Millennials ndio Kizazi kilichofeli zaidi katika malezi ya watoto

Millennials ndio Kizazi kilichofeli zaidi katika malezi ya watoto

Tafuteni majina yenu jamani haya majina Millennials, Gen-Z, Gen X, Baby Boomers, The Silent Generation etc ni majina ya Kimarekani yanayofuata historia yao, mambo yao, timeline yao.

Unaweza kutumia neno hilo la generations za Kimarekani kuwaita Watanzania halafu ukaliharibu kabisa kwa sababu linakuwa halina sifa zile zile za Wamarekani wenyewe.

Kwani huko Tanzania hakuna vitu vyenu, hamna historia yenu, hamna timeline yenu, hamna vyenu vya kuita vizazi vyenu mpaka mviite vizazi vyenu kwa majina ya Kimarekani?
Kizazi cha Mwalimu/Ujamaa-Waliozaliwa Nyerere akiwa rais.
Kizazi cha ruksa/soko huria; 1985-1995
Kizazi cha ubinafsishaji; 1995-2005
Maisha Bora; 2005-2015
Kizazi cha miondombinu na wasiojulikana; 2015-2025
Kizazi cha October 29/Uchawa: 2025-
 
Nakubali , ila Kuna muda inatakiwa urahisishe mambo ili uleweke kwa haraka na wabongo 😂

Barubaru nadhani imetoka kwa Wagiriki neno "Barbaroi" kumaanisha non Greek ambao walikuwa wanawaona kama uncivilized , likaja Afrika Kuna jamii ikawa inaitwa 'Berbers' Wazungu wakawa wanaita 'barbarians' watu wasiostarabika. Ikaja Swahililand ikaitwa "barubaru"

Hizo assumptions zangu kuhusu "barubaru" kama Kuna makosa nisahihishe
Sijui kuhusu exact etymological chain, ila ulivyoelezea ina make sense.

Kwa sababu katika Kiswahili Barubaru ni kijana mdogo mwenye nguvu, aghalabu kijana aliyepata balehe karibuni, anayeweza kutumia nguvu zaidi kuliko akili pengine. Kwa hivyo kuna namna ya kuendana na ulivyosema. Ila ni kijana, wa kiume, ambaye ndiyo kwanza kapata balehe, mwenye nguvu, mwenye kuweza kutumia nguvu zaidi ya akili, kwenye lahaja nyingine neno linahusiana na Varuvaru. Rough. Barbarian.
 
Gen Z bongo ana soma na kibatari 😆
Style yetu naona iwe
-Watoto walio zaliwa kipindi cha Kikwete
-Watoto walio zaliwa kipindi cha jiwe
-Watoto walio zaliwa kipindi cha kazi na utu kipindi cha elninyo ya jua na joto kali etc
Sisi Bishoo Nyangema anajiita 2Pac 😂😂😂
 
Moja kwa moja ;

Tunapozungumzia Millennials tunamaanisha wale waliozaliwa kuanzia 1981 mpaka 1996 , kumekuwa na trending ya kulaumu watoto katika mmomonyoko wa maadili na kusahau chanzo kikuu ambacho ni wazazi wao .

Millennials wengi ndio wamezaa watoto waliozaliwa kuanzia 2010 walioanza mapema ni 2005 ambao ni wachache sana . Na ukiangalia trending kizazi kilichopinda zaidi ni cha watoto wa kuanzia 2005 to 2010 na kuendelea .

Ukiacha mambo ya utandawazi na mitandao ila kiukweli Millennials wengi wanalea watoto kizembe sana , unakuta Mzazi na mwanae kama mtu na Shoga yake hakuna mipaka wala kumuogopa Mzazi kama zamani wao wako bize kwenye utafutaji kufuatilia malezi ya watoto , kugundua matatizo mapema na kuyatibu hawana muda huo .

Hiki kizazi cha 2010 ni balaa mtaani kwangu tu Kuna vibinti vidogo single mothers sidhani kama wamevuka hata miaka 20 , na kwa haraka haraka wapo kama 9 hivi wanalea sasa , wengine wanepata ujauzito wakiwa sekondari , wengine baada ya kumaliza la 7 , wengine baada ya kumaliza form 4 na wote hao wazazi wao ni millennials , kwa upande wa Kiume hapo wahuni na wavuta bangi ndio wamejazana wengi ponapons yao wamekimbilia kuwa bodaboda .

Millennials unakuta Mzazi anafurahi na hasemi kitu ndani ya nyumba yake watoto wamejaza nyimbo za hovyo za bongo fleva na Singeli zilizojaa matusi na uhuni mwingi zinabondwa tu na wakati mwingine wakiwaimbisha watoto wao , hapo bado upande wa movies tamthilia zenye maudhui mabaya ya umbea , kuhamasisha ngono nk . Niliwahi kuanzisha mada athari ya hivyo vitu katika kuharibu akili ya watoto na maadili.

Sisi ambao wazazi wetu hawakuwa Millennials ilikuwa tukifanya kosa mtu unatetemeka mpaka kurudi nyumbani unaogopa wazazi hawafagilii ujinga , Millennials wao mtoto ni mfalme .

Nina mengi ila kwa Leo niishie hapo

#UziTayari
Watoto wengi waliozaliwa 200-2015 ni zao la silent generation na few millenials. Usitulaumu kwa makosa ya wengine. Watoto wetu wengi wanaanzia 2015 kuja mbele.
 
Ukiyakuta sasa yana kejeli/Laumu kizazi cha 2000 lazina ushangae.

Like, Its your sons and doughter, N You failed to raise them as a parrent.
 
Tafuteni majina yenu jamani haya majina Millennials, Gen-Z, Gen X, Baby Boomers, The Silent Generation etc ni majina ya Kimarekani yanayofuata historia yao, mambo yao, timeline yao.

Unaweza kutumia neno hilo la generations za Kimarekani kuwaita Watanzania halafu ukaliharibu kabisa kwa sababu linakuwa halina sifa zile zile za Wamarekani wenyewe.

Kwani huko Tanzania hakuna vitu vyenu, hamna historia yenu, hamna timeline yenu, hamna vyenu vya kuita vizazi vyenu mpaka mviite vizazi vyenu kwa majina ya Kimarekani?
Kumekuchaaa 😂😂😂
 
Ukiyakuta sasa yana kejeli/Laumu kizazi cha 2000 lazina ushangae.

Like, Its your sons and doughter, N You failed to raise them as a parrent.
Ndio Kizazi chenye kutumia matusi zaidi kuwakanya watoto . Hawaoni aibu kutukana mbele ya watoto wakati kizazi cha 55 -75 ni mwiko kutukana mbele ya watoto
 
Kizazi cha Mwalimu/Ujamaa-Waliozaliwa Nyerere akiwa rais.
Kizazi cha ruksa/soko huria; 1985-1995
Kizazi cha ubinafsishaji; 1995-2005
Maisha Bora; 2005-2015
Kizazi cha miondombinu na wasiojulikana; 2015-2025
Kizazi cha October 29/Uchawa: 2025-
😂😂😂😂 umetisha sana, Lol
 
Kumekuchaaa 😂😂😂
Sasa watu wamepigana vita zao, wakavipa vizazi vyao majina yao kutokana na vita zao.

Na sisi tunataka kudandia majina yao hapohapo kama tuna fit kwenye historia yao jamani?

Kwani sisi hatuna mambo yetu na vita zetu?

Hili jambo nalo tutasema ni gumu sana linahitaji wawekezaji wa nje na fedha za kigeni?
 
Una nini lakini? 😂😂😂
 
Tafuteni majina yenu jamani haya majina Millennials, Gen-Z, Gen X, Baby Boomers, The Silent Generation etc ni majina ya Kimarekani yanayofuata historia yao, mambo yao, timeline yao.

Unaweza kutumia neno hilo la generations za Kimarekani kuwaita Watanzania halafu ukaliharibu kabisa kwa sababu linakuwa halina sifa zile zile za Wamarekani wenyewe.

Kwani huko Tanzania hakuna vitu vyenu, hamna historia yenu, hamna timeline yenu, hamna vyenu vya kuita vizazi vyenu mpaka mviite vizazi vyenu kwa majina ya Kimarekani?
Mambo mengi tumeiga, mengi tunafanya kwa sababu tunaacha vya kwetu, hatujui vya kwetu au hatuna uwezo wa kuwa na vyetu.

Hili la majina naona ni dogo tu, kama lina athari basi ni kidogo tu.
 
Rafiki yangu dini zimeshindwa kabisa kutengeneza jamii yenye maadili mazuri, watoto wote wenye tabia za kishenzi wanatokea ukanda wa watu wanaojiita washika dini

Lakin ukienda jamii za kifugaji kama wasukuma watoto wa huko bado Wana maadili mazuri sana
 
Mambo mengi tumeiga, mengi tunafanya kwa sababu tunaacha vya kwetu, hatujui vya kwetu au hatuna uwezo wa kuwa na vyetu.

Hili la majina naona ni dogo tu, kama lina athari basi ni kidogo tu.
Kuna mambo unaweza kuyaona madogo, lakini kifalsafa, kisaikolojia, ni makubwa sana.

Yana establish dominance, deep kwenye mawazo kabisa mnajikataa kuwa katika dunia hii, nyie si watu kama Wamarekani.

Yani mmepewa uhuru fulani, lakini mmekuwa kama yule kuku ambaye ameshazoea kufungwa kamba kwa muda mrefu, hata kamba ikikatwa anabaki palepale kashazoea hali ya kufungwa kamba.

Leo mmewaweka juu kama mwenge.

Halafu kesho mnakaa nao mezani hao Wamarekani, mna negotiate mkataba.

Watawapiga tu.
 
Kwa mantiki hiyo, waafrika(watanzania) turudi mezani tuanze upya maana kama ni hiyo dominance na nguvu tulishawapa, walishaichukua, wanaitumia kwa namna ambayo hata tukimbie marathon wao wakiwa wamelala fofofo bado hatuwafikii.

Nini ambacho tunajivunia kama taifa, Nyerere alisema hata bei ya korosho wanapanga wao. Tunajivunia nini!
 
Back
Top Bottom