizo ili huko mbeleni mtu ajue anazitumia hizo kampuni akijua KASORO zake na kupunguza malalamiko ya kuuliza hapa mbona hela zangu hazijafika

KAZI IENDELEE watu waendelee kumwaga tips sasa ligi zimerudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…